Usiache kazi yako ya ajira na kukimbilia ujasiriamali kama nguvu ya hivi vitu huvijui vizuri.

MuuzaStudyMaterials

JF-Expert Member
Aug 15, 2018
408
454
Sawa, najua mnaambiana kuwa hakuna tajiri aliyeajiriwa. Acheni upotoshaji, kila tajiri kaajiriwa na biashara yake na anafuata masharti na matakwa ya biashara yake la sivyo hio biashara itampiga katafunua.

Achana na hayo, nataka kuwaambia hivi wale wanaocha kazi yao ya ajira na kuanza ujasiriamali. Kwamba, kabla hujaacha kazi yako ya ajira, HAKIKISHA UNAELEWA bila kupepesa macho the power of:

1. Business Mentorship - Business nyingi zinazaliwa na kufa kifo cha ghafla kwa kukosa 'coaching' yaani kwa kukosa usaidizi ama utazamaji ama ushauri wa mtu mzoefu kwenye hio business.

2. Marketing - Niamini navyokuambia, vile unavyowaza kuwa idea yako ya biashara ni nzuri ujue ni nzuri kweli wala hudanganyi. Ila tu utaanza kuona idea yako ni ya kipuuzi kama ukikosa kufanya marketing. Bila Marketing unajitia kitanzi moyoni mwako na idea yako nzuri huku ukitazama idea yako ikifa kifo cha taratiiiiiiiiiibu bila kelele.

3. Risk Analysis - hapa mzee baba lazima ujue kila uchochoro wa mwelekeo wa business yako. Lazima uinyambuenyambue ujue jana, leo na kesho ya biashara yako. Ujue nzige wapo wapi, madudu wapo wapi, nini kimesimama, nini kitasimama, nini kitaanguka, nini kinaanguka, n.k.

Sasa, kujua hayo yote 'Read a lot' namaanisha soma sana kuhusu nini unachofanya na nini Dunia kinachofanya /kilichofanya /kitakachofanya, etc.

Nyongeza:
Business kama business yenye ufanisi mkubwa KAMWE haifanywi na mtu mmoja, bali hufanywa na watu wawili na wala sio watatu. Na kama wapo watatu basi kati yao mmoja hana nguvu yeye ni ndio mzee. Hivyo hakikisha unampata mtu sahihi wa kuwa naye kwenye business yako (hahahaha jamani nafaa nichukueni).
 
Hivi vitu vinategemeana yaani walioajiriwa na waliojiajiri tusiubeze upande mmoja, wapo wanaofanikiwa kupitia kuajiriwa na wengine wanafanikiwa kupitia kujiajiri. Pia ninayaheshimu mawazo ya mleta uzi.
 
Hivi vitu vinategemeana yaani walioajiriwa na waliojiajiri tusiubeze upande mmoja, wapo wanaofanikiwa kupitia kuajiriwa na wengine wanafanikiwa kupitia kujiajiri. Pia ninayaheshimu mawazo ya mleta uzi.
Hv kuna upande umebezwa? Au unatumia hisia kusoma thread!
 
Back
Top Bottom