Usidanganyike: Hakuna malaika anayekuja kutoa roho yako, dead man knows nothing

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,629
106,595
a1912169128_16.jpg

Kuna jamaa kwake kafunga vipaza sauti hua anaweka mawaidha na dua kiislamu, ni jambo jema sana hili. Ila sasa katika mawaidha aliyoyaweka jana usiku saa 4 kaweka mawaidha yanayohusu Kifo, kwakweli yale mawaidha yalinikosesha amani ya moyo maana yalikua yanaogofya na kutisha hasa, yalikua yanahusu jinsi malaika wa mauti anavyokuja kuchomoa roho.

Nilikua interested zaidi hiyo sehemu ambapo Malaika anakuja kuchomoa roho, na ndio kilichofanya niandike mada hii jinsi mimi navyo elewa dhana ya Kifo, sijui wengine mnaielewa vipi. Mimi navyoelewa wakati wa kufa hakuna malaika Azrael wala kiumbe yoyote yule anayekuja kutoa roho ya mtu. Lengo la mada hii sio kukashfu dini wala imani za watu, bali kuelimishana na kuelekezana bila kashfa.

Dhana ya Kifo

Kwanza kabisa viumbe vyote vimeumbwa katika mifumo miwili ambayo ni Mortals na immortals. Mortals ni viumbe vyote ambavyo vinaweza kufa mfano binaadamu, wanyama, mimea n.k Immortals ni viumbe wote ambao wanaweza kudumu maisha yote kama haitatokea wakauwa Wanaojulikana zaidi ni jelly Fishes na baadhi ya bacteria. Futurist na wanafalsafa mbalimbali wanasema kwamba binaadamu wa karne hii ya 21 baada ya miongo kadhaa anaweza kufanikisha kuwa katika mfumo wa Immortal kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia na hasa kwenye madawa na matibabu..pia Extending of life span will be possible mpaka kufika miaka 170. usibishe SOMA.

Kifo: Kwa upande wangu naweza fafanua kifo ni kitendo cha Roho kuuacha mwili huu wa nyama na kwenda Dimmension nyingine na mwili kubaki duniani,mwili utabaki duniani ili kukamilisha circle ya kwa kuoza na kuruhusu viumbe wengine kutokea...Mtu anapokufa anaanza kufa kiungo kimoja kimoja mwisho kabisa ubongo ndio unamalizika, kinachotoka katika mwili wa binaadamu ni roho (Soul). Kwenye computer kuna chip inaitwa BIOS Chip hii kazi yake ni kubeba taarifa zote za kompyuta husika..Hivyo Roho ni kama Bios Chip, Roho ndio inabeba taarifa zoote zinazokuhusu wewe ikitoka inaondoka nazo, mwili unabaki unaharibika. Ndio maana Vitabu vya dini vinasema Mungu anahukumu Roho sio mwili, kwakua mwili unakua hauna kazi tena.

Hakuna kiumbe yoyote anayekuja kukutoa roho sijui anakuja kuivuta kuanzia kwenye kidole cha Mguu HAKUNA. Maisha ya binaadamu ni kama jenereta lililowekewa mafuta, mafuta hayo yatafika muda fulani yaishe yakiisha tu basi Jenereta litazima. Tuchukulie Mwili ni Jenereta, Mafuta ni Muda (Time), Sasa iko hivi kinachofanya mwili ufe ni muda! Though time seem to be Illusion but it is Virtual Real.Muda ndio unafanya kiumbe fulani afe, Ndio maana Wanasayansi wanafanya kila njia kufanikisha kwenda kinyume na muda kwa kutumia Time Travelling (Ref: Time travel,itakua suruhisho la kifo). Duniani tumewekewa muda ili tuweze kufanya shughuli zetu za kila siku kwa kuufuata, Pia mwili wa binaadamu umewekewa Muda fulani ukifika tu basi roho yako haina budi kuuacha mwili, sasa hapo haijalishi Roho yako itauacha mwili kwa kutumia njia ipi. Ndio maana wanasayansi wanaona wakifanikisha kutengeneza Time travelling Machine
watakua wanaweza ku-loop from one point to another point with a different Time.

Sasa iko hivi baada ya process ya mtu kufa ikimalizika Roho inakua enda kwenye eneo linalofahmika kama After death au Eternal Realm,Roho ikiwa eneo hilo inakua kwenye mfumo wa Spirituality. Kwenye eneo hilo Time is Timeless, Roho ikiwa hapo haiwezi kufa tena,roho haiwezi kuzeeka wala kukua maana Hakuna Muda. muda upo kwa binaadamu tu...Ndio maana mtu akifufuka leo hii atajua kua alikua tu kalala muda mfupi uliopita. Usidangnyike eti kuna malaika hua anakuja kaburini anaanza kukufanyia mahojiano na kukupa mateso.Hakuna kitu kama hiko Deadman knows nothing, Deadman tells no Tale.

Malaika ni Roho, kapewa uwezo wakubadilika kwa kuvaa umbo lolote lile analotaka kutokana na majukumu husika aliyopewa, anaweza kubadirika mwanamke au mwanaume au kiumbe yoyote. Yesu ni Roho, alipokuja duniani alivaa umbo la kiume, Ukifa roho yako inakua kwenye mfumo wa Immortal, ndio hapo sasa roho yako ikiwa convicted to hell or Heaven itaishi Daima..maana Huko muda hau-exist.

Maoni yangu

Dunia imebadiriki,vizazi vimebadirika..inawezekana kipindi hiki vizazi vya Millenial generation (watu waliozaliwa kuanzia 1982 mpaka 2004 na Generatiion Z (watu waliozaliwa kuanzia 2005 mpaka leo hii) inawezekana ndio vizazi vilivyo elimika na kustaarabika zaidi kuwahi kutokea hapa duniani kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia pamoja na mabdiriko ya kimazingira...Hivyo Peoples are not fools anymore, Viongozi wa imani za kidini inabidi wabadili approach wanazotumia katika kuwarudisha watu kundini. Tusiwatishie watu kwa mambo ya kufikirika kama hayo ya Malaika kuja kukuvuta roho wakati hata huyo anayekuhadithia hajawahi kupata hata Near Death Experience kiufupi hata yeye kahadithiwa na mtu aliyehadithiwa.

Hizi dini kubwa mbili duniani ndio zinaongoza kua na wafuasi mambumbumbu ndio maana hata ugomvi wa sisi kwa sisi hauishi.ELIMU ELIMU ELIMU. Ukingalia kwa makini unaweza ona Zile imani tunazoziona hazina maana kama Budhism,Taoism,Atheism,Induism nk wao wanaongoza kwa kua watu wapole na wanahekima sana wajua kwa nini? Kwao hawana mipaka kwenye elimu, kichwa kitupu ni sawa na debe tupu..kichwa kilichojaa vitabu ni sawa na debe lenye maji ndani. unaweza pima yupi mpiga kelele.

Kwa wenzetu hasa mabudha wao husoma kila kitu,falsafa, fizikia,Spiritaul enlightment,astronomy, biolojia nk nk ndio maana ukimkuta budhist mahali hua wako very smart upstairs, au Monk wa Shaolin wako very smart mno maana wao hadi Martial arts hujifunza na wanaijua vizuri mno. Wachawi nao wanajua mengi mno maana wanasoma vitu ambavyo viko beyond the limit (uchawi ni sayansi isio songa mbele, conservative) sie tunajisome vitu kufuata mtaala.

Huku kwetu kwa Dini ya waroma Huku tunatembea na Psychology, Philosphy na Theology. Angalau huku mambo sio mabaya maana hvyo vitu vitatu vinawasaidia kuwaunganisha watu kwa kutumia akili zaidi. Ila kwa dini kutoka kwa warabu kidogo huko hali ni mbaya hasa kwa wafuasi wa bara la afrika, wao elimu ahera tu! elimu dunia kwao haramu angalau sasa hivi wanabadirika ndio maana wakiambiwa kuna jamaa hua anakuja kubeba roho na vitisho vingine vingii wao huamini. Jamni tuwekeze kwenye elimu.

Learn, Learning never exhaust the Mind,and knowledge will keep you Free and Peace
-Vers
 
Ingependeza angekuja marehemu mmoja akatuthibitishia ulichoandika hapa, otherwise utakuwa umeunga unga maneno tu,inashangaza sana kiumbe usiyeijua hata dakika yako moja mbele ni nini kitakutokea kisha uje kuzungumzia habari za kifo humu.
 
Mkuu pia nimekuwa nikijiuliza hiki kitu siku nyingi;

"Ni kwanini mahubiri mengi yanajengwa katika dhana ya kutia hofu badala ya kuelimisha wafuasi?"
Mfano;

"Israil atakuja na kuanza kunyofoa roho ya mtu kuanzia kidolen hadi utosin kwa maumivu makali mno"

"Siku moja Mtume(S.W.A),alipita makaburini akasikia sauti;maswahaba wakamuuliza hizo sauti ni za nini akawajibu ni sauti za mayahudi wakiteswa humo makaburini"

"Atakuja malaika (kaburini) na kumuuliza huyo mtu(maiti/marehemu),jina lako ni nani?,Dini yako ni ipi?,mola wako ni nani,mtume wako ni yupi,ndugu zako ni kina nani(Kwa lugha ya kiarabu)"

"Na kwa ajili yao(maiti walioshindwa kujibu maswali) yatakuwapo marungu ya chuma,kila wapigwapo watatamani kutoka kaburini wasiweze."

"Maiti anajua ni nani anayemwosha,anayembeba na anayemzika na anasikia mambo yote"

Hayo ni miongoni mwa hayo mafundisho na yapo mengi ya kutisha zaidi.
Najiuliza pia ikiwa Mungu ni wa upendo kwanini anawataabisha hivyo watu?.

*Lakini pia inakuaje mwenye hekima (aliyepewa hekima zaidi na M.Mungu) zaidi ya wanadamu wote waliopata kuishi Nabii Suleyman,akubaliane na hoja zako kuwa mtu akifa hajui chochote kabisa na wakati huo huo kuna vitabu vinafundisha tofauti?.*

Hapa chini nimenukuu maneno mfanano ya Suleyman yanayokubaliana na ulichoandika.

SWALI:(halihitaji jibu)

Je,Mungu hutumia njia hizo hizo pindi atoapo roho za nguruwe,paka na ng'ombe?.

NOTE:Anavyokufa huyu(Mwanadamu),ndivyo anavyokufa yule (mnyama) na WALA MTU HANA CHOCHOTE CHA KUMSHINDA MNYAMA WOTE HUENDA SEHEMU MOJA!.

20191019_181032.jpeg
20191019_180919.jpeg
 
...................Ingependeza angekuja marehemu mmoja akatuthibitishia ulichoandika hapa otherwise utakuwa umeunga unga maneno tu,inashangaza sana kiumbe usiyeijua hata dakika yako moja mbele ni nini kitakutokea kisha uje kuzungumzia habari za kifo humu.
Kwahiyo hao wanaosema izrael anakuja hafu anvuta roho yako unawaambia vipi..
 
Mkuu pia nimekuwa nikijiuliza hiki kitu siku nyingi;

"Ni kwanini mahubiri mengi yanajengwa katika katika dhana ya kutia hofu badala ya kuelimisha wafuasi?"
Mfano;

"Israil atakuja na kuanza kunyofoa roho ya mtu kuanzia kidolen hadi utosin kwa maumivu makali mno"

"Siku moja Mtume(S.W.A),alipita makaburini akasikia sauti;maswahaba wakamuuliza hizo sauti ni za nini akawajibu ni sauti za mayahudi wakiteswa humo makaburini"

"Atakuja malaika (kaburini) na kumuuliza huyo mtu(maiti/marehemu),jina lako ni nani?,Dini yako ni ipi?,mola wako ni nani,mtume wako ni yupi,ndugu zako ni kina nani(Kwa lugha ya kiarabu)"

"Na kwa ajili yao(maiti walioshindwa kujibu maswali) yatakuwapo marungu ya chuma,kila wapigwapo watatamani kutoka kaburini wasiweze."

"Maiti anajua ni nani anayemwosha,anayembeba na anayemzika na anasikia mambo yote"

Hayo ni miongoni mwa hayo mafundisho na yapo mengi ya kutisha zaidi.
Najiuliza pia ikiwa Mungu ni wa upendo kwanini anawataabisha hivyo watu?.

*Lakini pia inakuaje mwenye hekima (aliyepewa hekima zaidi na M.Mungu) zaidi ya wanadamu wote waliopata kuishi Nabii Suleyman,akubaliane na hoja zako kuwa mtu akifa hajui chochote kabisa na wakati huo huo kuna vitabu vinafundisha tofauti?.*

Hapa chini nimenukuu maneno mfanano ya Suleyman yanayokubaliana na ulichoandika.

SWALI:(halihitaji jibu)

Je,Mungu hutumia njia hizo hizo pindi atoapo roho za nguruwe,paka na ng'ombe?.

NOTE:Anavyokufa huyu(Mwanadamu),ndivyo anavyokufa yule (mnyama) na WALA MTU HANA CHOCHOTE CHA KUMSHINDA MNYAMA WOTE HUENDA SEHEMU MOJA!.

View attachment 1238491View attachment 1238492
Mkuu..
Ndio yale yale baadhi ya dini wanatumia maneno ya kutisha ili kuwa vuta watu..Kwakweli sidhani ni sahihi. Inabidi wafahamu kua vizazi vimebadirika tena ukiwapa stori za kutisha ndio wanaona huyo Mungu hana ishu kama atakua mkatili kiasi hiko
 
Kabisa Mkuu,yaani kuna mafundisho mengine hata mtu mwenye uwezo mdogo tu wa kufikiri hawezi kukubaliana nayo,chukulia tu mfano mdogo kwa watu hawa wawili;

1: Aliye zimia (Fainting).
2: Anaendaliwa kwa ajili ya Surgery(Genaral Anesthesia).

Wanakoswa uwezo kabisa wa kujua hata kuwaza,Wako wapi, wanafanya nini,ni mahali gani,wamezungukwa na kina nani, na wanafanyiwa nini.

Vipi itakuwakuwaje kwa mtu aliekufa?..

20191019_200008.jpeg
 
Hivi vitisho ndiyo vilinifanya nihamehame dini kutafuta penye afadhali,kumbe kule nilikoingia ndiyo kunatisha zaidi

Siku ya kwanza tu swala ya asubuhi muadhini anaita watu wakaswali alisema
"Kitanda chako ndiyo jeneza lako,nikavuta shuka mpaka kichwani,jamaa akaendelea na hilo shuka ulilojifunika ndiyo sanda yako,waislam amkeni

Dah sikulala tena ile siku,nakumbuka asubuhi ndiyo nikapata akili ya kujua michezo yao baada ya kuanza kuhoji na.kusoma

Angalau sasa nimekata minyororo ya dini niko huru sana na amani.
 
Hahahaaa it's very scary. Mamdogo alikua anapenda kutupiagia hizo stori..Kwakweli chumban tuilikua tunaogopa kwenda usiku..kulala
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom