Ushuhuda Toka Loliondo....Serikali Inaficha Nini Loliondo..Wakati Wanajua Hakuna Tiba?

Napenda kutoa ushuhuda wangu katika mjadala wa Loliondo ambao umekuwa ukivuma sana katika blog ya michuzi kwa siku za hivi karibuni. Nawapongeza vijana wetu wakina, Magidd Mjengwa, mashaka john na bwana Mwilima. Hawa vijana wameongea mengi sana ya maana, na ninaungana nao katika hili, kwani hakuna cha tiba wala cha nini kwa babu. Wale wote waliojifanya wamepona, ndo wale wanaokufa

Kwanza, mimi ni muhathirika wa ukimwi. Niliomba ruksa ya dharura ofisini, nikafungasha, na kuondoka kwenda kwa babu. Nilipata kikombe changu baada ya siku nne tu. Kwa sasa nadhani inachukua zaidi ya wiki au mbili kumfikia babu. Yalioyonikuta loliondo, naogopa hata kuadisia; tulilala nje kwa kipindi chote. Nilishudia watu waliokuja na dripu toka hospitalini. Kweri watu wamekata tamaa humu nchini. Baada ya kupata kikombe changu, nilirudi zangu DAR. Siku 12 zikapita nikawa situmii ARV’s , ghafla hali yangu ikawa mbaya sana ikabidi nikimbizwe hospitalini. Nilizirudia ARV zangu na sasa hali yangu imeimarika kiasi
Rafiki yangu, mwenye virusi vya ukimwi naye alienda kwa babu, karudi, na kuanza kutangaza kwamba kapona. Jana hali yake ikawa mbaya kweli, ikabidi tumpeleke hospitali ya amana. Ina maana wiki tatu aliamini amepona, kumbe ugonjwa ukawa unamtafuna zaidi. Nadiriki kusema wazi kwamba sidhani yupo hata mmoja aliyepona kwa babu. Kilichonishangaza zaidi ni hali niliyoikuta loliondo.

Nikiwa kwenye foleni, watu wanne wamefariki pale nikiwatizama, ila kuna mdada wa makamu alikata roho akisubiri muda wake wa kupata kikombe. Cha ajabu, ndugu zake badala ya kuurudisha mwili wake kwao Dodoma, walijifanya kuondoka naye na matokeo yake kumtupa njiani kama kilometa 20 toka hapo kwa babu. Watu wengi wametupwa njiani, hasa pale ndugu wanaposhindwa na cha kufanya. Ili kuiokoa jamii dhidi ya magonjwa ya mlipuko huko loliondo na watu kutupwa kama wanyama polini, serikali inabidi iingilie kati, kwani hali ya loliondo ni mbaya zaidi na viombo vya habari vinatufichia ukweli...jamani, kuna kitu loliondo, kuna kitu kinafichwa. aliyepima kabla ya, na kupata matokeo negative baada ya, ajitokeze. mimi sikuluka foleni, na nilikuwa na imani mpaka hali yangu inakuwa mbaya nilidhania nimepona ukimwi....
Mollel

Ahsante sana Mkuu kwa mchango wako huu muhimu sana. Mimi ni mmoja wa wale ambao nilikuwa nasubiri uhakika wa watu kupona magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, saratani n.k. toka kwa madaktari wao wanaowatibu. Nilitegemea Madaktari hao watufahamishe Watanzania kwamba Wagonjwa wao kadhaa wa ugonjwa sugu mmoja au mwingine waliofanikiwa kupata kikombe cha Babu baada va kuchukuliwa tena vipimo vyao vimeonyesha kwamba hawana tena (ma)ugonjwa huo, lakini mpaka sasa hivi sijasikia hata daktari mmoja aliyeweza kututhibitishia hili. Hapo kwenye nyekundu hata mimi nililiwazia hilo kwamba labda Watanzania wengi ni Wagonjwa (au wamekata tamaa) ndio maana kukawa na umati uliokithiri kule nyumbani kwa Babu. Ugua pole Mkuu na Mungu akubariki.
 
Stigma/unyanyapaa utakufanya useme uwongo ili usiendelee kutengwa na jamii.mtu alikuwa ni HIV infected halafu jamii ikamnyooshea vidole na kumsimanga, basi kwa vyovyote vile akitoka kwa babu lazima ajinadi kuwa amepona ili arudishe dignity yake kwa wanaomnyanyapaa.

So far hakuna tiba ya HIV na bado kuna safari ndefu ya kuipata.mungu asaidie ipatikane kinga otherwise leo atazuka babu kesho bibi mtondogoo mjukuu!
 
Eti imani, Ndio nini imani? wewe watu wanakufa unasema hawakuwa na imani! Watanzania tunazidi kujidhalilisha leo karne ya 21 bado tunafikra za enzi ya mawe? Eti hujapona co's hukuwa na imani sasa mtu alitokatoka vipi mpaka kwenda Loliondo na adhabu ya safari,Nauli ghali foleni siku 13 alafu mijitu inaongelea imani. mambo ya Kibwetere msitulete hapa kutetea Ubaradhuli na Ushirikina, jana Rafiki yangu kipenzi alikuwa Muathirika wamemzika kwao.Dodoma alikuwa ana hali nzuri akaacha kutumia ARVs toka arudi Lolys kwa Babu yenu tar 21 Jan 2011 wiki iliopita alinipigia simu dada yake akanipa nionge nae alikuwa anatia huruma alikuwa anaongea kwa tabu sanaa moja ya kauli zake za mwisho kwangu aliniusia kuwa Watu wasighilibike wakaendelea na Uasherati kwa kujipa Matumaini eti kuna KIKOMBE au BAKULI Hakuna kitu kama hicho namsikitikia na ananiuma sana rafiki yangu Bora angeendelea na Dozi ya ARVs Pole sana Wanafamilia yake R.I.P JAROME

Pole sana. Tusipokuwa makini watakufa wengi tu. Hata mimi mjomba wangu amekufa baada ya kupata kikombe ikabidi tuingie gharama za kuupeleka mwili wake nyumbani, Inasikitisha sana.
 
Eti imani, Ndio nini imani? wewe watu wanakufa unasema hawakuwa na imani! Watanzania tunazidi kujidhalilisha leo karne ya 21 bado tunafikra za enzi ya mawe? Eti hujapona co's hukuwa na imani sasa mtu alitokatoka vipi mpaka kwenda Loliondo na adhabu ya safari,Nauli ghali foleni siku 13 alafu mijitu inaongelea imani. mambo ya Kibwetere msitulete hapa kutetea Ubaradhuli na Ushirikina, jana Rafiki yangu kipenzi alikuwa Muathirika wamemzika kwao.Dodoma alikuwa ana hali nzuri akaacha kutumia ARVs toka arudi Lolys kwa Babu yenu tar 21 Jan 2011 wiki iliopita alinipigia simu dada yake akanipa nionge nae alikuwa anatia huruma alikuwa anaongea kwa tabu sanaa moja ya kauli zake za mwisho kwangu aliniusia kuwa Watu wasighilibike wakaendelea na Uasherati kwa kujipa Matumaini eti kuna KIKOMBE au BAKULI Hakuna kitu kama hicho namsikitikia na ananiuma sana rafiki yangu Bora angeendelea na Dozi ya ARVs Pole sana Wanafamilia yake R.I.P JAROME

Babu alichagua kutumia 'imani" kwa sababu hilo haliwezi kupingika kiurahisi kwani liko katika abstract sense, na siyo material. Kweli Watz tumefuzu kwa utapeli -- hasa katika utapeli huo sasa wanaingia ma-septuegeranians!
 
Ahsante sana Mkuu kwa mchango wako huu muhimu sana. Mimi ni mmoja wa wale ambao nilikuwa nasubiri uhakika wa watu kupona magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, saratani n.k. toka kwa madaktari wao wanaowatibu. Nilitegemea Madaktari hao watufahamishe Watanzania kwamba Wagonjwa wao kadhaa wa ugonjwa sugu mmoja au mwingine waliofanikiwa kupata kikombe cha Babu baada va kuchukuliwa tena vipimo vyao vimeonyesha kwamba hawana tena (ma)ugonjwa huo, lakini mpaka sasa hivi sijasikia hata daktari mmoja aliyeweza kututhibitishia hili. Hapo kwenye nyekundu hata mimi nililiwazia hilo kwamba labda Watanzania wengi ni Wagonjwa (au wamekata tamaa) ndio maana kukawa na umati uliokithiri kule nyumbani kwa Babu. Ugua pole Mkuu na Mungu akubariki.

Hilo ndilo linanifanya mimi kuona kwamba serikali hii ina lake jambo kuhusu utapeli huu. Kwa nini serikali haifanyi utafiti unaoeleweka ili kuwaridhisha wananchi wake iwapo tiba ya Babu inafaa au haifai? Badala yake inaachia tu wananchi kujirundika porini na kufa, kama siyo kwa wanyama wakali (kuna mama mmoja mwenye mimba aliraruriwa na chui akienda kujisaidia kichakani) basi ni kuhangaika katika kusubiri foleni, na kama siyo hapo, basi ni baada ya kupata kikombe kutokana na kufikiri mtu kapona na kuzitupa dawa zake za mahospitali?

Mbona serikali hii imekaa kijingajinga namna hii?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimempoteza staff mwezangu,tumemzika leo alikuwa kwenye ARV lakini aliacha kutokana na kunywa kikombe cha babu.so sad!
Huyu babu ni muuaji!!!serikali ichukue hatua isije ikatokea janga kama la kibwetere.
 
Naombeni kuuliza hivi kabla ya babu watu walikuwa hawafi??? :A S-key::A S-key::A S-key:
 
Hilo ndilo linanifanya mimi kuona kwamba serikali hii ina lake jambo kuhusu utapeli huu. Kwa nini serikali haifanyi utafiti unaoeleweka ili kuwaridhisha wananchi wake iwapo tiba ya Babu inafaa au haifai? Badala yake inaachia tu wananchi kujirundika porini na kufa, kama siyo kwa wanyama wakali (kuna mama mmoja mwenye mimba aliraruriwa na chui akienda kujisaidia kichakani) basi ni kuhangaika katika kusubiri foleni, na kama siyo hapo, basi ni baada ya kupata kikombe kutokana na kufikiri mtu kapona na kuzitupa dawa zake za mahospitali?

Mbona serikali hii imekaa kijingajinga namna hii?

Mkuu CP, unategemea nini kutoka kwenye Serikali iliyojaa wasanii. Wameweza kufanya utafiti wa kuhakikisha maji hayo hayana madhara kwa matumizi ya Binadamu lakini wakati huo huo wamekuwa kimya kuhusu utafiti kama kweli maji hayo yanaponya magonjwa sugu mbali mbali kama ambavyo inavyoaminiwa na Watanzania wengi.
 
Walikuwa wakifa, lakini si kwa uzembe wa kujitakia kama huu unaopatikana uko lolly!

Kwani wengi wanaoumwa ukimwi si wa kujitakia au Uzembe? Je, hao wanaotumia ARV hawafi? Serikali haiwezi kumpiga marufuku Babu, wagonjwa ndio wanaoweza kwa kutomfuata na tiba yake.
 
Pole sana, watu wamepona wengi tu. Ili wewe naona issue yako ni serious anza kuhesu siku

acha kukatisha tamaa watu.kwanza hata ukimwi wenyewe ni imani tu,haupo kinachosumbua ni umasikini alisema mbeki HAKUNA UKIWI.kama upo liyumba angeshakataa ugali kitambo,mnaokinbilia ARV itakula kwenu.
Kuhusu dawa ya babu huo ni mradi wa kanisa kama ilivokua DESI ni usanii kama ndodi alivostage manage leo star tv.kesho i mean leo asubuhi anatibu bure mgonjwa aje na kingilio cha kumuona doctor tu,dawa bure eti sababu kuna mtu kajitolea kumlipia matangazo yake tv.
Wachungaji nimewakubali kwa ubunifu wa kusaka ngawira
 
mimi hapa JF nimeishaonekana kituko kwa kupinga huu uponyaji. kuna mtu mpaka amefikia hatua ya kusema akipata mke kama MJ basi yeye atakuwa mtu wa kushinda na kukesha bar tu!

sasa taratibu ukweli unaanza kuonekana. msishangae watu wakianza kubadili ID na avatar zao hapa JF!
 
........Na mie ngoja nitoe ushuhuda wangu, mama yake na rafiki yangu alikuwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu, alikuwa anatumia dawa za hospital na zilikuwa zinamsaidia vizuri tu.

wiki 3 zilizopita alikwenda kwa babu kupata kikombe..... mwenyewe kwa imani alisema kapona.Hivyo kwa muda wa wiki 2 akaanza kutokuwa makini na dawa zake za kisukari na diet...........ijumaa kisukari chake kilipanda zaidi, wakamkimbiza hospital lakini kwa mapenzi ya Mungu hii jumamosi amefariki.
 
Nilisikia kwa babu wiki iliyopita hata saa mbili haikuchukua watu walienda na kugeuza sasa unasema wiki mbili bila uhakika why

Poleni wote wagonjwa wa hili na kile ila babu kasema IMANI sasa mtu ukiacha kutumia dawa ambazo sidhani kama alisema ukinywa kikombe changu acha dawa

Ok nataka kusema watu wanaachaje dawa bila ya kujiangalia? Sidhani kama mtu umepona maumivu ukaendelea chukua dawa panadol na kwenda kupima pia utakufa au sasa mtu unaachaje dawa na hujijui kama umeweka imani from muda ulikuwa unaondoka home kwako na kufikiria unaenda kwa babu???

Hata makanisani watu wanashauriwa waende kuchekiwa na unahimizwa kutoacha kuamini umepona na kuamini ni sio kutenda dhambi tena

Haya umesaliwa hata kusali na kumshukuru Mungu hufanyi, dhambi unaendelea kutenda wala humuogopi Mungu jamani shetani si atakurudia na kama ulipata ufunuo ukajisahau ndio unalo

Endeleeni kuwa na Mungu na imani msisahau imani

Wengi munaenda makanisani mnahubiriwa na fake prophet mbona hamlalamiki mbona mnafall kwa huongo wao bila kujijua mbona wengine mnaombewa kwa nguvu za giza hamsemi kitu??? Hamjijui eeh??

Sasa kama wewe humuamini babu basi wewe nani kukataza watu ni dhambi kama unakatisha tamaa watu sababu hukupona wewe
Acha kutaka watu wasiende kila mtu na bahati yake ndio maana vidole haviko naurefu sawa
Kama hao wa Michuzi mibaba haina kazi wajitoe picha tuwaone
 
IMANI

Mfano mwanamke anayevuja damu kwa miaka 12 alifikiri na kuamua kuwa akishika hata nguo ya Yesu atapona as kulikuwa na watu wengi na ikaja kupita baada ya kuishika tu

Ukiwa na imani usitie shaka na uwe umejisikia it is done,

Omba Mungu akupe moyo wa kuwa na imani
Biblia ina zaidi google mistari ya faith as kuna urahisi sana wa kusoma biblia online

Mungu alisema ukiwa na imani utaweza ambia mlima uhamie baharini na utahama

Ila ukijiachia jamani shetani mbaya so sali sali

Tubarikiwe
 
Kwani wengi wanaoumwa ukimwi si wa kujitakia au Uzembe? Je, hao wanaotumia ARV hawafi? Serikali haiwezi kumpiga marufuku Babu, wagonjwa ndio wanaoweza kwa kutomfuata na tiba yake.

vipi kuhusu kisukari na B.P.
 
Back
Top Bottom