Usiamini Mtu: Heri lawama kuliko hasara. Karibu ujifunze kupitia visa hivi

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
MKASA WA KWANZA: Unanihusu mimi mwenyewe

Naanza na rafiki yangu:
Juzi jumamosi nimeamka salama, baada ya kufanya mambo yangu nikaona ngoja nimtembelee jamaa mmoja hivi ni rafiki yangu sana. Nimekutana nae na katika kupiga stori mbili tatu akaanza kulalamika kuwa 'ametapeliwa' sh. 450,000 na mtu ambae anamuamini kabisa. Ilikuwaje?, huyu rafiki yangu alinunua kifaa cha kutumia umeme kipya kutoka kwa mshikaje wake sasa kwakuwa ni washikaji, jamaa hakupewa risti na maisha yakaendelea. Kifaa ni kipya kabisa na kwenye boksi kinasoma warranty miaka 2.5..Jamaa angu ametumia kile kifaa ndani ya muda mfupi sana kikaanza kuzingua..Katika kukirudisha dukani, jamaa ake akamruka kuwa yeye sio aliyemuuzia na akamwambia kama kweli alinunua pale atoe risti..Huyu rafiki yangu hakuamini kama rafiki yake angemfanyia hivi..Hana cha kufanya, kwa sababu hana ushahidi wa risti imebidi ale hasara tu..UAMINIFU umemponza.

Tuje kwangu sasa:
Baada ya mkasa wa rafiki yangu nikakumbuka kisa changu ambacho kilinitokea mwaka jana na nilivyotumia akili ya kuzaliwa kukitatua..

Mwaka jana mida kama ya mwezi wa 9, kuna kitu nilikuwa nakihitaji sana. Na kama ilivyodesturi yangu, vifaa vinavyotumia umeme huwa sinunui used (mkononi). Ni bora nikaingia gharama kubwa kununua mpya. Tuendelee..

Sasa nikakumbuka kuna rafiki yangu anafahamiana na mmoja wa wauzaji wa hivyo vifaa nikamuomba anifanyie connection (aliwahi kumuuzia kifaa kingine). Kweli nikapata namba za yule mshikaji nikawasiliana nae na tukaelewana bei na nikamwambia poa, kesho jioni niletee. Huyu mshikaji ofisi yake ipo sehemu X halafu mimi nipo mbali na pale (Y)..almost 30 minutes kwa bodaboda. Akaniambia kesho jioni saa 12 nakuletea mwenyewe. Uzuri kitu chenyewe ni portable, nikamwambia poa ila HAKIKISHA ukija unakuja na risti, warranty pamoja na vitu vyote muhimu vinavyokuwa pamoja na hicho kifaa kikiwa kipya. Na kwa msisitizo zaidi nikamtumia na message. Akajibu poah.

Imepita kama dakika 20 nampigia simu uko wapi?, akasema nimempa bodaboda wangu anakuletea mimi nimepata dharura kidogo (Kumbuka mpaka hapa huyu jamaa simjui na hanijui kwa sura, nilifanyiwa connection tu na mtu ninaemwamini). Baada ya dakika 2 bodaboda ananipigia simu akajitambulisha akanambia nimepewa mzigo wako na fulani kwahiyo nipe dakika kadhaa nitakuwa hapo..Nikasema poah. Baada ya dakika kama 18 jamaa akanipigia simu akanambia nimefika, kwakuwa nilikuwa nishasogea kituoni nikamuona. Muda huo yapata saa 2 usiku.

Akanambia mzigo wako huu hapa (kweli kitu box jipya na liko sealed), nikamwambia mkuu, hapa mimi natoa hela almost nusu milioni, siwezi kukukabidhi kwa juu juu tu bila kujiridhisha. Halafu pia hapa ni barabarani kupeana hela nyingi barabarani na kwa muda huu sio vizuri. Huwezi jua nani anakuona hii ni kwa usalama wako na wangu. Usiwe na haraka, twende home tukakabidhiane. Nikapanda bodaboda yake haooo hadi home. Kufika home nikaanza mchakato wa kuhesabu pesa..then kabla sijafungua box nikamuomba risiti na warranty..Jamaa akasema warranty card ipo ndani ya box ila risiti hajapewa labda nimuulize muuzaji.

Nikaona sio inshu, nikachukua simu nikampigia jamaa..Nikamwambia mbona risiti siioni?, akasema hamna shida nimuamini tu..nikakataa. Akasema mara hela niliyotoa ni ndogo sana (amenifanyia discount) kwahiyo hawezi kutoa risiti. Nikakataa. Akasema tena nichukue mzigo then kesho atanitumia risiti au atanipigia picha. Nikakataa nikamwambia tuliongea tukakubaliana na msg nilikutumia na ukasema umeielewa. Akaendelea kusisitiza nimuamini tu mbona kashafanya biashara na rafiki yangu. Nikakataa, nikamwambia mkuu bila risiti, sichukui mzigo. Jamaa atarudi nao hadi siku ukiwa na risit ndio nitaupokea.

Pale boda boda akaanza mara nimuamini jamaa anamjua ni mtu poa na chochote kikitokea nimpigie hata yeye simu. Nilimwambia tu mkuu, siwezi kumuamini mtu (Marafiki zangu walishanisaliti nikapoteza imani na watu). Ujue hapa natoa hela sio makaratasi?..Hivi mfano ungekuja na huu mzigo then mimi nikwambie nakupa hela kidogo halafu 50k nitakutumia jamaa angekubali?..Akakosa jibu. Nikamwambia pole kwa usmbufu, mrudishie jamaa na kama vip chukua hii 2k utaongezea hata mafuta halafu mengine we na jamaa mtajuana. Akasema nisijali (nadhani aliielewa logic yangu), tukaagana kwa amani akasepa. Biashara haikufanyika.

Hoja zangu ni hizi: Je ningechukua na ikitokea dharura nikirudishe, atanipokea? Duka lake hata silijui, si ataniruka?..Nimetoa hela natakiwa kuwa na amani na kifaa changu. What if ni cha wizi mi nitajuaje japo ni kipya?

Kesho yake nilimcheki rafiki yangu yule aliyenifanyia connection nikamueleza hali halisi na kumwambia biashara ilishindikana..Cha ajabu sasa, kumbe hata rafiki yangu kifaa chake alichonunuaga pale alipewa bila risiti..Nikamwambia alikosea sana na aombee kisizingue otherwise hiyo warranty haitakuwa na nguvu...HERI LAWAMA KULIKO HASARA...USIWE MWEPESI KUAMINI WATU otherwise hauthamini kitu unachokitoa.

MKASA WA PILI: Huu unamhusu mtu na mdogo wake

Hawa ni kaka wa damu kabisaa..Naomba mkubwa nimuite Paul halafu dogo nimuite Peter (Kama psquare japo sio mapacha). Huu mkasa ulitokea kitambo ila bado sekeseke lake hadi leo lipo.

Miaka kama 6 iliyopita, Paul alinunua kiwanja kwa ajili ya kujenga. Maisha yakaendelea baadae Paul akaelewana na Peter (Kwa kumuamini tu kuwa ni mdogo wake wa Damu) wakaingia makubaliano bila maandishi kuwa Peter ajenge kwenye kiwanja cha Kaka yake. Yaani kiwanja cha Paul ila nyumba inajengwa na Peter.. Partnership grade A kabisa hahahaha..

Maisha yameendelea..miaka imekatika..Sijui wamezinguana nini tu wale jamaa..Sasa hivi Paul anamwambia Peter atoe nyumba yake kwenye kiwanja chake (aibomoe). Peter hataki anasema kama vipi iuzwe nyumba na kiwanja arudishiwe hela yake..au kama inawezekana Paul ainunue hiyo nyumba. Paul naye hataki maana anasema nyumba ramani ni mbuvo haipendi...Utata juu ya utata.

Kukubaliana kwao sio tatizo japo walifanya makubaliano ya ajabu sana (mimi siwezi) na yenye upendo mkubwa sana ndani yake. Tatizo linakuja waliaminiana kwa mdomo tu...Yangekuwepo maandishi leo usingekuwa utata..Hadi leo mahusiano yao sio mazuri. Mama yao ndio anahangaika kuwapatanisha ila sio rahisi..Sijui itakuwaje.

HITIMISHO:
Wakuu, walioanzisha maswala ya risiti na mikataba hawakuwa wajinga. Ni kweli unaweza ukawa unamuamini mtu ila kwenye vitu serious weka maandishi..Mimi hata leo ndugu yangu akitaka kuniuzia kitu cha thamani kubwa...Lazima maandishi yawepo...Learn the lesson.
 
Hv mfano mtu anataka kukuapeli si anaweza kukupa hata risiti fake?? Yaan anakuwa na vitabu viwili vya risiti, wakija TRA anaonesha kitabu tofauti,,ukija mteja anakupa risiti tofauti. Sku yametokea ya kutokea anakuruka risiti sio ya duka lake.
 
kweli mkuu..nimeiona logic yako.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
unafanya biashara na mtu ujui duka lake umfahamu ata kwa sura alafu unadai na lisiti...

hata ungechukua iko kifaa alafu kikabuma hiyo lisit yako kam ushaidi ungempelekea nani wakati hata duka ujui lilipo
 
Sawa..nimeelewa mkuu..kuna sehemu nimeona weakness yangu..ila heri nusu shari kuliko shari kamili
 
Upo sahihi... ila kwa wengine sisi risiti hata tukipewa zinapotea zenyewe tu .. ule utaratibu wa sheli kukupa risiti kila ukiweka mafuta huwa naona kama unanikwaza na kunijazia uchafu kwenye gari..
Siku ukijaziwa mafuta afu yakawa na shida ndo utaelewa umuhimu wa kutunza risiti, walau basi hata kwa siku kadhaa kabla hujaongeza mafuta mengine. Maana vingnevyo mafuta yanaweza kuzingua na mwenye kituo akakukataa
 
Mkuu maisha hayatabiriki unaweza kukaza upewe risiti ili usipate hasara, Kumbe house girl anamaliza gesi kwa kuchemsha maharage,

Kulinda pesa isipote ni sawa na kulinda samaki baharini wasivuliwe. Ukilinda bagamoyo tegeta watu wanavua,
 
Upo sahihi... ila kwa wengine sisi risiti hata tukipewa zinapotea zenyewe tu .. ule utaratibu wa sheli kukupa risiti kila ukiweka mafuta huwa naona kama unanikwaza na kunijazia uchafu kwenye gari..
Risiti au mikataba na vyeti vyako binafsi na watoto vinatakiwa vitunzwe kwa umakini sana kwani unaweza kuwa na box file na kuhifadhi ndani ya sanduku la bati vinakuwa salama years and years

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
MKASA WA KWANZA: Unanihusu mimi mwenyewe

Naanza na rafiki yangu:
Juzi jumamosi nimeamka salama, baada ya kufanya mambo yangu nikaona ngoja nimtembelee jamaa mmoja hivi ni rafiki yangu sana. Nimekutana nae na katika kupiga stori mbili tatu akaanza kulalamika kuwa 'ametapeliwa' sh. 450,000 na mtu ambae anamuamini kabisa. Ilikuwaje?, huyu rafiki yangu alinunua kifaa cha kutumia umeme kipya kutoka kwa mshikaje wake sasa kwakuwa ni washikaji, jamaa hakupewa risti na maisha yakaendelea. Kifaa ni kipya kabisa na kwenye boksi kinasoma warranty miaka 2.5..Jamaa angu ametumia kile kifaa ndani ya muda mfupi sana kikaanza kuzingua..Katika kukirudisha dukani, jamaa ake akamruka kuwa yeye sio aliyemuuzia na akamwambia kama kweli alinunua pale atoe risti..Huyu rafiki yangu hakuamini kama rafiki yake angemfanyia hivi..Hana cha kufanya, kwa sababu hana ushahidi wa risti imebidi ale hasara tu..UAMINIFU umemponza.

Tuje kwangu sasa:
Baada ya mkasa wa rafiki yangu nikakumbuka kisa changu ambacho kilinitokea mwaka jana na nilivyotumia akili ya kuzaliwa kukitatua..

Mwaka jana mida kama ya mwezi wa 9, kuna kitu nilikuwa nakihitaji sana. Na kama ilivyodesturi yangu, vifaa vinavyotumia umeme huwa sinunui used (mkononi). Ni bora nikaingia gharama kubwa kununua mpya. Tuendelee..

Sasa nikakumbuka kuna rafiki yangu anafahamiana na mmoja wa wauzaji wa hivyo vifaa nikamuomba anifanyie connection (aliwahi kumuuzia kifaa kingine). Kweli nikapata namba za yule mshikaji nikawasiliana nae na tukaelewana bei na nikamwambia poa, kesho jioni niletee. Huyu mshikaji ofisi yake ipo sehemu X halafu mimi nipo mbali na pale (Y)..almost 30 minutes kwa bodaboda. Akaniambia kesho jioni saa 12 nakuletea mwenyewe. Uzuri kitu chenyewe ni portable, nikamwambia poa ila HAKIKISHA ukija unakuja na risti, warranty pamoja na vitu vyote muhimu vinavyokuwa pamoja na hicho kifaa kikiwa kipya. Na kwa msisitizo zaidi nikamtumia na message. Akajibu poah.

Imepita kama dakika 20 nampigia simu uko wapi?, akasema nimempa bodaboda wangu anakuletea mimi nimepata dharura kidogo (Kumbuka mpaka hapa huyu jamaa simjui na hanijui kwa sura, nilifanyiwa connection tu na mtu ninaemwamini). Baada ya dakika 2 bodaboda ananipigia simu akajitambulisha akanambia nimepewa mzigo wako na fulani kwahiyo nipe dakika kadhaa nitakuwa hapo..Nikasema poah. Baada ya dakika kama 18 jamaa akanipigia simu akanambia nimefika, kwakuwa nilikuwa nishasogea kituoni nikamuona. Muda huo yapata saa 2 usiku.

Akanambia mzigo wako huu hapa (kweli kitu box jipya na liko sealed), nikamwambia mkuu, hapa mimi natoa hela almost nusu milioni, siwezi kukukabidhi kwa juu juu tu bila kujiridhisha. Halafu pia hapa ni barabarani kupeana hela nyingi barabarani na kwa muda huu sio vizuri. Huwezi jua nani anakuona hii ni kwa usalama wako na wangu. Usiwe na haraka, twende home tukakabidhiane. Nikapanda bodaboda yake haooo hadi home. Kufika home nikaanza mchakato wa kuhesabu pesa..then kabla sijafungua box nikamuomba risiti na warranty..Jamaa akasema warranty card ipo ndani ya box ila risiti hajapewa labda nimuulize muuzaji.

Nikaona sio inshu, nikachukua simu nikampigia jamaa..Nikamwambia mbona risiti siioni?, akasema hamna shida nimuamini tu..nikakataa. Akasema mara hela niliyotoa ni ndogo sana (amenifanyia discount) kwahiyo hawezi kutoa risiti. Nikakataa. Akasema tena nichukue mzigo then kesho atanitumia risiti au atanipigia picha. Nikakataa nikamwambia tuliongea tukakubaliana na msg nilikutumia na ukasema umeielewa. Akaendelea kusisitiza nimuamini tu mbona kashafanya biashara na rafiki yangu. Nikakataa, nikamwambia mkuu bila risiti, sichukui mzigo. Jamaa atarudi nao hadi siku ukiwa na risit ndio nitaupokea.

Pale boda boda akaanza mara nimuamini jamaa anamjua ni mtu poa na chochote kikitokea nimpigie hata yeye simu. Nilimwambia tu mkuu, siwezi kumuamini mtu (Marafiki zangu walishanisaliti nikapoteza imani na watu). Ujue hapa natoa hela sio makaratasi?..Hivi mfano ungekuja na huu mzigo then mimi nikwambie nakupa hela kidogo halafu 50k nitakutumia jamaa angekubali?..Akakosa jibu. Nikamwambia pole kwa usmbufu, mrudishie jamaa na kama vip chukua hii 2k utaongezea hata mafuta halafu mengine we na jamaa mtajuana. Akasema nisijali (nadhani aliielewa logic yangu), tukaagana kwa amani akasepa. Biashara haikufanyika.

Hoja zangu ni hizi: Je ningechukua na ikitokea dharura nikirudishe, atanipokea? Duka lake hata silijui, si ataniruka?..Nimetoa hela natakiwa kuwa na amani na kifaa changu. What if ni cha wizi mi nitajuaje japo ni kipya?

Kesho yake nilimcheki rafiki yangu yule aliyenifanyia connection nikamueleza hali halisi na kumwambia biashara ilishindikana..Cha ajabu sasa, kumbe hata rafiki yangu kifaa chake alichonunuaga pale alipewa bila risiti..Nikamwambia alikosea sana na aombee kisizingue otherwise hiyo warranty haitakuwa na nguvu...HERI LAWAMA KULIKO HASARA...USIWE MWEPESI KUAMINI WATU otherwise hauthamini kitu unachokitoa.

MKASA WA PILI: Huu unamhusu mtu na mdogo wake

Hawa ni kaka wa damu kabisaa..Naomba mkubwa nimuite Paul halafu dogo nimuite Peter (Kama psquare japo sio mapacha). Huu mkasa ulitokea kitambo ila bado sekeseke lake hadi leo lipo.

Miaka kama 6 iliyopita, Paul alinunua kiwanja kwa ajili ya kujenga. Maisha yakaendelea baadae Paul akaelewana na Peter (Kwa kumuamini tu kuwa ni mdogo wake wa Damu) wakaingia makubaliano bila maandishi kuwa Peter ajenge kwenye kiwanja cha Kaka yake. Yaani kiwanja cha Paul ila nyumba inajengwa na Peter.. Partnership grade A kabisa hahahaha..

Maisha yameendelea..miaka imekatika..Sijui wamezinguana nini tu wale jamaa..Sasa hivi Paul anamwambia Peter atoe nyumba yake kwenye kiwanja chake (aibomoe). Peter hataki anasema kama vipi iuzwe nyumba na kiwanja arudishiwe hela yake..au kama inawezekana Paul ainunue hiyo nyumba. Paul naye hataki maana anasema nyumba ramani ni mbuvo haipendi...Utata juu ya utata.

Kukubaliana kwao sio tatizo japo walifanya makubaliano ya ajabu sana (mimi siwezi) na yenye upendo mkubwa sana ndani yake. Tatizo linakuja waliaminiana kwa mdomo tu...Yangekuwepo maandishi leo usingekuwa utata..Hadi leo mahusiano yao sio mazuri. Mama yao ndio anahangaika kuwapatanisha ila sio rahisi..Sijui itakuwaje.

HITIMISHO:
Wakuu, walioanzisha maswala ya risiti na mikataba hawakuwa wajinga. Ni kweli unaweza ukawa unamuamini mtu ila kwenye vitu serious weka maandishi..Mimi hata leo ndugu yangu akitaka kuniuzia kitu cha thamani kubwa...Lazima maandishi yawepo...Learn the lesson.
Inaonekana huko mikoani watu wanapata faida sana asee, hadi kumtumia mteja mzigo wa nusu milioni bila hata yeye kuweka senti tano kama assurance, hiyo ni biashara kichaa hiyo na wanaofanya mara nyingi wamekurupuka kufanya biashara

Option 1. Fuata mzigo dukani

Option 2. Tuma hela ya mzigo na yakutolea na bodaboda

Kikubwa unatakiwa ujue warranty sio burden ya retailer, yeye anachotakiwa kufanya ni kuchukua hicho kifaa na kukirudisha kwa supplier na wewe usubirie hao wenye kampuni wakutumie kipya sio umuingize yeye hasara
 
Mkuu usitumie nguvu nyingi kulinda pesa....! Ila tumia nguvu kubwa kuzitafuta ziwe nyingi Ilihali matumizi yako yazidiwe na kiasi cha pesa ulichonacho. Ukiona matumizi yako yanazidi kipato chako usipunguze matumizi ila tafuta namna ya kuongeza kipato kitakachozidi matumizi yako....!
 
Mkuu..upo sahihi...

Kufata mzigo dukani ilikuwa inawezekana ila tu alijitolea yeye mwenyewe kufanya delivery...na kuhusu gharama za bodaboda zilikuwa juu yake kwa sababu alijitolea mwenyewe kuleta...Kuhusu kutuma pesa kabla hujapokea mzigo ni ngumu..hapa inatakiwa hand in hand..

BTW option 1 ndio nzuri zaidi na ambayo hata leo nitakuwa naitumia.
 
Mkuu usitumie nguvu nyingi kulinda pesa....! Ila tumia nguvu kubwa kuzitafuta ziwe nyingi Ilihali matumizi yako yazidiwe na kiasi cha pesa ulichonacho. Ukiona matumizi yako yanazidi kipato chako usipunguze matumizi ila tafuta namna ya kuongeza kipato kitakachozidi matumizi yako....!
asante mkuu..logic yangu sio kulinda pesa...bali kufanya vitu kiutaratibu...ina maana hata ukiwa na hela nyingi sanaa utakuwa unanunua nunua tu vitu bila kuwa na assurance..sio kweli...Naamini hata Mo hawezi fanya hvyo...siyo mbaya ukijifunza mkuu.
 
MKASA WA KWANZA: Unanihusu mimi mwenyewe

Naanza
Pointi. hizi warrant huwa sijui hata zina maana gani. Maana hata kifaa kikiharibika pamoja na kuwa na rist utasumbuliwa mpaka utabwaga manyanga mwenyewe.
 
Mkuu usitumie nguvu nyingi kulinda pesa....! Ila tumia nguvu kubwa kuzitafuta ziwe nyingi Ilihali matumizi yako yazidiwe na kiasi cha pesa ulichonacho. Ukiona matumizi yako yanazidi kipato chako usipunguze matumizi ila tafuta namna ya kuongeza kipato kitakachozidi matumizi yako....!
kwa hiyo kama pesa alizo nazo zikiwa nyingi kuliko matumizi akubali kupata hasara za rejareja? azitumie ovyo?
 
Mdomo si maandishi....

Binadamu ni yuleyule tangu enzi.....

Makaratasi na kalamu ndio KINGA ya kila mmoja......

#KaziIendelee
 
Upo sahihi... ila kwa wengine sisi risiti hata tukipewa zinapotea zenyewe tu .. ule utaratibu wa sheli kukupa risiti kila ukiweka mafuta huwa naona kama unanikwaza na kunijazia uchafu kwenye gari..
Ni kweli mkuu ila amini ipo siku hizo risiti utakuja kuona umuhimu wake, hata mimi nilikuwa na huo utaratibu wa kuignore risiti lakini yaliyonikuta nimejifunza.
 
Back
Top Bottom