Usidanganyike, Ni muhimu kwa Vijana kuwa na URAFIKI na jinsi tofauti

LENDEYSON

JF-Expert Member
Sep 27, 2013
2,996
2,659
Sijui Kama heading nimeiweka vizuri ila naamini mtanielewa tu.
Kuna ushauri hutolewa na wazazi, ama walezi, na pia Viongozi wa Dini, kuwakataza Vijana wa kike na kiume kuwa na "URAFIKI"( yaani Boyfriend na Girlfriend).
Hii sii sahihi, Madhara Yake nimeyaona. Mimi Ni victim katika Hili. Nimejizuia kwa kufuata ushauri Kama huo, nimesoma nimemaliza, nimekuja uraiani, kwenye Maisha halisi, mapenzi yakaanza kunivurugia ukubwani, baadhi ya vitu vidogo tu unashindwa kuvielewa kutoka kwa mwenzako, mnaishia kuachana, unabaki unaumia tuuu.

Niseme wazi, mapenzi yanawaumiza Sana waliokuja kuyaanza ukubwani. Wazazi Ni vema mkawaruhusu watoto na at the same time muwa guide katika URAFIKI. Hii itawasidia huko mbeleni. Yaani pamoja na kuoa, bado navurunda Mambo mengi nakuwa Kama beginner.

Ni ushauri tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahusiano ni muhimu katika kujenga ndoa Imara.

Suala la uendeshaji mahusiano ndio suala mtambuka, lina mapokeo tofauti tofauti miongoni mwa watu ingawa mafundisho ya kiimani(Dini) zilizopo zimetoa muongozo wa kuendesha mahusiano.

Ukifeli kujenga msingi nyumba/jengo halitakuwa imara.
 
Back
Top Bottom