Ushuru wa magari bandarini Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushuru wa magari bandarini Dar

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mkubwa Dawa, Sep 21, 2009.

 1. M

  Mkubwa Dawa Member

  #1
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naomba nichukue fursa hii kuomba msaada kufahamishwa kuhusu ushuru wa kutoa gari bandarini. Je kuna unafuu wowote wa kodi kwa mwanafunzi wa kitanzania aliyekuwa masomoni ng'ambo anapotaka kuingiza gari ya matumizi ya binafsi? Na kama ipo afueni ya kodi je ni asilimia ngapi inatakiwa kulipia ushuru? Vile vile nilikuwa naomba kama naweza kufahamishwa links za madalali wa magari japan.
  Shukrani.
   
 2. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hakuna msamaha wa kodi kwa mwanafuzi wa ki-TZ aliyekuwa nje kwa masomo pale anapofika nchini na kutaka kununua gari, labda uwe mtumishi wa umma tayari. Ila kama gari ulilinunua ukiwa huko ng'ambo na ukalitumia angalau kwa mwaka mmoja kama sikosei ndo kodi hupungua ukija nalo japo sijui ni kiasi gani.

  Mawakala wa magari japani waweza kutembelea links hizi hapa japo kwa uchache.
  www.autotrader.co.jp, http://www.tradecarview.com, http://ccnjp.com. www.japanesevehicles.com.

  Pia waweza kuutumia mtandao vizuri kutafuta mawakala huko maana wako wengi mno ila uwe makini kuna watu walituma pesa na hawakupata hayo magari.
   
 3. M

  Mkubwa Dawa Member

  #3
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ahsante rmashauri ntajitahidi niiingie kwa hao mawakala nijaribu kuangalia.
   
 4. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama ulinunua gari na kulitumia ukiwa huko nje kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja ukirudi nalo bongo hautakiwi kulipa kodi ya aina yeyote.
   
 5. M

  Mkubwa Dawa Member

  #5
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ahsante ndugu mwendapole kwa kunijuza kuhusu hiyo taarifa.
   
 6. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2009
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Kwa kuongezea, utalipa tu kodi ya uchakavu (chuma chakavu) kama gari ni la chini ya mwaka 2000 isipokuwa pickups/double cabin, malori, matrekta na mabasi. Vinginevyo kama waliosema hapo juu, kaa na gari mwaka mmoja nje ya nchi na utaliingiza bila ushuru
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hii sheria ya kijinga kweli, yaani ununue gari ulitumie ndio ukileta upate punguzo la ushuru, badala ya kuhamasisha kuleta gari mpya ndio upewe punguzo la ushuru, serikali yetu na sheria zake zinazotungwa na wachaga wa pale TRA zinatuhamasisha tulete ma-scrap! ajabu kubwa hii.

  Ingekuwa, ukitoka nje, kama unasoma au kufanya kazi huko, hakikisha gari lako ulilokwisha kulitumia bovu bovu, liache huko huko na jaribu kuja na jipya au jipya jipya (kama una uwezo) na sisi (serikali) kukuhamasisha na kuhamasisha wengine wafanye bidii ya kwenda nje, tutakupa ahueni ya ushuru asili mia 100. Au mtu kakaa anasoma, ka save vipesa vyake, kajinyima hata kula vizuri huko nje ili akirudi anunuwe gari japo sekeni-hendi aje nalo, naye japo aonekane kweli katoka nje, anaambiwa mpaka awe amekaa nalo huko nje zaidi ya Mwaka, sasa hii ni akili kweli?

  Hii mitunga sheria ya nchi yetu inatunga sheria za kiroho mbaya tu, misheria ya kukomoana tu. Hivi lini tutajikombowa japo kwa kuwa na sheria za kusaidiana badili ya hizi za kukomoana. Hiki kipengele cha ''zaidi ya mwaka mmoja'' kina husu nini? na kina faida gani? Hata mtu akienda katika ki semina au ki shoti-kozi cha miezi miwili, akajipatia kigari chake cha dola elfu mbili, ukimsaidia ushuru si umemsaidia maisha yake na usafiri na umehamasisha yeye na wengine kufanya bidii ya kwenda huko nje? Hii fikira ya kuwa magari ni kitu luxury, ililetwa na nani hasa?
   
 8. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukabila! ukabila! ukablia! Mkuu Dar es Salaam, sheria zinapitishwa na bunge au kuna kabila la kupitisha sheria?
   
 9. M

  Mkubwa Dawa Member

  #9
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Shukrani Hebrew ntajitahidi nitafute matrekta maana naona magari madogo imeonekana luxury kulingana na sheria za ushuru.
   
 10. M

  Mkubwa Dawa Member

  #10
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ahsante Mwalimu Zawadi lakini tumlaumu nani TRA au bunge lilopitisha sheria maana gari nadhani ni kitu ambacho mtu unahitaji kula siku lakini bado kodi ipo juu na mizengwe chungu nzima!
  Kulikoni TRA?
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mkubwa Dawa kama unataka Gari zuri pasipo na wasiwasi jaribu kuwasiliana na mimi kwa email nitakupa Contact ya mtoto wa kaka yangu anaishi UK uwasiliane nae yeye ndio shughuli zake za kununuwa magari na kuuza huko UK na ni mkweli hana wasi wasi kimaisha ukiwasiliana nae tu anaweza kukuletea hapo bongo kwa njia ya contena ili mradi mkubaliane nae bei nitumie email ili nikupe contact zake email yangu ni fewgoodman@hotmail.com
   
 12. M

  Mkubwa Dawa Member

  #12
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  MziziMkavu ntawasiliana na wewe basi kwa hotmail ili nijue kiunagaubaga zaidi. Shukrani!
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....mimi naomba kujua njia gani nitumie kukwepa huo ushuru, sitaki kukaa nalo mwaka mmoja ughaibuni!

  :mad: haiwezekani baada ya kulipa ushuru na gharama za usafirishaji najikuta nimetumia almost 100% ya bei nilonunulia 'mtumba' wangu!...

  mfano, 25% Import Duty, 18% Excise Duty, na 5% VAT yote ya nini haya wakati Wabunge wanasamehewa ushuru kila miaka mitano wanapoingiza 'mashangingi' ya zaidi ya 30m/=?
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  KWa mara ya Kwanza naoana mkuu Dar es salaam unaanza kuadmit kuwa kuna mambo ovyo Tanzania. Siku zote wewe unaonekana kuunga mkono kilakitu kinachofanywa na serikali. Siamini kama kweli ni wewe Mkuu Dar es salaam unawashambulia watunga sheria ambao siku zote unawapigania na kuwasifu. Naona kweli Idd el fitr imetuletea mengi, nawashauri jamani tuendelee kufunga akili zetu zinarudi kuwa nzuri.
   
 15. M

  Mkubwa Dawa Member

  #15
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  .... nami ndipo nafikwa na majonzi kuhusu viongozi wetu wadanganyika kwani sheria huwanufaisha wao kwanza Wabunge na wengineo na kutuacha hoi sisi hoe hae! Natamani ningeuliza hili swali la nyongeza bungeni kwa mheshimiwa yeyote. Kweli maisha bora kwa kila Mtanzania ni ndoto ya bulicheka...!
  Kalaghabao nchi imeuzwa!
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...yana mwisho haya :mad:, si unakumbuka miaka ile eti kuwa na Colgate, TV na VCR au $ USD ni mhujumu uchumi? au kuendesha gari jumapili unavunja sheria?

  ...kubadilisha " ...zidumu 'fikra za mwenyekiti wa CCM'" itatuchukua muda sana!

  Wengine wanajiuzia kwa 10% ya bei walionunulia magari Brand new, ...yaani mtumishi wa serikali ana Vogue, BMW, au Merc M class,...kwa jasho la naaaaaaaaani?....

  Bora sie walala hoi tutafute njia za kukwepa ushuru kwa hali yeyote ile. Nipeni mbinu...
   
 17. Naumia

  Naumia Member

  #17
  Sep 22, 2009
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na wewe kabisa. Mimi mwenyewe nimemaliza shule nikanunua kigali changu back in June 09, na nillikuwa najiandaa kurudi nyumbani in December 09 sasa naambiwa inabidi nikae na hili gari kwa mda wa mwaka mzima...balaa tupu. Nimejaribu kupeleleza lakini ukweli ndiyo uwo na pia nimeambiwa kwamba still kuna percentage ntakayo lipa even though gari langu ni la 2006..ItÂ’s not going to be 100% free.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wachaga nao, Tanzania hakuna ukabila, Tanzania tuna watani tu, sasa kama wewe unajuwa mtani wa Mchaga ni nani basi utajuwa kabila langu ni nani!
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Labda hujasoma vizuri post zangu, mie namuunga mkono JMK kwa nguvu zote. Na hapo juu huoni nilivyo-wa-kandia Wachaga?
   
Loading...