Usibweteke kisa tu kiongozi mkubwa anatoka kwenu au ni wa dini yako

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Huwa najiuliza sana kwa nini watu wakisikia mmoja ya watu kutoka mkoani kwao, wilayani kwao wanashangilia sana kana kwamba wamepata uokovu. Watu wamekuwa wakabila na wadini sana kiasi kwamba hushangilia kila mmoja ya watu kutoka kwao hupata uteuzi kama vile uwaziri, naibu waziri na vyeo vingine vya kitaifa.

Maendeleo yako yatatokana na jitihada zako, ubunifu wako, uchapakazi wako na mambo kama hayo.

Usitegemee waziri ama kiongozi yeyote kutoka kijijini kwenu, wilayani kwenu, mkoani kwenu ama kutoka dini yako atakuletea maendeleo as individual entity.

Wala huwa hatuwazii sana kama mtu ni binafsi.

Nyerere alikuwa mkuu wa nchi kwa miaka 23 lakini aliiacha Butiama ikiwa na hadhi ya kijiji.
Mkapa alikuwa rais kwa miaka kumi na kabla ya hapo alikuwa waziri wa wizara nyingi tu lakini mpaka leo LUPASO sio mji wala mji mdogo.

Kikwete kadhalika kaiacha Msoga yake ikiwa bado ni kijiji na alikuwa na uwezo wa kufanya chochote lakini maslahi mapana ya nchi yalimfanya aisiiwazie sana Msoga kuliko kuiwazia nchi.

Rais hata awe wa dini yako hatakufanya wewe usitoe sadaka msikitini wala kanisani kwako.

Hakutokuwa na impact kwenye maisha yako positively eti kisa tu rais ni wa dini yako ama kabila lako.

Usije kufikiri waziri mkuu akiwa wa dini yako, kabila lako kuna kitu cha ziada utapata kwa sababu hiyo.

Tudijiingize huko kwani hayo mambo hayana faida hata kidogo kwa taifa letu, badala yake ni kutugawa tu bila sababu ya msingi.

Kwangu mimi kabila na dini yeyote kutoa viongozi wakuu wa kutaifa hata kwa miaka 300 ni sawa tu as long as Tanzania inasonga mbele na tunaishi kwa amani.

Tuendelee kuilinda na kuipenda nchi yetu milele daima.
 
Back
Top Bottom