USHUHUDA: Watanzania tuwe wakweli juu ya ufugaji wa kuku

Kak
Tena usipojipanga kwenye chakula utasema umelogw maana kuku wanakula hatari kama viwavi unaeza nunua gunia la pumba ukatengeneza chakula manina hat mwezi gunia halitoboi daah,hakuna jambo rahisi chini ya jua
Mkuu lkn walikupa faida?!!
 
Tanzania kuna upotoshaji mkubwa sana, wengi wetu ni waongo waongo sana. Penye ukweli tunapindisha.

Ili ufuge kuku wa kienyeji, tena kwa banda la hali ya chini kabisa, ni lazima uwe na vitu vifuatavyo :-

(Kwa banda la mita 9 kwa mita 3)

1. Eneo la kutosha kwa ajili ya banda

2. Muda wa kutosha kuwahudumia kuku

3. Uwe na mtaji wa siyo chini ya Milioni 1.5 kwa ajili ya kujengea banda tu

Gharama ya fundi siyo chini ya laki 1.5 , mabati used siyo chini ya mabati 15 @ 8,000 TZS , matofali ya kuchoma 800 300 TZS, misumari ya bati 2 kg @ 5,000 TZS , Binding wire , bawaba , cement 12 bags , kufuli 1 @ 5,000 TZS , kitasa 1 @ 4,000, mbao ( 2 x 2 , 3 x 2 ) 800 Rft , mirunda 12 @ 5,000 TZS , Chicken mesh 1 Roller 80,000 TZS , Wavu mgumu 2 Rollers @ 12,000 , usafiri na mengineyo madogo madogo.

4. Uwe na walau laki 3 za kununua kuku wakubwa wanaokaribia kutaga

Ikumbukwe tu , kuku 1 ni kati ya TZS 10 - 15,000

Watanzania tuwe wakweli , tuache uongo na ushabiki wa vitu tusivyovijua kwa vitendo.
Tatizo sio la watanzania tatizo ni la kwako, umeshindwa kung'amua huo ufugaj wako kwa hizo gharama utaufanyia wapi na unaanza na Kuku wangapi? Kwa huo mtaji unaouzungumzia maana yake unataka kuanzia na mradi Mkubwa kidogo lakin mtu anayetaka kuanza angalau na Kuku 10 au 20 hawezi kutumia mtaji huo au hata Kuku 50 mtaji huo ni mkubwa, Mimi nilitengeneza banda la fut 5 kwa 6 likawa na floor mbili kwa sh. 250000/=, nilinunua kuku 12 wa miez mitano walianza kutaga kwa sh. 12,000/=@ walitaga mayai nikakusanya trei moja ndani ya siku 4 nikaenda kutotolesha nikapata vifaranga 26 ambavyo nilivilelea mpaka vikakua, kwa mtindo huo huo nilifikisha Kuku 60 walipokuwa nikawauza wote, kuna changamoto ilinikabili, chakula wanakula ndio lakin kama unawafungia bila kuwaruhusu hapo watakukost, kwahiyo ni vile unachukulia,mambo ndo yanavyokuwa
 
Tatizo letu tunataa faida ya fasta fasta ndo shida yaani unataka ufuge ndani mwezi uanze kula faida hicho kitu hamna utaishia kusema waongo, cha kuelewa ni hiki kila mradi una changamoto zake ila ukiamua ni kupambana nazo
 
Kwa kuwa wafugaji wengi hawahitaji kujifunza ndo maana wanahangaika na chakula. Mimi natumia ngano, naotesha chakula (Hydroponics Fodder) - ambapo kilo mbili za ngano zinanipatia chakula kilo 14/16. Hizo ngano kilo moja naipata kwa gharama ya Tshs. 1,200 / 1,500. Hivyo suala la chakula kwangu sio shida; labda changamoto inakuja kwenye muda wa kuotesha - zoezi hili la kuotesha ni endelevu kama kupiga mswaki kila siku ila unapata chakula bora kwa gharama nafuu.
Kuhusu virutubisho natumia EM.1 ambayo lita moja inanipatia lita 20 za virutubisho ambavyo naweza kutumia mwaka mzima na kiasi kingine nikawauzia wafugaji majirani wanaoona umuhimu wa hivyo virutubisho.
Kwa ujumla nimekuwa mfugaji kwa muda mrefu hadi nimeona kuwa kufuga ni namna unavyoji-tune kufanya hiyo kazi.

Mkuu naomba Msahada tutani EM.1 ndo nini?
 
Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo. Karibu kituoni kwetu nikupeleke sehemu ninapofanyia shughuli hizo uone kwa macho yako. Sifichi chochote kwa sababu najua watanzania ni wazembe kutenda. Hata ukiona najua hutakuwa mshindani kwangu kwa sababu tayari umelemaa fikra.

Mkuu unafugia maeneo gani nikutembelee, mimi nipo Dsm
 
Mkuu inategemea mwezi wa 9/2018 nimetumia laki 5 kujenga banda lenye ukubwa wa 3*5M
Nikanunua kuku 5 jogoo 1 na tetea 4 kwa 67,000
Nikanunua chakula nikachanganya mwenyewe pumba debe 7 mashudu,dagaa, chokaa, mifupa tolat 48,000
Chanjo ya kideri 7elfu!
Mpaka sasa nina vifaranga 43 wana mwezi sasa.ninewanyanganya mama yao Nategemea mwezi wa1 2018 wataanza kutaga tena!
Ukisikiliza wanaopinga wanadhani garama za ujenzi zipo costant nchi nzima!!
Kuna amabo wana access ya kupata mabanzi... Pia wapo wenye accesa ya kupata used playwood so inategemea.

Unaweza kuanza hata kwa laki 2 tuu

Ahsante sana mkuu
 
Mkuu naomba unijuze hiyo EM. 1 ni nini hata kama ni pm
Napenda sana kufuga kuku na ninao kama 50 hv we nimekuelewa sana ila mleta mada kwa kweli hapend watu wafuge me nmetengeneza banda na kununua kuku wale wenye mwezi mpaka miezi 2 hata laki sidhani kama ilifika mpaka ss kuku wanajitegemea chakula wenyewe mana nauza mayai nawachukulia vyakula
Kwa kuwa wafugaji wengi hawahitaji kujifunza ndo maana wanahangaika na chakula. Mimi natumia ngano, naotesha chakula (Hydroponics Fodder) - ambapo kilo mbili za ngano zinanipatia chakula kilo 14/16. Hizo ngano kilo moja naipata kwa gharama ya Tshs. 1,200 / 1,500. Hivyo suala la chakula kwangu sio shida; labda changamoto inakuja kwenye muda wa kuotesha - zoezi hili la kuotesha ni endelevu kama kupiga mswaki kila siku ila unapata chakula bora kwa gharama nafuu.
Kuhusu virutubisho natumia EM.1 ambayo lita moja inanipatia lita 20 za virutubisho ambavyo naweza kutumia mwaka mzima na kiasi kingine nikawauzia wafugaji majirani wanaoona umuhimu wa hivyo virutubisho.
Kwa ujumla nimekuwa mfugaji kwa muda mrefu hadi nimeona kuwa kufuga ni namna unavyoji-tune kufanya hiyo kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufugaji wa kuku ni uwekezaji kama ulivyo uwekezaji mwingine. Hivyo lazima ujipange kimtaji na uwe tayari kukabiliana na hasara yoyote itakayojitokeza.
sio kukabiliana na changamoto, ufugaji kuku wa jienyeji ni biashara unaanza na hasara mkononi. Kifupi hakuna kuku wa kienyeji mjini, wapo vijijini. Mazingira ya mjini hayatoshelezi kuwapa nafasi ya uasilia. Matokeo wanafugwa kama wa kisasa na ubora wa nyama na mayai kuwa duni.
 
Wafugaji wa ndege ( hasa Kuku) serious naona hawajachangia kabisa kwenye huu uzi.
Kiufupi niwashauri wanaotaka kufuga kiuhalisia na wakaona faida ya ufugaji wa ndege hasa Kuku wa Kienyeji, Mayai pure( layers) au chotara, angalau Uwe na Kuku wengi waliofikisha umri wa kutaga ndipo utaona faida ya ufugaji huu tofauti na hapo inakuwa unaishi na ndege....nazungumzia economies of scale....
Ufugaji wa kuku ni uwekezaji, ni biashara yenye tija ikiwa utaiona hivyo.
 
Back
Top Bottom