Ushuru wa kusainiwa mkataba kwa Serikali za Mitaa ni halali?

Green_Touches

Member
Dec 25, 2016
67
18
Heshima kwenu wakuu.

Kuna hili suala limenipa utata, nilipeleka mkataba wa makabidhiano ya Chombo cha usafiri Serikali za Mitaa ili usainiwe sehemu husika ili kuthibitisha makabidhiano yetu kama wakazi wa mtaa wake.

Lakini cha kushangaza Mwenyekiti alikataa kusaini mkataba huo bila malipo anayodai kuwa ni Ushuru wa kusaini Mkataba. Je, kuna uhalali wa Ushuru huu na ni Ushuru ambao unatambulika kisheria na upo katika Serikali zote za Mitaa au ni huku kwetu tu?

Nahitaji msaada kuhusu hili maana kumekuwa na usumbufu mwingi kwa serikali zetu za Mitaa na Wenyekiti kufanya Ofisi sehemu ya Biashara kujipatia kipato.

Asanteni sana.
 
tena hujanikitu mm nikikaimu bila 10% siweki sign na kugonga muhuri 1000-2000
Sasa mkuu hii ya 10% inatambulika kisheria kwamba ni tozo halali kwa wananchi wanaohitaji huduma hii.
Na je kunakua na stakabadhi yoyote inayohalalisha malipo ya ushuru huo wa 10%.
 
Sasa mkuu hii ya 10% inatambulika kisheria kwamba ni tozo halali kwa wananchi wanaohitaji huduma hii.
Na je kunakua na stakabadhi yoyote inayohalalisha malipo ya ushuru huo wa 10%.
Elewa kitu kimoja tu....Siku hzi hakuna cha bure
Ukienda setikali za mtaa,Ukienda mahakamani ni hvyo hvyo.....

Ova
 
Sasa mkuu hii ya 10% inatambulika kisheria kwamba ni tozo halali kwa wananchi wanaohitaji huduma hii.
Na je kunakua na stakabadhi yoyote inayohalalisha malipo ya ushuru huo wa 10%.
hio 10% ipo na risiti unapewa kabisa lakini hizo zingine sikupi risiti sababu nizachai nanauli na nisiri na si lazima
 
kwani wako kwenye payrolls? tuanzie hapo kwanza! mkuu hata kwenye nyumba za ibada kuna sadaka ambayo imezoeleka ni utamaduni wa kumtolea Mwenye enzi lakini machangizo, mafungu fulani, zaka, sehemu ya 10/fungu la kumi/kutegemeza/shukurani/changizo la mahitaji maalum haviepukiki. fumbua macho zamani cha bure ilikuwa salamu. saivi salamu inataka vocha. kama ni laivu msalimie msela/mdada atakuacha na neno NINUNULIE CHAI; utadhani wewe ndiwe mlinzi wa safe za world bank!
 
Hiyo kisheria ya utendaji na katiba ya serikali za mitaa haijatoa idhini kwa mwenyekiti au watendaji kutoza pesa yoyote ila kwa mwananchi ambayo haipo kisheria hivyo suala hili la watu kutozwa pesa pindi unaenda kweny serikali za mitaa mfano: kutoa 2000 ya marua ya Utambulisho nikosa kisheria
 
Back
Top Bottom