Ushujaa wa askari huyu ni wa kipekee, wadau tumpongeze

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,191
Katika hali isiyo ya kawaida askali wa kikosi cha zimamoto nchini huko mkoani Kagera wilaya ya Ngara, amefanikiwa kumuokoa mtoto mchanga kutoka kwenye shimo la choo kwa kutimia kamba ambayo ilishikiliwa na wananchi ili aweze kuingia shimoni kumtoa mtoto huyo.

Hapa chini ni kipande cha sinema kikionyesha tukio hilo, ila mtu yeyote anayemfaham askali huyo hebu PM nimcheki kwa pongezi kidogo.

NB: Pamoja na ukosefu wa vitendea kazi kama tunavyoona kwa mabeberu ila jamaa katumia taaluma yake ipasavyo na wananchi kumpakampani iliyotakiwa 👏👍.


UPDATE:
Kopro Denis ambaye aliyemuokoa mtoto anayekisiwankuwa na umri wa mwaka mmoja, amefanya maamuzi ya kipekee kwa kuamua kumchukua mtoto aliyemuokoa ili awe mmoja wa familia yake na kusema atamlea na kumpa huduma zote kama mtoto wake.



PICHA 👇:
Binti akiwa na furaha pamoja na afya inayoendelea kuimarika, picha inayofuatia chini akiwa amebebwa na mwanafamilia huku Copro Denis akiwa pembeni.
Picha kwa hisani ya Ukwaju.
2410549_1590614764724.png


2410548_1590614704232.png
 
Sioni jambo la kishujaa hapo sana sana tu tunamshukuru kwa kuokoa maisha ya mtoto. Hiyo ni kusema ame apply kwa vitendo mafunzo aliyopewa akiwa chuoni.....

Wakati mvua za masika zikiisha hapa Dar, nikiwa ofisi kwaku,kwa mbele hapa maeneo ya Kimara-Suka kuna mto umepita halafu kuna kidaraja ambacho huwa maji yakizidi huwa yanapita juu.

Sasa kuna binti mmoja alitaka kupita lakini hakuwa na uelewa vizuri wa lile daraja kwa bahati mbaya alikanyaga upande wa pembeni akadumbukia na maji yalianza kum-push kuelekea chini ya calvati ka daraja.

Kwa bahati mzuri niliona, nikapiga mbio fasta nikazama mule majini nikambeba na kutoka nae. Hayo ni maji yaliyokuwa yanakwenda kasi na sina mafunzo yoyote ya kupiga mbizi.

Kwa hiyo kwa kitendo alichofanya askari huyo sio ushujaa coz ameapply kile alichofundishwa, no any extra-ordinary skills.

Lakini, tunamshukuru kwa kujitoa kuokoa maisha ya mtoto huyo👏👏
 
UJUE MAZOEZI YA KUSHUKA NA KAMBA WANAFANYA KILA SIKU! Wakati mwingine wajibu wa mtu tusiugeuze story!
Mbona madakitali wanapasua watu matumbo hatusemi? mbona wajenga minara wananing'inia hewani kuhatarisha maisha tunachukulia poa tu, mafundi ujenzi maghorofani wanajenga zote hizo ni kazi za risk! Iweje leo KUSHUKA na KAMBA iwe story Wakati mtu yupo kazini?

We must change!
Kila mtu awajibike ipasavyo!
Humo kwenye shimo kaingizwaje huyo mtoto? anyway!
Let us be fare!

Hapo TULIPASWA KUAMBIWA TAARIFA ZA ZIMAMOTO ZILILIPOTIWA MDA GANI KWA SIMU GANI, NA RESPONSE IKAJA MDA GANI?

Maana ukitaka kuelewa ZIMAMOTO wanawahi au kuchelewa piga namba yao halafu utueleze Kama umefanikiwa kuwapatahewani chap
 
Yericko mwenyewe na yeye ana kopi. Ngoma draw
Unapenda sifa sana lakini bahati mbaya huna kitu kichwani we si ndiyo uliekopy na kupaste maelezo ya Yeriko ukayaleta jukwaa la intelligence ... Yeriko aka kushukia ?
 
Tumezoea (ingawa sio vyema) kusikia vichanga wakitupwa ila hii mmh hatari, mkubwa mkubwa hivyo ujasiri wa kumtupa unatoa wapi!
 
Back
Top Bottom