Usia wangu kwa akina dada wanaochumbiwa kuolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usia wangu kwa akina dada wanaochumbiwa kuolewa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Sep 18, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,204
  Likes Received: 3,995
  Trophy Points: 280
  MAMBO 5 YA KUEPUKA MARA TU UNAPOCHUMBIWA
  Kuna mambo kadhaa ambayo msichana anatakiwa kuwa makini nayo katika kuhakikisha uchumba wake unadumu na kufikia hatua ya kuolewa na kwenda kuanza maisha mapya.
  Yapo mengi lakini nitagusia matano ambayo kwa utafiti wangu ndiyo
  yamekuwa yakiwafanya wengi wakimbiwe na wachumba wao na kuachwa wakilia.


  Mazoea na wanaume


  Wapo ambao wamejikuta wakiachwa solemba kufuatia tabia zao za kuwa na mazoea ya kijinga na wanaume.
  Yawezekana kabla ya kuchumbiwa marafiki zako wakubwa walikuwa wanaume (Wapo wanawake wa aina hiyo). Unachotakiwa kufahamu ni kwamba hakuna mwanaume anayefurahia ukaribu wa mchumba wake kwa wanaume wengine.
  Hata kama hakuna uhusiano wa kimapenzi lakini epuka sana kujichekelesha kwao, kuongozana nao, kukaa nao au hata kuwasiliana nao. Ukifanya hivyo utakuwa unamkwaza mchumba wako na inaweza kuwa moja ya sababu za kukuchenga.


  Marafiki micharuko


  Ukishachumbiwa, kuna marafiki zako ambao ¬Ďautomatikale¬í unatakiwa kuachana nao. Nazungumzia wale micharuko ambao hawawezi kukushauri vizuri juu ya maisha yako.
  Hata wale ambao wamekuwa wakikushawishi kila wikiendi muende mkajirushe, baada ya kuchumbiwa unatakiwa kujiweka mbali nao ili kumpa amani mchumba wako.


  Tabia za kisichana


  Ukishachumbiwa wewe si msichana tena, utakuwa ni mama mtarajiwa wa familia yako. Tabia za kisichana kama vile kuvaa mavazi yasiyo ya heshima, kukaa vijiweni kuongea mambo ya umbeya na nyinginezo kama hizo hutakiwi kuendelea kuwa nazo.


  Kujifanyisha


  Alichokupendea huyo mchumba wako anakijua mwenyewe, kwa maana hiyo unatakiwa kuendelea kubaki wewe kama wewe. Usijifanyishe kwa namna yoyote kama ambavyo baadhi ya wasichana wamekuwa wakifanya.


  Eti umeshaolewa


  Kuolewa ni mpaka pale mtakapoingia kanisani, msikitini nk na kufungishwa ndoa. Kama bado hamjafika huko, wewe bado ni mchumba tu na hata kwenye ndoa unaweza usifike.
  Kwa maana hiyo hutakiwi kuhamia kwa mwanaume kama ambavyo baadhi wamekuwa wakifanya. Unachotakiwa kufahamu ni kwamba kitendo cha wewe kuchumbiwa kisha kuamua kubeba virago vyako na kwenda kuishi na mwanaume ni kuwakosea wazazi.
  Msomaji wangu, yapo mengi ya kuepuka mara tu unapochumbiwa lakini haya machache yanatosha kwa leo. Jiangalie tabia zako, zile ambazo unajua wanaume wengi haziwafurahishi, jiepushe nazo ili kumjengea mchumba wako mazingira ya kukamilisha taratibu za ndoa yenu.
   
 2. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,758
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ngoja nimuite Mwali nahisi anahusika hapa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,293
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hayaaa wafunde haooo!!!!
   
 4. piper

  piper JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mafunzo murua kabisa, nataraji wamekupata barabara
   
 5. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,802
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  mh,ngoja nihifadhi huu uzi for future use. make hata mchumba sijampaja. siku nikimpata nitarudi kuusoma tena. asante MziziMkavu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 41,934
  Likes Received: 9,795
  Trophy Points: 280
  Duuuuuu! Funzo toshaaaaaa!
   
 7. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,218
  Likes Received: 7,733
  Trophy Points: 280
  Wanaume bwana siku ya kwanza tu akikuona, ameshaamua kama Atakuoa!, Atapita tuuu!, Ataonja! au Hatumbukiii kabisa! Hayo mengine ni MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI @ RTD enzi hizooo!
   
 8. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,061
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 180
  Umesomeka mkuu..nipo uchumbani sasa, hivyo inasaidia kuzidi kujielimisha!!
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,134
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  mmmhhh! Akina dada mna kazi
   
 10. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 80
  Asante sana bro, hii itanisaidia!
   
 11. MSEZA MKULU

  MSEZA MKULU JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 3,740
  Likes Received: 4,381
  Trophy Points: 280
  mkuu uso sahihi asilimia nyingi tu. hata mimi nilililawi kushindana na bibie mmoja maana yeye japokuwa ni mchumba bado analeta tabia hizo.
   
Loading...