Usidanganywe Ukatega dawa ya kumnasa Mchawi aumbuke hadharani. Nakuhakikishia Baraza la Wachawi nchi nzima watakukalia kikao wakuondoe fasta!

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,444
2,000
Fanya yote ufanyayo!

Lakini usidanganywe ukathubutu kuweka dawa ya kumnasa mchawi ili Wananchi wamwone hadharani kuwa kanasa na mapichapicha Wamchukue!

Ndugu, nakuhakikishia ukitoboa kwenye kikao Cha pannel ya wachawi sijui!

Sababu ya kukuondoa!
Uchawi ni chama Kama vyama vingine! kila mwanachama huwa Ni lazima atembee kwenye CODE za kichawi kulingana cheo chake.

Mchawi Ni Kama mwanajeshi wa Jeshi lisiloonekana, Hivyo Unapomuabisha hadharani unakuwa Kama umeua mwanajeshi akiwa na sare za jeshi, unakuwa umevunja miiko yote ya wachawi! Kwahiyo lazima wakuondoe tu hakuna namna.

UNAYORUHUSIWA KUMFANYA MCHAWI
Tiba nyingi za kichawi ni:

Kuzuia, Kinga, au Kama unaadhibu mpige kombora akafilie mbali, au umpige kombora aache damu pale uone, ila yeye akafie mbele huko! (hii ni fair play katika ulimwengu wa giza)

Lakini kumnasa mchawi hadharani ready -handed yaani laivu Ni sawa na kushika mpira ndani ya 18 box, kinachoamuliwa pale ni matuta (penalty).

Mchawi huwezi kumtambua kirahisi, mchawi ni kama Corona, hafi kwa nyundo.
  • Ebu waza Leo ukamnasa mtu maarufu aliyekatiza kwenye anga zako inakuwaje na mapicha picha
  • Ebu waza leo ukamnasa waziri au mkuu Sana akiwanga na mapicha picha ukampiga!
  • Ebu waza viongozi wa taasisi kabisa wanavyoheshimika itokee umemnasa laivu akiwanga!
  • Ebu waza umnase mtu aliyejivika uchungaji wa kabisa!
Hivyo lazima wakuondoe na wewe ili usiwaharibie!

Waganga na wachawi wanajuana! Ukijidai umepewa dawa Kali na mganga wako, kwenye kikao Cha wachawi wakikutana lazima atapatikana mchawi nguli zaidi piga ua lazima wakuondoe!

Halafu usichojua ni kwamba, kila dawa Ina asili, ni kama risasi ukiitumia kuua, wataalam wakiokota wanaweza kujua silaha uliyotumia!

Tumia dawa zote za kuzuia, kufukuza au kuumiza akafie mbele kwa mbele lakini Usithubutu kumnasa LAIVU Mchawi! Vinginevyo ujipange kwa Vita!

NOTE! Katika hili Namaanisha kwa MCHAWI siyo kwa MWIZI

***MWIZI RUKSA KABISA KUMNASA LAIVU ***
 

Loftins

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
7,554
2,000
Hamna dawa ya kumnasa mchawi na hakuna baraza la wachawi stop fooling wasiojua.

Kuna dawa za kumjua anayekuroga/aliyekuroga, aliyeharibu mambo yako, aliyemchukua mkeo, anayemuharibu mkeo/mumeo n.k ila si hivyo unavyofikiri.

Mathalani Mganga ana uwezo wa kumfanya mchawi akose nyumba yako, asahau lengo aliloliijia nyumbani kwako n.k

Mchawi ni destroyer, na Mganga ni destroyer msaidizi.

Ahsanteni Naitwa Loftins
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,444
2,000
Hamna dawa ya kumnasa mchawi na hakuna baraza la wachawi stop fooling wasiojua.
.
Kuna dawa za kumjua anayekuroga/aliyekuroga, aliyeharibu mambo yako, aliyemchukua mkeo, anayemuharibu mkeo/mumeo n.k ila si hivyo unavyofikiri.
.
Mathalani Mganga ana uwezo wa kumfanya mchawi akose nyumba yako, asahau lengo aliloliijia nyumbani kwako n.k
.
Mchawi ni destroyer, na Mganga ni destroyer msaidizi.
Ahsanteni Naitwa Loftins
Sasa akikosa mlango wa kutoka maana yake Ni nini ...au kwako kiswahili Cha kunasa umekielewaje!?
Anaweza akawa anapita lakini anapofika eneo lako umetega Mambo yako dish linayumba ana nasa
 

Bess

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
389
500
hao watunguaji wenyewe Ni wanachama!
..........
Halafu tambua hili ,Kama yesu alikutana na shetani laivu akamwachia aende zake!
we Ni Nani hadi umshikilie Mchawi!
jaribu uone!
Acha kutisha watu, kama vipi katisha mbele ya mlokole, sio mlokole jina bali aliye na chata ya damu ya mwanakondoo wa Mungu
 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,629
2,000
hao watunguaji wenyewe Ni wanachama!
..........
Halafu tambua hili ,Kama yesu alikutana na shetani laivu akamwachia aende zake!
we Ni Nani hadi umshikilie Mchawi!
jaribu uone!
Kama watunguaji ni wanachama,Sasa kwann mwanachama A amtungue B..
Huyo B si angejikaza tu🤔

Nijaribu uone wkt umekuja ku surrender hapa kwamba mnatunguliwa..
Hapa si kujaribu uliza wenzio walitunguliwaje wakaaibika na ww ukasikia na kuja kulialia kwamba wachawi watakaa nchi nzima,ili kumroga mtunguaji.
😅😅😅
Dalili za uoga,Eti jarbu uone.
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,444
2,000
Eti wachawi wanajuana ahahahaha wewe kacheze unakochezaga bana wachawi hawana chama wala taasisi wala vicoba.
.
hata ukiona waganga wa jadi wana chama kimbia hao sio waganga ni waganga njaa tu wanabahatisha.
Sibishani na mpumbæv! kwani huko kwenu hakuna wachawi! Tega uone
 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,629
2,000
hao watunguaji wenyewe Ni wanachama!
..........
Halafu tambua hili ,Kama yesu alikutana na shetani laivu akamwachia aende zake!
we Ni Nani hadi umshikilie Mchawi!
jaribu uone!
Kama watunguaji ni wanachama,Sasa kwann mwanachama A amtungue B..
Huyo B si angejikaza tu🤔

Nijaribu uone wkt umekuja ku surrender hapa kwamba mnatunguliwa..
Hapa si kujaribu uliza wenzio walitunguliwaje wakaaibika na ww ukasikia na kuja kulialia kwamba wachawi watakaa nchi nzima,ili kumroga mtunguaji.
😅😅😅
Dalili za uoga,Eti jarbu uone.

Soma hii..
Luka 11:21-22
Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama;
[22]
lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang’anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.

Ndio maana wababe tuna wahamisha mitaa wanga/wachawi/walozi.

Ndio maana tunafunga anga, wanga wakipita wanaishia kudharirika.
Wanakua mateka wetu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom