aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 792
- 1,144
HAKUNA mtu mwenye akili timamu ataunga mkono umwagaji wa damu waliofanyiwa raia wa kigeni waliokuwa wakipata chakula kwenye mkahawa maarufu wa Luqman, mtaa wa Mkunazini mjini Zanzibar.
Kijana anayekisiwa kufika umri wa miaka 25, aliingia kwenye mkahawa huo maarufu kwa vyakula vya Kizanzibari, na kushambulia watu watatu hapohapo na wengine watatu wakati akitoka nje kwa nia ya kukimbia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali ametangaza kuwa kijana huyo amekamatwa na anahojiwa kwa upelelezi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani.
Watu sita kuchomwa visu, haihitaji nguvu nyingi za kufikiria ili uelewe kuwa kilichofanywa ni haramu.
Kamanda Nassir aliwataja majeruhi kuwa ni Mauget Gerarol (66), raia wa Ufaransa ambae amejeruhiwa pembeni ya jicho la kulia, Jennifer Wolf (24), raia wa Ujerumani ambaye amejeruhiwa sehemu ya kichwa na Anna Catharina (20), raia wa Ujerumani aliyejeruhiwa kichwani.
Mtuhumiwa alikimbia na akiwa njiani umbali wa mita 60 kutoka Luqman, alikutana na vijana wengine waitwao Hassan Abdalla anayeishi Kiponda (24) na raia wa Canada, Liying Liang na kuwajeruhi kwa kuwachoma kisu. Hassan alijeruhiwa mdomoni na Liang alichomwa kisu shavuni.
Baadaye alimchoma kisu Sajad Hussein (55). Majeruhi wote walikimbizwa Hospitalli ya Tasakhtaa Global iliyopo Majestic mjini Zanzibar walikotibiwa. Wote waliruhusiwa kutoka baada ya matibabu isipokuwa Mauget ambaye hali yake ilikuwa haijawa nzuri.
Licha ya tukio lile kuumiza, pia mapokezi ya tukio yanasikitisha na kuumiza vilevile. Wapo walioanza kuichoma visu vya udini Zanzibar, wakiilaumu imani ya wengi wa watu wa Zanzibar kuwa ndio chanzo.
Wengine wakaja na hekaya ya ajabu wakisema ndio madhara ya kulazimisha watu kufunga.
Ni kauli ya ajabu, msema kauli ya namna hii haeleweki kirahisi hasa kwa mazingira ya tukio lenyewe lilivyotokea. Labda hata uwezo wake wa kufikiri ni mdogo, asingechanganya uongo ndani ya tukio hilo.
Kwanza hakuna mtu aliyelazimishwa kufunga Zanzibar. Pia majira ya tukio lilipotokea (saa moja za usiku) katika mkahawa husika, hakuna uhusiano na kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani.
Nilipitia ukurasa mmoja wa habari nikakutana na maoni mengi yasiyoingia akilini, baada ya ukurasa huo kuiweka habari ile. Anasema, “Kwani wenzetu Z’bar hawana upendo kwa wenzao wa dini nyingine mbona Bara kuko shwari.”
Kwani nani kamwambia tukio la watu kuchomwa visu lina uhusiano wa chuki za kidini? Mtu aliyechoma visu usiku, tena akachoma visu raia wa kigeni na wenyeji. Uko wapi uhusiano wa dini na tukio hili?
Unaweza kuhisi msemaji ni mpinga udini lakini ukweli sio mpinga udini ila ni ‘mdini.’ Sababu ni kwamba hakuna njia yoyote ya kuhusisha tukio la kihalifu na imani ya watu wengine, ikiwa huna chuki na imani hiyo.
Nimekutana na watu katika kutoa maoni yao wanausukumia lawama Uislamu moja kwa moja. Pengine wanaelewa dini ya mtuhumiwa, sawa.
Lakini swali la msingi linakuja: mtuhumiwa ndivyo alivyodai kuwa ameshambulia kwa visu kwa sababu ya imani yake? Hajasema hivyo. Sasa mtu ukihusisha tukio lile na dini, kwangu ndio naona ulivyo na chuki.
Walimwengu wanaelewa mauaji ya kutisha aliyoyafanya Adolph Hilter aliyekuwa kiongozi wa Kinazi wa Ujerumani, barani Ulaya, pia inaeleweka alikuwa mfuasi wa dini gani, lakini ni ujinga kuhusisha dini yake na unyama alioufanya.
Hata Mfalme Leopold II wa Ubelgiji ambaye aliendesha mauaji ya Waafrika wasiopungua milioni 10 na meteso ya watu kuachwa mikono vibutu katika taifa la Congo, pia walimwengu wanaelewa alitokea dini gani. Lakini vilevile ni ujinga kuhusisha imani yake na unyama alioufanya.
Kuna mambo mawili hapa ni lazima yaeleweke. Moja: Kuna watu hutumia imani ya dini kufanya vitendo viovu katika jamii zetu. Watu hawa wako katika dini zote, hufanya kwa sababu ya chuki au ujinga na kuzitumia dini kama kisingizio.
Ukienda India utakutana na Wahindu wa misimamo mikali, ukila tu ng’ombe wanakuua. Wao ng’ombe wanamuabudu. Mnyanmar wapo Mabudha wa siasa kali wanachinja na kuua jamii ya Rohingya, wanaisafisha ardhi yao ili isiwe na wafuasi wa dini nyengine isipokuwa wao tu. Mashariki ya Kati yapo makundi ya Kiislamu wanachinja na kuua pia nao kisingizio kikiwa ni dini.
Ukisogea kwa majirani zetu, Afrika ya Kati utakutana makundi ya Kikristo yanafanya unyama wa kutisha kwa kisingizio cha dini yao.
Hata Mayahudi-Mazayuni wa siasa kali wapo, ndio hao wanaonyanyasa na kupora ardhi, sababu yao kubwa ni kuwa kitabu cha dini yao ndio kinawapa nguvu.
Jambo la msingi kuelewa kuwa katika imani zote kuna watu wakorofi; huzitumia imani kama ngazi ya kutendea maovu. Mara nyingi hutokana na uelewa duni au hata chuki tu ambazo mtu hujifunza kutoka kwa viongozi wake.
Ukiwa unaelewa kuwa dunia iko hivyo, wala hupati tabu ya kumuoneshea kidole mwenzako, wakati imani yako unaelewa wazi kuna watu wanaitumia vibaya.
Pili: Kuna watu ni wafuasi wa dini fulani. Hutenda maovu lakini hawatoi madai kuwa imani ndio zimewasukuma kutenda hayo.
Ikiwa vikosi vyetu vya usalama vinarikodi wahalifu na ufuasi wa dini zao, naamini utakutana na wahalifu wa dini zote.
Kundi hili la pili wapo wengi katika jamii zetu, na ndio sawa na kile kilichotokea Zanzibar. Aliyejeruhi watu kwa kisu hakuleta madai kuwa dini yake ndio imemsukuma kufanya hivyo.
Jambo la ajabu na la kusikitisha ni kuzuka baadhi ya Watanzania wakaanza kupiga zumari za udini. Wakati tukio halihusiani na imani, kipi sasa kikufanyacho kulipigia chapuo la udini; kama si chuki dhidi ya imani ya wengine?
Kuhusisha imani ya mamilioni ya watu kwa tukio la mtu mmoja ambaye amefanya kwa sababu zake binafsi, sioni mantiki yake.
Eti kwa sababu anatokea sehemu fulani, kule kuna watu wengi wa imani fulani na kipindi hiki ni cha Ramadhani, basi moja kwa moja ni dini yake tu ndio iliyomsukuma. Fikra nyepesi sana. Za kijinga kabisa.
Na huo ndio udini hasa. Udini wa mwenye chuki na dini ya wengine. Huwezi kupambana na wahalifu kwa kuanza kutengenezea hukumu za ajabu ajabu kama hizi, kuhukumu matukio kwa sababu za kieneo na kiimani?
Katika hali kama hii, jambo kubwa na la msingi ni wapenda amani kuwa kitu kimoja, sio kubuni vitu vya uongo na visivyosaidia kujenga umoja.
Ni haki watu kusimama pamoja kupingana na yule anayetumia imani kufanya ukorofi.
Pasipokuwa na ukweli wa ukorofi basi pasitengenezwe hadithi za kusisimua za kuhusisha imani yake na unyama anaoufanya mtu.
Ikishakuwa ni mazoea kuyaangalia mambo kwa jicho la chuki za kibaguzi na dini; kuanza kuiona imani fulani ni tatizo katika jamii, ikae akilini kitakachofuata ni kuwachukia wafuasi wa imani ile.
Hatutojenga jamii yenye mtangamano na mahusiano mazuri ikiwa unawaona wengine ni tatizo kwa sababu ya imani zao, hata mapenzi na utulivu wao huujali tena. Huko siko.
Tukio la kihalifu libaki kuwa la kihalifu, lisipambwe kwa mapambio ya chuki za kidini au kikabila.
La muhimu polisi kuimarisha ulinzi na mbinu za kisasa kupambana na wahalifu. Wachoma visu vya vyuma wadhibitiwe, pia jamii iwe pamoja kupambana na wahalifu wa wachomaji visu vya udini kwenye migongo ya imani za wengine.