Ushuru wa Mafuta Unatuumiza, Kenya washapunguza JK tafadhali Waige Majirani Zako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushuru wa Mafuta Unatuumiza, Kenya washapunguza JK tafadhali Waige Majirani Zako

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Uswe, Apr 19, 2011.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mashara wangu unakatwa 30% PAYE. kile kidogo kinachobaki, kwa kila elfu mbili ninayolipa kununua lita moja ya petroli serikali inachukua sh. 600, Kumbuka hii ni baada ya kunikata 30% kwenye mshahara wangu hata kabla haujafika mikononi mwangu!

  Kenya wananchi wamepiga kelele na serikali imesikia, Leo katika KBC nimesikia serikali IMEPUNGUZA KODI ya mafuta ili kumpa ahueni mtumiaji wa mwisho, Naishauri Serikali ya Tanzania Ifate mfano huo.

  Katika nchi nyingi middle east retail price ya petroli ni kati ya sh 240 hadi 500 kwa lita, najua kuwa wao ndio wazalishaji wa mafuta na kuna gharama inatumika kabla mafuta hayajatufikia sisi lakini bei inatokaje sh 240 pale Saudi Arabia, au sh 255 Libya au sh 285 Quatar na kufikia sh 2100 Tanzani kwa Lita?

  Crude oil kwa sasa ipo at $ 110 per barrel ambayo huwa na around 142 Litres of crude oil, na hii barrel moja ikiwa refined unapata

  Petrol Lita 74
  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]distillate fuel oil Lita Lita 35
  [/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]kerosene-type jet fuel Lita 15.5[/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]
  [/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]residual fuel oil Lita 9[/FONT]
  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]liquefied refinery gasses[/FONT] 1.9 gallons
  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]still gas 1.[/FONT]9 gallons
  Coke 1.2 gallons

  na mazagamazaga mengine mengi, Ukiangalia huo mchanganuo hapo utaona hata kama barrel moja ikifika $ 180 bado bei ya lita moja sokoni haitakiwi iwe 2100.

  Serikali has to do something.

  Nawasilisha!
  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]
  [/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]
  [/FONT]
   
 2. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  duh nashukuru kwa mchanganuo! kumbe ni wizi mtupuuuu lazima tuandamane ila isije kuwa kama kwa MU7 amewapiga biti wasithubutu kuandamana
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mkuu hapa tz kodi ni nyingi mno.ktk kila lita moja kuna makato yafuatayo
  TPDC wanachukua chao
  TIPER wanachukua chao
  TANROAD wanachukua chao(wakati wateja wengine hawatumii barabara,ie meli,train na generators)
  INCOME TAX wanachukua chao
  EWURA wanakula chao
  Kuna mfuko unaitwa PRICE WINDFALL wa kubalance bei wanakula chao
  Mwenye kituo cha mafuta anakula chake...
  Bado gharama halisi za kuzalisha na kufikisha hiyo bidhaa hapa
  hapo si lazima bei ifike 2100
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  ndugu 60 percent ya sh 2100 ni hizo kodi uchwara za govt!ina maana kenya mafuta itakua Tsh 1200 kwa lita!moshi arusha tanga mara tukae mkao wa kutumia mafuta ya magendo toka kenya! Mimi naona hiyo ni sababu tosha ya kuandamana kudai wapunguze kodi,deficit ijaziwe na pembe za tembo wetu wanazouza kimagendo kwa wachina!
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ahsante Uswe na Inko!
  Afu hapo watakuja wachumi sijui watakwambia china inflation imefanyaje sababu marekani kaenda iraq sijui hata brazil...... upuuuuuuuuuuuzi tu, hivi viserikali legelege kama vyetu hapa bongo wala havina ubunifu kwa maisha mema ya watu wake,
  wizi mtupu!
   
 6. U

  Uswe JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Na Ukumbuke hizo kodi ni zile tunaita indirect tax, wakati huo tayari unakuwa ushagongwa direct tax ambayo ni PAYE, yaani hapa Tanzania Income unayopata almost 50% inaenda serikali kama kodi (both direct na indirect)

  Je tunapata thamani ya kodi yetu? Je hizi pesa zinazokusanywa na serikali kupitia kodi zinafanya kazi gani? si ndio hizi zinatoa ruzuku kwa vyama badala ya kununua dawa za hospitali? si ni hizi zinalipa wanasiasa marupurupu ya ajabu wakati hatuna vyoo wala vitabu mashuleni? Ni wakati sasa tuhoji kwa nguvu zote namna kodi yetu inatumika
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wakuu nimesoma hii michanganuo miwili na nikajiuliza sana, kweli kuna uhalali wa bei ya mafuta kufika 2100.. nikaona hakuna uhalali wowote... inabidi tuamue kweli kabisa kwa dhati ya mioyo yetu tufanye mabadiliko tumechezewa sana sasa inatosha. Waliua tipper makusudi ili wawe wanajipangia bei sababu wao ndio waagizaji. Kuna haja ya kuandamana kuishinikiza serikali ifanye inavojua bei ya mafuta ishuke!!
   
 8. U

  Uswe JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kenya wananchi wameonesha nia tu ya kutaka kupinga na serikali ika-act fasta kwa kupunguza ushuru, tukumbuke wanasiasa hawaathiriki sana na bei za mafuta wala kiwango cha kodi, kwa sababu wao ndio watunga sheria wana exemptions kibao, we ushawahi kujiuliza kwa nini wabunge hawalipi kodi? kwa nini vyama vya siasa vipewe ruzuku? kwa nini serikali kila asubuhi wanaongeza tu kodi hata siku moja hawawazi kupunguza? ITS ABOUT TIME WE START QUESTIONING HOW IS GVT USING OUR MONEY!
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  kenya hata bidhaa za viwandani hushuka na kupanda bei kutokana na hali halisi ya gharama.Tanzania sijawahi ona bidhaa ikishuka bei mpaka kuwe na shinikizo la bidhaa pinzani ya nje
   
 10. U

  Uswe JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wanasiasa ni wanyonyaji, wenyewe hanajipa exemption ya kodi na wanatumia pesa za walipa kodi kula raha
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,464
  Likes Received: 5,707
  Trophy Points: 280
  mmhh huyu akili zake atapunguza mafuta ya taa pekee tuongezewe michakachuo kwenye magari yetu loh..wacha yabaki hivihvi
   
 12. U

  Uswe JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kodi kwenye mafuta ishuke
   
Loading...