Usiandike Jina la mtoto Mmoja tu kwenye Mali ambayo itakuja kuwa urithi wa familia nzima

Ramon Abbas

JF-Expert Member
May 4, 2021
1,964
3,897
Ewe mzazi, ushawahi kujiuliza swali nini kitatokea wewe ukishafariki? Mali ulizonazo leo kama ardhi, nyumba, viwanja na magari vinatawanyika vipi kwa familia yako?

Ni jambo jema sana kununua assets mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya baadae lakini unapoandika jina la mtoto mkubwa kama mmiliki, kumbuka utakuja kuwafanya hawa wadogo wahangaike sana kuja kunufaika na ile asset, vijana wa sasa sio waaminifu kama wa zamani.

Ndugu wazazi, Hati ikishaandikwa jina la mtu, na serikali ikathibitisha hilo, basi jua huyo ni mmiliki hali wa hicho kitu, HAKUNA MTU ATAKUJA NA KUSEMA NI MALI YETU.

Kijana mkubwa anaweza kuwadhulumu wadogo zake kwa kigezo kwamba BABA ALIMNUNULIA HICHO KITU hivyo wao hawatohusika huko.

Ni hayo tu kwa leo.

Tukutane kwenye comments
 
Hivi mume akifariki na mke akawa bado yupo hai, kwani mali hazibaki mikononi mwa huyo mama?
Nimeuliza kwa kuwa nataka kuelimishwa. Au mpaka nayeye awepo kwenye mirathi?
 
Hivi mume akifariki na mke akawa bado yupo hai, kwani mali hazibaki mikononi mwa huyo mama?
Nimeuliza kwa kuwa nataka kuelimishwa. Au mpaka nayeye awepo kwenye mirathi?
Mke harithi Mali za mume anayerithi ni mtoto.

Mke ana sehem ya Mali atakayopewa bali si Mali zote.
 
Back
Top Bottom