Usidharau wazazi wako wao ndio walipanga wewe uje Duniani

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,161
15,835
Usije ukadharau wazazi wako mkuu, Wazazi ni watu wazito katika maisha yako,hakuna mwenye mwisho mzuri kwa kuwadharau wazazi wake, hiyo ndo kanuni ya ulimwengu.

Jiulize tu kuwa hapa duniani ulipo ulitaka mwenyewe uje au umekuja kwa sababu wazazi wako ndo walipanga uje?

Kama hukupanga wewe kuja hapa unadhani kuwa aliepanga wewe uje atafurahi kuona haumjali wala kumthamini?

Eti unasema una mambo mengi huwezi kuwasaidia wazazi wako,yani umepelekwa ugenini na waenyeji alafu unataka ujifanye ushaujua mji tayari, heshimu wazazi.

Unajua kuwa wazazi kibao wanatoa mimba lakini wazazi wako wakakukaushia uje nawe ushangae hapa duniani?

Unaposubiri mzazi akuombe ndo umpe unadhani na wao wangesubiri wewe uombe kuzaliwa ungekuepo?

Unaposema mzazi anaomba hela sana,msumbufu,analeta umasikini kwa kukutegemea wewe mtoto kwani wao hawakuona kuwa wewe mtoto wanaekuleta duniani kuwa utaleta umasikini?

Unaonaje wewe kuwahudumia watu ambao wanajjilea wenyewe na vile wao kukuhudumia wewe ambae pia wanakulea.

Usisubiri mzazi akuombe, msaidie mzazi uongeze furaha katika maisha yako.

Pesa ni takataka tu ambayo imepewa thamani na watu, thamani ni chakula mavazi na malazi.

Hakikisha wazee wako wanakula, wanavaa na kulala salama.
 
Usije ukadharau wazazi wako mkuu, wazazi ni watu wazito katika maisha yako,hakuna mwenye mwisho mzuri kwa kuwadharau wazazi wake,hiyo ndo kanuni ya ulimwengu.

law of nature Na amri ya Mungu. waheshimu wazazi hupate miaka mingi na heri duniani
 
Na nyie wazazi acheni kuzaa ovyo ovyo wakati Hauna hata uwezo wa kulea katika maisha bora. Unazaa mtoto bila kumpa msingi wowote Wa kumuendeleza halafu unatengemea akupe hela!? Mpe mtoto msingi Wa maisha ili baadae mtegemee
 
kwani wao si waliitaji mtoto ndio wakanizaa mimi, kwani kunizaa kwao ilikuwa ni msaada kwangu kwamba wasingelinizaa ningesikitika, kuzaana ni wajibu wa viumbe wote haijalishi mtoto ni msaada kwako au la. Hata virusi vya korona wanazaana
 
Back
Top Bottom