Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
Napenda kutoa ushuhuda wangu katika mjadala wa Loliondo ambao umekuwa ukivuma sana katika blog ya michuzi kwa siku za hivi karibuni. Nawapongeza vijana wetu wakina, Magidd Mjengwa, mashaka john na bwana Mwilima. Hawa vijana wameongea mengi sana ya maana, na ninaungana nao katika hili, kwani hakuna cha tiba wala cha nini kwa babu. Wale wote waliojifanya wamepona, ndo wale wanaokufa
Kwanza, mimi ni muhathirika wa ukimwi. Niliomba ruksa ya dharura ofisini, nikafungasha, na kuondoka kwenda kwa babu. Nilipata kikombe changu baada ya siku nne tu. Kwa sasa nadhani inachukua zaidi ya wiki au mbili kumfikia babu. Yalioyonikuta loliondo, naogopa hata kuadisia; tulilala nje kwa kipindi chote. Nilishudia watu waliokuja na dripu toka hospitalini. Kweri watu wamekata tamaa humu nchini. Baada ya kupata kikombe changu, nilirudi zangu DAR. Siku 12 zikapita nikawa situmii ARV's , ghafla hali yangu ikawa mbaya sana ikabidi nikimbizwe hospitalini. Nilizirudia ARV zangu na sasa hali yangu imeimarika kiasi
Rafiki yangu, mwenye virusi vya ukimwi naye alienda kwa babu, karudi, na kuanza kutangaza kwamba kapona. Jana hali yake ikawa mbaya kweli, ikabidi tumpeleke hospitali ya amana. Ina maana wiki tatu aliamini amepona, kumbe ugonjwa ukawa unamtafuna zaidi. Nadiriki kusema wazi kwamba sidhani yupo hata mmoja aliyepona kwa babu. Kilichonishangaza zaidi ni hali niliyoikuta loliondo.
Nikiwa kwenye foleni, watu wanne wamefariki pale nikiwatizama, ila kuna mdada wa makamu alikata roho akisubiri muda wake wa kupata kikombe. Cha ajabu, ndugu zake badala ya kuurudisha mwili wake kwao Dodoma, walijifanya kuondoka naye na matokeo yake kumtupa njiani kama kilometa 20 toka hapo kwa babu. Watu wengi wametupwa njiani, hasa pale ndugu wanaposhindwa na cha kufanya. Ili kuiokoa jamii dhidi ya magonjwa ya mlipuko huko loliondo na watu kutupwa kama wanyama polini, serikali inabidi iingilie kati, kwani hali ya loliondo ni mbaya zaidi na viombo vya habari vinatufichia ukweli...jamani, kuna kitu loliondo, kuna kitu kinafichwa. aliyepima kabla ya, na kupata matokeo negative baada ya, ajitokeze. mimi sikuluka foleni, na nilikuwa na imani mpaka hali yangu inakuwa mbaya nilidhania nimepona ukimwi....
Mollel