Ushuhuda: Wauzaji wa Trekta Afrika Kusini

Hongera sana kwa mapambano kama trekta ya case haikusumbui kuna mtu kanunua mwaka hana August 2021 leo limekata ring hata waranti haijaisha na wamegoma kurekebisha
 
Hivi ni Trekta aina gani zuri kwa ubora wa kazi ?
Nina mpango wa kununua moja nijalibishe biashara ya kulima mashamba ya watu kwa malipo hasa mkoa wa Morogoro eneo la Ifakara, ambako wakulima ni wengi.
 
Wale wadau wa trekta kuna wasap group tukutane tusaidiane ushauri na utatuzi wa haya mambo nicheki 0653 639214
 
Ni sahihi mimi nilitoka huko kabla ya uzi huu. Yakanishinda nikachukua Case used 3,000 hrs kwa 39.5m pamoja na jembe. Mkuu ile Swaraj inakamua balaa
Mm nlienda July 2021 pale suma jkt ilikuwa 48.6m 4w 75hp ila kwa sasa ni 52.8m wanasema ukichelewa kidogo itafika hata 56m ukienda msimu sio wa kilimo bei inakua cheee last month nmechukua case 53m ila ikifika October nazan takua hata 58m na yule wa jembe chapa samaki saizi ni 10.2m ila kanambia wakileta mzigo mwingine takua zaidi ya hapo
 
Wale wadau wa tractors manunuzi matengenezo ushauri kupeana connection na kusaidiana tukutane wasap group kwa link hii Wadau wa tractors bongo
 
Mkuu nashukuru sana. Barikiwa sana, huu uzi nilianzisha baada ya kuona tractor zinauzwa bei nzuri sana SA. Nami nipo njiani kufanya maamuzi magumu. Bahati mbaya tu mi nimekuwa mpenzi sana wa Massey Furgudon, hasahasa MF 290.
Mkuu, tayari ulishapata chuma?
 
Mkuu nakushauri tafuta fundi anayezijua zaidi MF akuambie changamoto zake na kama utamudu kuzikabili. wakati natafiti kila fundi na opereta waliniambia MF inazingua sana hydrolic nikaacha nazo.
Kumbe ndiyo mchezo wake? Kazini kwangu nilishawahi kutumia MF ilikuwa inasumbua sana hydraulic, kila muda ki-pini kimechomoka kinadondokea humo ndani, ilikuwa shida sana mpaka tukaachana nayo! Sikujua kwamba ndiyo tabia ya MF zote aisee!
 
Hodi huku
Kumekuwa na nyuzi humu zikijadili uimara wa trekhlta zinazouzwa mitandaoni South Afrika. Uimara huo umekuwa ukitiliwa mashaka kulinganisha na bei ya trekta hizo. Ukiingia kwenye mitandao mingi utagundua bei ya trekta zilizotumika muda mfupi zikiuzwa mpaka milioni 15.

Achana na stori za mitandao na simulizi. Mwanenu huwa sikubali kushindwa nilifunga safari mwenyewe mpaka South. Twende taratibu nikupe udondozi wa shuhuda.

TRA na TBS
Kabla ya chochote nikaingia TBS kujua taratibu na gharama za ukaguzi.Nikamuonyesa msela picha kadha wa kadha ili anipe ABC. Kwanza akanipa hongera kichizi,akanitakia kila la kheri niingize chombo nizalishe chakula watu wale washibe. Akaniambia gharama ni laki 3 mpaka laki 4 na kazi inafanywa na NIT. Taratibu ni kwamba kama kutakuwa na hitilafu wataandika ripoti nirekebishe.

Baada ya hapo nikaendesha ndinga mpaka TRA waniambie ushuru ukoje, sio nilete chombo halafu kipigwe mnada. Jamaa akaniambia hakuna kodi kwenye trekta ila kuna ushuru kidogo tu nitalipa kama 0.6% na 1.6% ya bei. Nikampa invoice mbili tatu za wauzaji wa South zenye around 15m mpaka 20m tukaona haizidi laki 5.

Nikaona usinichezee,moja kwa moja nikaenda kupima Covid 19 tayari kwa kusafiri.

South Africa
Kabla sijaondoka nilikuwa na sample ya sellers kama 5 hivi ikiwemo niliopewa link na wadau humu. Watatu nikiwa na invoice zao tayari. Muda mwingi walikuwa wananipiga sound nilipe tu wanitumie mzigo. Sikuwa napepesa macho niliwaambia siwezi kuwa fala,nakuja mwenyewe kuangalia chombo nitafute fundi akague ndio nilipe. Mara oooh invoice ita expiry,nawaambia utaandika nyingine kwani shida iko wapi.

Moja kwa moja nikadondoka Cape Town ambapo ilionekana wauzaji wengi wapo kule. Nikaanza na wa kwanza ambaye mzigo wake ulinivutia sana. Nikampigia simu ku book appointment kesho asubuhi namtimbia. Akaniambia wamefunga wamehamia Pritoria. 🤣🤣 nikamwambia kwa kizungu we ni tapeli? Tumewasiliana kila siku unasema upo Cape Town,adress yenu inasoma Cape Town. Hakujibu.

Nikamcheki wa pili. Huyu adress ilikuwa na geogle location. Nikachukua uber kufika hapo hola kuna malls tu wala hawatambuliki. Kuulizia naambia wewe ni mtu wa 3 leo anaulizia hao jamaa.

Siku ikakata ikabidi nijisalimishe kwa mwanangu mmoja huku bongo aliwahi kuishi South miaka ya 2000s. Akaniunganisha na muhuni mmoja hivi mbongo. Sasa yule ndio akanipeleka kwa wenyewe kabisa.

Uhalisia
Hatimaye nikafika kwa wauzaji halisi wa trekta mpya na used. Kiukweli bei tunazodanganyana humu ni bei za matapeli tu. Lakini uhalisia ni tofauti na hakuna tofauti kuuubwa na bei za kina Chriss Lukosi na wauzaji wengine. Japo kwa mtu mwenye muda wa kutosha anaweza kupata trekta lililotumika mwaka hadi miwili kwa bei ya 30m.

Nikafanikiwa kupata trekta New Holland kali sana TT75 kwa 29m. Ngoma ikiwa kwenye muda wa kusafirisha ungepishana na msimu wa mvua. Kusafirisha kwa meli ambayo ni nafuu inachukua 14 mpaka 21days. Nikaona isiwe tabu hii milioni 2 ikipotea sio issue sana ngoja nikakomae tu huko huko. By the way nimekula bata na pisi mbili huko sio haba

Baada ya kurudi Tz nikapambana tena nikapata Case HP 75 4WD kwa 39.5m kwa mwarabu mmoja hivi.

Nitakuja kuhitimisha baadae,ngoja nitafute vibarua huku Iramba.

SA Wana madini hatari
 
Back
Top Bottom