USHUHUDA: Nilivyokutana na ushirikina kazini

Hall of famer

Member
Jan 12, 2021
45
142
Mambo vipi wakuu,

Kwanza nitajikita kwenye mada kutokana na personal experience ya hapa home Tz. Binafsi nimekulia mazingira ya dini sana , kwa hiyo mambo ya uchawi au ku-practice masuala ya kiganga /jadi sikuwahi.

Lakini kwa uzoefu na namna nilivyoona katika kutembea mikoa ya hapa Tanzania, hasa huko vijijini watu wamelazimika kutofanya Maendeleo, kuyahama makazi yao kwa kuogopa kulogwa. Unakuta eti Kijijini mtu alikuwa hawezi kujenga nyumba nzuri na kuezeka bati, ukifanya hiyo kitu unaanza kuandamwa na mambo mengine kama hayo.

Personal Experience.

Nilipoamua ku-resign kazi na kuanza mishe zangu binafsi, niliingia kwenye kazi za mining na huku ndio nilikutana na hayo mambo.

Tulienda kuanzisha mining site Handeni- Tanga. Aisee, nilikuwa nausikia tu ushirikina sasa kule ndio nilienda kuona. Yaani mtu analoga machine (Excavator) inakuwa haifanyi chochote, tunaita mafundi wa kila aina wanachokonoa wee ila waapi, na machine bado mpya.

Baadae one of the labors niliokuwa nao pale site akaniita na wenzake pembeni, wakaniambia ndugu yetu, hapa kutakuwa na kitu kimefanyika, wakanitaka twende na mganga ili tuka unlock. Mimi nikawa siamini kama mashine inaweza logwa na sikuwa na imani na zile mambo kbs.

Basi nikawauliza kama wanaweza kwenda wenyewe wafanye kwa niaba wakasema poa niwape elfu 20 wanunue kuku, basi mshikaji akanambia tuwape. Mini nikawapa wakaondoka bwana, hapo tumehangaika na fundi wiring na hydrologic system wote wanasema hawaona tatizo, ila machine haina kabisa nguvu ya kuchimba.

Wale wadau walirudi time za jioni around 5pm, na maji yenye dawa kwenye chupa pamoja na vimiti viwili. Wakasema Operator wa machine aweke mfukoni kimti kimoja na kingine aweke chini ya seat yake, na yale maji ya dawa imwagiwe machine na kuzunguka eneo la mgodi. Operator akasema fresh ,yeye alikuwa anaamini sana, wale jamaa wakamwaga maji kwny machine nakuzunguka pale site, na mwingine akaenda akaleta ka kuku kadogo akachimba shimbo pembezon mwa site akakafukia kale kakuku kakiwa kazima.

Baada ya hapo wakamwambia Operator awashe machine . Mi naangalia tuu km movie, aisee huezi amin machine ikawa na power kuzidi hata uwezo wake siku zote. Nikashangaa sana , jamaa wale wenyeji wanacheka wananiambia "karibu Tanga mgosi".

Hii ni kwa ufupi tu, nina mengi sana nime experience sehemu mbali mbali hasa katika kazi ya mining, maana mnaenda kuanzisha kazi sehem porini kumbe palikua ni mahali pa matambiko, basi vituko ni vingi nikijaaliwa muda nitakua naandika matukio mengine . Watu wana uwezo wakupoteza madini aridhini, yaani unachimba wee nakuunguza hela ila huoni kitu, wakati mwanzo mambo yalikua fresh kbs. Lakini mwisho wa siku nina Imani na Mungu , hatutakiwi kuweka Imani kwa waganga kwasababu nao ni binadam, uchawi upo na Mungu yupo.

Serikali haiamini katika uchawi, ni sawa kbs lakini ukweli ni kwamba uchawi umelostisha sana watu, pengine watu wangekuwa na maendeleo sehemu mbali mbali isingekuwa haya mambo. Siku hizi kidogo yanapungua ,nadhani muingiliano wa wageni na wenyeji sehemu mbalimbali unafanya watu ku-focus kwenye maendeleo. I'm not sure kama tumeshawah kuwa na sheria inayokemea haya mambo kwa kuwa ni invisible world.

Naomba niishie hapo kwa leo, najua wengi wetu tuna experience tofauti tofauti, kuwa huru ku share nasi tujifunze kitu.
 
Cha kushangaza akija mzungu, mchina au muarabu kuchimba kunakua hakuna vikwazo kama hivyo na wanafanikiwa kuchimba na kupata wanachokihitaji.

Pia ninashangaa Serikali haiamini uchawi ila anapokamatwa mchawi kaanguka uchi wanatia pingu na kumpeleka kituo cha polisi je kule anaenda kama mtuhumiwa wa nini au anaenda kuhukumiwa kwa kutokuvaa nguo yaani anatembea uchi.
 
"Na mwingine akaenda akaleta ka kuku kadogo akachimba shimbo pembezon mwa site akakafukia kale kakuku kakiwa kazima. Baada ya hapo wakamwambia Operator awashe machine. Mi naangalia tuu km movie, aisee huezi amini machine ikawa na power kuzidi hata uwezo wake siku zote"🤣🤣🤣
 
Kwani waarabu ,Wachina na wazungu hawana hizo mbanga MIGODINI?

Ungeishi nao ungekuwa na la kuhadithia hapa.🤣🤣
Cha kushangaza akija mzungu, mchina au muarabu kuchimba kunakua hakuna vikwazo kama hivyo na wanafanikiwa kuchimba na kupata wanachokihitaji

Pia ninashangaa Serikali haiamini uchawi ila anapokamatwa mchawi kaanguka uchi wanatia pingu na kumpeleka kituo cha polisi je kule anaenda kama mtuhumiwa wa nini au anaenda kuhukumiwa kwa kutokuvaa nguo yaani anatembea uchi.
 
Cha kushangaza akija mzungu, mchina au muarabu kuchimba kunakua hakuna vikwazo kama hivyo na wanafanikiwa kuchimba na kupata wanachokihitaji

Pia ninashangaa Serikali haiamini uchawi ila anapokamatwa mchawi kaanguka uchi wanatia pingu na kumpeleka kituo cha polisi je kule anaenda kama mtuhumiwa wa nini au anaenda kuhukumiwa kwa kutokuvaa nguo yaani anatembea uchi
Serikali haiamini uchawi ila kuna sheria ya kuzuia uchawi Tanzania.
 
Kwani waarabu ,Wachina na wazungu hawana hizo mbanga MIGODINI?

Ungeishi nao ungekuwa na la kuhadithia hapa....
Sidhani kwamba katika kazi zao kama hizi wanatumia uchawi, mara nyingi wanatumia elimu na vifaa bora ili kufanikisha malengo yao, naamini uchawi au ushirikina wanao ila sidhani kama wanatumia ktk mambo kama ya sayansi, Mm naishi nao huku
 
🤣🤣Ni kweli jamaa wanatumia vyote kwa ubora mkuu....
Kikubwa wako SYSTEMATIC na USIRI katika "mbanga" zisizoonekana huko migodini...
 
Cha kushangaza akija mzungu, mchina au muarabu kuchimba kunakua hakuna vikwazo kama hivyo na wanafanikiwa kuchimba na kupata wanachokihitaji

Pia ninashangaa Serikali haiamini uchawi ila anapokamatwa mchawi kaanguka uchi wanatia pingu na kumpeleka kituo cha polisi je kule anaenda kama mtuhumiwa wa nini au anaenda kuhukumiwa kwa kutokuvaa nguo yaani anatembea uchi
Yaan mkuu, hao wazungu na wachina wanafanya sn ushirikina kwenye sites kuliko unavyofikiri. Kuna mchina nilimshuhudia anachinja Mbuzi mwenyewe na dam ya mbuzi anaimwaga eneo la kazi huku anaongea kikwao. We waulize washkaji walofanya kaz na Chinese kwenye kandarasi mbalimbali watakwambia.
 
Hao jamaa wanaongoza....
Hao jamaa ni balaa zaidi....
Hao jamaa MUNGU wao ni PESA...hufanya lolote lile....
 
Sidhani kwamba katika kazi zao kama hizi wanatumia uchawi, mara nyingi wanatumia elimu na vifaa bora ili kufanikisha malengo yao, naamini uchawi au ushirikina wanao ila sidhani kama wanatumia ktk mambo kama ya sayansi, Mm naishi nao huku
Dah,! Mkuu huwajui vizuri hao ngozi nyeupe, hasa wa Hindi na wa China hao nd'o washirikina balaa Mimi nimefanya nao kazi mwaka wa kumi huu sio watu poa kabisa hakuna kazi wanafanya bila kafara pamoja na utaalam wao na mitambo yao yote.
 
Back
Top Bottom