Ushuru wa magari Arusha hadi ni kero kubwa.

LENGIO

JF-Expert Member
Apr 9, 2012
1,096
508
Aliyepewa tenda ya kukusanya ushuru wa magari arusha ana njaa kali anakusanya ushuru hadi mochwari na vituo vya polisi hadi benki kuu na tra.Ccm mnatupeleka wapi?
 
Ushuru wa magari Arusha noma ndugu yangu, ukijichanganya stand tu jua buku limekutoka wakati Ubungo kuingiza gari na kupaki na kutoka 300!!!!
 
Yaani huu ushuru ni kero hapa morogoro unapaki sehemu yoyote hata kama unaangalia pacha utakuta mtu wa kukusanya ushuru amefika....Huu ni ujinga kama munispaa inataka mapato kwanini wasijenge parking......Hii ni kero kwakweli. Na hata hizo pesa zinazokusanywa hatuoni maendeleo yoyote hii nchi tunaipeleka wapi? Viongozi hawaoni haya? au ndio miradi yao?
 
ni wapuuzi sana hawa watu wanaokusanya ushuru, hata ukiingia mahali ukakaa dakika kumi au tano lazima ulipe elfu moja, mimi kuna siku nimekataa kulipa na nikaondoka kwa sababu nilikuwa nataka kuibiwa kitendo cha kupaki nikamshusha mtu stand alikuwa anaelekea babati eti nikasikia wanakuja na myororor wao kwa nyuma wananifunga, ilitokea mtiti wa kufa mtu ikabidi waniachie wenyewe
 
Kwa kweli ushuru wa maegesho Hapa Arusha umekuwa kero kubwa ukienda stand kubwa ya mabus wanatoza ushuru usiku kucha mchana kutwa, kibaya zaidi wanatoza ushuru mpaka siku za sikukuu zakitaifa.
 
Back
Top Bottom