Usiache maandishi yako yaufichue uhalisia wako

Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
516
504
IMG_20181112_113554_052.jpg

"Usiache maandishi yako yaufichue uhalisia wako"

Sababu kuu ya thread hii na tafiti hii ni uchunguzi rahisi sana wa kimatokeo na ukweli ufichwao.

Katika robo fulani ya Dunia hii ya maarifa, mawazo ya kimaarifa yanaonekana kuwa ni yenye ufahamu mkubwa sana, tena hii bila kuzingatia ni nani mleta wazo. Ufahamu huo mkubwa unaletwa na utafiti wa kisaikolojia na tafiti mbalimbali zilizo fanyika tangu zamani. Ninaposema ufahamu mkubwa, ninamaanisha baadhi ya mambo na habari fulani vimekuwa rahisi sana na kurahisishwa kwa wakati huu tuliopo, mfano vyanzo vya taarifa vimekuwa vingi sana na hii imesababisha kujitosheleza na kujionyesha kwa jamaa nyingi zenye chaguzi fulani za mafundisho fulani kwa jamii au mahali fulani kwa misingi ya udhaifu ya uelewa wa sehemu mahalia. Mfano katika misingi ya uelewa binafsi ya ufahamu wa michakato ya kisayansi, kisaikolojia, kihistoria, hoja na habari za kisiasa, dini na muundo wa matukio binafsi ikiwa ni pamoja na ufanisi katika uandishi wa mseto. Sasa issue ipo hapo, hapa kumekuwa na watu wa aina mbalimbali wakiitaji kuviishi vipawa hivyo bila ya uwepo wa nguvu ya asilia na uchaji wa misingi ya kweli ya kile wakiandikacho au kukifikisha kwa hadhira kwa namna yoyote ile.


Hata hivyo wakati wachunguzi wa kisaikolojia wameleta mawazo fulani ya kimaadili kwa data ya ujenzi wa tiba ya kisaikolojia, mara nyingine wamerejea kwa mkazo wao wa kisaikolojia kuwa wao wenyewe na mawazo yao wakati mwingine wanakuwa wapumbavu kwa kushindwa kudhibiti miemko yao mara nyingi katika kuwasilisha jambo fulani kwa hadhira
(kama utaiga tabia fulani na kujifichia katika maandishi saidizi toka vyanzo vya taarifa na kusahau kuificha tabia yako ya asili, iliyojaa ujinga na upuuzi ndani yake, utagundulika tu. Kamwe huwezi kuificha asili yako na uelewa wako wa mambo jinsi ulivyo)

pia kumbuka mawazo ya kujenga ni mwanga wa kuufunua ukweli na kuijua purpose ya chanzo husika, yaani taarifa uliyoipata au kuisoma kutoka kwa mleta taarifa,na mwanga huo wa maswali na mawazo toka kwa hadhira ni kipimo tosha cha kujua ni nini nia ya mleta taarifa na ukuu wu umuhimu wa taarifa husika. Utaratibu huu unapaswa kupimwa kwasababu kauli hizi au habali nyingi zinatengenezwa tu na kutiwa chumvi nyingi ya kuonyesha kuwa ndani yake Kuna jambo kubwa sana lililofichwa vyema na kushindwa kueleweka na hadhira au labea uwe genius, wakati sio kweli ni uongo mtupu na habari za kupikwa.

Kwa maana nyingine, robo fulani umuhimu wa mawazo na taarifa za kisaikolojia,kisayansi, kisiasa au taarifa fulani nyeti au waziitazo tafakalishi zinazotokana na mawazo ya watu wa kisasa zinaharibiwa tu na wale walio na habari au vyanzo vya habari na taarifa, Kisha kutokana na uelewa wao mdogo hushindwa kuielezea vyema hadhira na kuamua kujibu kwa matusi na kejeli za kipuuzi mbele ya kadamnasi.
Asanteni.
 
Back
Top Bottom