Usifanye kosa hili kwenye mapenzi, utajuta daima. Utageuka kuwa chizi uropoke peke yako barabarani

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,119
Najaribu tu kuukumbusha ubongo wako kidogo, jambo dogo ila ndio source ya mambo yote mabaya katika ndoa au mapenzi.

Usiwe na mahusiano ya kimapenzi na mtu unayempenda wewe huku hujajihakikishia kuwa anakupenda pia au la.

Kuwa katika mapenzi na mwanamke au mwanaume anayekupenda na si unayempenda. Ikitokea na wewe umempenda pia itakuwa vizuri zaidi.

Usiuruhusu moyo ukutawale kwenye mapenzi, moyo utakupeleka direct kwa mtu unayempenda bila kujali anakupenda au la na mwisho wa siku utajikuta umeumia.

Kuna nyuzi nyingi za vijana kufanyiwa upumbavu na wapenzi wao humu ndani. Hii inatupa picha kuwa wamependa na hawajapendwa.

Upendo ndio utamfanya mwenzako akuonee huruma na si kukufanya ATM machine kila siku.

Upendo ndio utaleta msamaha toka kwa mwenzi wako pale utakapomkosea.

Upendo ndio utamfanya mwenzako asikucheat hovyohovyo.

Upendo ndio utamfanya mwenzako akusikilize mnapopanga mipango yenu ya kiuchumi.
 
mwanzo nilijua mwanamke akikupenda hakusaliti hata kidogo

nilijidanganya sana
mkuu kinacholeta usaliti ni tamaa na mtu anaeza kusaliti japo bado atabaki anakupenda, hata sie wanaume huwasaliti tunaowapenda bt bado huendelea kuwapenda.
 
Ukiacha Mungu na wazazi, siku zote unapendwa na watu walio chini yako... na wewe unapenda walio juu ya viwango vyako.

Umeelewa hapo!

Hii ndo sababu ya kila mtu kusaka kilicho bora kwake, kilicho juu yake... ukitaka 'wanaokupenda' basi ukubali kupokea chini ya kiwango maana ni mara chache mno aliyekuzidi akawa anakupenda bila kutia juhudi zako.
 
Hii nayo point,lakin mim bado npo kwa mtoa Uzi,ukitaka uishi kwa amani inabid umpende anaekupenda,usilazimishe kupendwa
 
mkuu kinacholeta usaliti ni tamaa na mtu anaeza kusaliti japo bado atabaki anakupenda, hata sie wanaume huwasaliti tunaowapenda bt bado huendelea kuwapenda.
Mimi ukishanisaliti nahesabu hakuna upendo hapo...kwa maana upendo hauumizi,haufanyi mambo yake yenyewe wala hauna mawaa yeyote yale..
 
Mimi ukishanisaliti nahesabu hakuna upendo hapo...kwa maana upendo hauumizi,haufanyi mambo yake yenyewe wala hauna mawaa yeyote yale..
mkuu usaliti na upendo ni mbingu na nchi, havina mahusiano eti mtu akikusaliti basi hakupendi no, mtu anasaliti anaposhindwa kuidhibiti tamaa ilomshika, na hili linatokea coz sie binadam si wakamilifu means kukosea ndo ukamilifu wetu.
 
ndio maana nikasema MIMI
 
Back
Top Bottom