Ushuhuda wa familia yetu: Nguvu kubwa itumike kuwafundisha watoto kujitegemea ili wasisote kama sisi wahitimu wa vyuo

Dah!

Waafrica sasa tumeanza kuamka! Hongera kwa kujiongeza chief!

Mi binafsi now Nina 34 yrs lakini bado nazurura, sina uhakika wa maisha na hii yote sababu sina ujuzi

Ujuzi ni muhimu Sana kwa maisha ya sasa

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Nachoamini ni kwamba mtu hujifunza mambo ambayo yanadumu kichwani pindi awapo chini ya miaka 18.

Ni mda huu wengi wanakazania watoo kushika namba moja shuleni, matuisheni hadi weekend, kuwapelekea watoto shule za boarding kwa fasheni, kupiga watoto wasipofanya vizuri darasani, n.k Hali hii inamfanya mtoto awe anajua elimu ya darasani tu, kimbembe kinaanza mtoto kamaliza chuo na lafaulu vizuri tu lakini ndio hivo tena kupata kazi sikuhizi ni ngumu sana.

Binafsi kwa sasa navyolea watoto wangu, moja yupo shule ya msingi ila namlea nikiwa na taswira kwamba akimaliza chuo atakosa ajira japo siombei iwe hivi ila ni kuangalia uhalisia, Najitahidi na ntajitahidi kadri niwezavyo awe na ujuzi katika mambo mbali mbali yatayomsaidia hata akikosa ajira,
 
Coaster alinunua kwa kukopa au shughuli hizo hizo za kinyozi?
Mkuu hata sina uhakika, ila nakumbuka kile kipindi biashara alizokua anafanya nilizozijua mimi ni kuwa kinyozi na kuchezesha hii michezo ya video ambayo ilimwingizia pesa nzuri tu kila siku.
 
Yaani acha tu, braza alipoanza kuwa kinyozi wengi sana walimnyoshea vidole na kumcheka kwamba ana masters na hana ajira, kitu kilichomsaidia braza ni elimu yake kuitumia kwenye harakati zake tangu kaanza kuwa kinyozi, alikuwa na elim kwa hio haya mambo kama kutunza pesa haikuwa shida kwake, leo hii mtu hawezi kuamini kwamba alikuwa kinyozi.
Mtaji alipata wapi boss?
Alianza nishingapi kwanza??
 
Habari zenu wakuu,

Leo nmeona nitoe neno hapa, zama zimebadilika wadau, Kukazia elimu zamani ilikuwa ni kujiongezea uhakika wa kujitegemea ukiwa mkubwa kwa kuajiriwa serikalini au kwenye makampuni.

Na hata mimi binafsi kwenye familia yetu wazazi wetu walituasa sana tusome sambamba na adhabu kali na vipigo barabara pale tuliposhuka uwezo darasani.

Tupo wanne kwenye familia, wote tumemaliza vyuo, brother ana mssters, sista ana degree, mimi nina degree na cpa, mdogo wangu ana masters.

Ni mimi peke yangu ndie niliebahatika kupata ajira serikalini.

Hao wengine wamesota sana hizi ajira, nakumbuka kipindi flani braza na sista walimlipa kiongozi wa shirika flani ili tu wafanye kazi hapo kwa kujitolea ili waingeze experience na ikiyokea bahati basi waajiriwe lakini matokeo yake hata ajira zilipotangazwa nabinterviews kufanyika hawakuchaguliwa, inauma sana.

Baada ya kuona msmbo sio mambo na muda unaenda, braza akawa amechoka sana, braza akakodi frem akawa ni kinyozi, nakumbuka sekondari blaza alikuwa ni kinyozi wa shule yao huko boarding kwa hio ujuzi alikuwa nao, basi kutokana na umahiri wake na kuwa na wateja wengi aliozoeana nao kidogo blaza stress zikaanza kuisha, akajichanga akanunua hizi playstations michezo ya video akawa anachezesha mfuko ukazidi kutuna, biashara ikawa imenoga akajaribu kuweka costa barabarani zinazoenda wilaya nyingine.

Muda ukaenda akaongeza nyingine nae akanunua gari ya kutembelea, maisha yakaanza kuwa safi, saizi navyoongea hapa braza yupo vizuri angalau, ana miradi mingi tu lakini ile biashara ya kinyozi hajaifunga na ni lazima kila mwezi aende pale hata siku moja atshinda pale ananyoa wateja wanamshangaa, na kinachomsaidia ni kwamba ana elimu na anaongea kiingereza fresh tu kinachimsaidia. Kajenga nyumba, mke wake nae ana biashara yake ya duka kubwa tu la vipodozi, watoto wake wanasoma shule private.

Kwa upande wa sista aliolewa lakini hajakaa kizembe, tangu zamani sista alikuwa anapenda sana kupika, ndo kalenga biashara yake hapa alianzishaga kupika chakula home then anaenda kuuza kwenye frem yake, pesa akaingiza akafungua kamgahawa ka kizushi anapikia huko huko, bwana wake akamuongezea mtaji saizi ana restaurant na kama ni pesa anazichapa.

Kwa huyi mdogo wangu, mtoto wa mwisho, nae ajira ka apply sana japo ana mwaka moja tangu amalize chuo, anaendelea ku apply lakini tukamshika mkono asizubae wakati anaomba hizo ajira, kwa sasa yupo kwa braza ndie msaidizi wa blaza, na braza anampa mshahara wa laki 6 kila mwezi, tunategemea kumchangia mtaji aanze biashara yake akifikia miaka 26, Kwa sasa ana 24 tumeona bora ajifunze funze kwa braza biashara kwanza.

Kuhusu mimi kiukweli nimepata kuwa na wivu wa kimaendeleo, yani pesa anayoingiza kaka na dada kwa miradi yao, pamoja na huu mshahara wangu wa muhasibu mwenye degree + cpa serikalini bado siwezi kuwafikia kipato chao, hali hii ikanifungua akili na kuacha kuridhika na mshahara, mwaka juzi december nilifungua biashara ambayo nilipata changamoto sana hususani za kuibiwa ila nilisaidiwa sana kuzitatua kwa kutumia ushauri wa kaka na dada, Biashara yangu kwa sasa faida inayoingiza kwa mwezi baada ya gharama haifikii hata robo ya mshahara wangu, ni kinachouma hasa ukizingatia mtaji nliupata kwa mkopo lakini bado nakazana ivo ivo, changamoto kubwa ni kwamba mimi muda mwingi nipo kazini anabaki dada wa kazi
This is a great testimony ever! I think wakuu, mindsets zetu zibadirike, zama zimeshabadirika. Saizi ajira ni chache ukilinganisha na nambe ya wahitimu wanaomaliza kila mwaka. So, self-employment matters a lot.
 
Nachoamini ni kwamba mtu hujifunza mambo ambayo yanadumu kichwani pindi awapo chini ya miaka 18.

Ni mda huu wengi wanakazania watoo kushika namba moja shuleni, matuisheni hadi weekend, kuwapelekea watoto shule za boarding kwa fasheni, kupiga watoto wasipofanya vizuri darasani, n.k Hali hii inamfanya mtoto awe anajua elimu ya darasani tu, kimbembe kinaanza mtoto kamaliza chuo na lafaulu vizuri tu lakini ndio hivo tena kupata kazi sikuhizi ni ngumu sana.

Binafsi kwa sasa navyolea watoto wangu, moja yupo shule ya msingi ila namlea nikiwa na taswira kwamba akimaliza chuo atakosa ajira japo siombei iwe hivi ila ni kuangalia uhalisia, Najitahidi na ntajitahidi kadri niwezavyo awe na ujuzi katika mambo mbali mbali yatayomsaidia hata akikosa ajira,
Bora ufanye Ivo mkuu!!

Pia usisahau na kumpeleka kusoma course hot cake za kompyuta km graphic design n.k

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Huyu Jamaa aliyeleta uzi haelezei vizuri hii issue
Mtaji wa kuanzia saloon bro wako alipata wapi?
 
Mtaji alipata wapi boss?
Alianza nishingapi kwanza??
Huyu Jamaa aliyeleta uzi haelezei vizuri hii issue
Mtaji wa kuanzia saloon bro wako alipata wapi?
Mkuu biashara ya kinyozi sidhani kama mtaji wake ni wa kutisha kusema kwamba unazidi hata milioni.

Frem aliyokodi ya kawaida sana, alikuwa na ujuzi tayari wa kunyoa, viti, kioo, mashine niliona kama vimeshatumika huenda alinunua kwa mtu maana nae alikuwa anayajua haya mambo ya kinyozi kwa mda mrefu tangu sekondari.

Sijajua alipopata mtaji lakini ni mtaji wa kawaida tu maana ilikuwa saloon ya kawaida sana
 
Habari zenu wakuu,

Leo nmeona nitoe neno hapa, zama zimebadilika wadau, Kukazia elimu zamani ilikuwa ni kujiongezea uhakika wa kujitegemea ukiwa mkubwa kwa kuajiriwa serikalini au kwenye makampuni.

Na hata mimi binafsi kwenye familia yetu wazazi wetu walituasa sana tusome sambamba na adhabu kali na vipigo barabara pale tuliposhuka uwezo darasani.

Tupo wanne kwenye familia, wote tumemaliza vyuo, brother ana mssters, sista ana degree, mimi nina degree na cpa, mdogo wangu ana masters.

Ni mimi peke yangu ndie niliebahatika kupata ajira serikalini.

Hao wengine wamesota sana hizi ajira, nakumbuka kipindi flani braza na sista walimlipa kiongozi wa shirika flani ili tu wafanye kazi hapo kwa kujitolea ili waingeze experience na ikiyokea bahati basi waajiriwe lakini matokeo yake hata ajira zilipotangazwa nabinterviews kufanyika hawakuchaguliwa, inauma sana.

Baada ya kuona msmbo sio mambo na muda unaenda, braza akawa amechoka sana, braza akakodi frem akawa ni kinyozi, nakumbuka sekondari blaza alikuwa ni kinyozi wa shule yao huko boarding kwa hio ujuzi alikuwa nao, basi kutokana na umahiri wake na kuwa na wateja wengi aliozoeana nao kidogo blaza stress zikaanza kuisha, akajichanga akanunua hizi playstations michezo ya video akawa anachezesha mfuko ukazidi kutuna, biashara ikawa imenoga akajaribu kuweka costa barabarani zinazoenda wilaya nyingine.

Muda ukaenda akaongeza nyingine nae akanunua gari ya kutembelea, maisha yakaanza kuwa safi, saizi navyoongea hapa braza yupo vizuri angalau, ana miradi mingi tu lakini ile biashara ya kinyozi hajaifunga na ni lazima kila mwezi aende pale hata siku moja atshinda pale ananyoa wateja wanamshangaa, na kinachomsaidia ni kwamba ana elimu na anaongea kiingereza fresh tu kinachimsaidia. Kajenga nyumba, mke wake nae ana biashara yake ya duka kubwa tu la vipodozi, watoto wake wanasoma shule private.

Kwa upande wa sista aliolewa lakini hajakaa kizembe, tangu zamani sista alikuwa anapenda sana kupika, ndo kalenga biashara yake hapa alianzishaga kupika chakula home then anaenda kuuza kwenye frem yake, pesa akaingiza akafungua kamgahawa ka kizushi anapikia huko huko, bwana wake akamuongezea mtaji saizi ana restaurant na kama ni pesa anazichapa.

Kwa huyi mdogo wangu, mtoto wa mwisho, nae ajira ka apply sana japo ana mwaka moja tangu amalize chuo, anaendelea ku apply lakini tukamshika mkono asizubae wakati anaomba hizo ajira, kwa sasa yupo kwa braza ndie msaidizi wa blaza, na braza anampa mshahara wa laki 6 kila mwezi, tunategemea kumchangia mtaji aanze biashara yake akifikia miaka 26, Kwa sasa ana 24 tumeona bora ajifunze funze kwa braza biashara kwanza.

Kuhusu mimi kiukweli nimepata kuwa na wivu wa kimaendeleo, yani pesa anayoingiza kaka na dada kwa miradi yao, pamoja na huu mshahara wangu wa muhasibu mwenye degree + cpa serikalini bado siwezi kuwafikia kipato chao, hali hii ikanifungua akili na kuacha kuridhika na mshahara, mwaka juzi december nilifungua biashara ambayo nilipata changamoto sana hususani za kuibiwa ila nilisaidiwa sana kuzitatua kwa kutumia ushauri wa kaka na dada, Biashara yangu kwa sasa faida inayoingiza kwa mwezi baada ya gharama haifikii hata robo ya mshahara wangu, ni kinachouma hasa ukizingatia mtaji nliupata kwa mkopo lakini bado nakazana ivo ivo, changamoto kubwa ni kwamba mimi muda mwingi nipo kazini anabaki dada wa kazi
blessed
 
Tukiachana na fashion na kufuata mkumbo ushauri mzuri ni huu:

Kama hutaki kuwa daktari basi Ukishajua kusoma na kuandika, ukajua kujumlisha na kutoa nenda kaitafute elimu itakayokupatia fedha kwa sababu hata wenye elimu za juu kabisa wakishazipata hizo elimu watarudi chini kuitafuta elimu itakayowapatia fedha au wakaajiriwa na wewe.
 
Dah!

Waafrica sasa tumeanza kuamka! Hongera kwa kujiongeza chief!

Mi binafsi now Nina 34 yrs lakini bado nazurura, sina uhakika wa maisha na hii yote sababu sina ujuzi

Ujuzi ni muhimu Sana kwa maisha ya sasa

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Hivi kuchanganya perfume nao ni ujuzi eeh!!?

Kama ndiyo..tafuta wale wanaochanganya wakufundishe utafute kamtaji uanze kusaka pesa.. perfume za kupima zinalipa sana
 
Back
Top Bottom