COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,598
- 3,644
This is a true story:
Mimi ninasomeja mtoto wa Marehemu kaka yangu, binti huyo sasa yupo form three (shule siitaji). Huyu binti yetu alipewa ujauzito akiwa darasa la saba mwishoni.
Matokeo yalipotoka alikuwa amefauru kwenda sekondari ya serikali, hivyo alishindwa kwenda kujiunga na masomo maana mimba ilikuwa kubwa.
Alipojifungua, wazazi wake walijaribu kufuatilia ile nafasi kwa Mkuu wa Shule, lakini Mkuu wa shule alikataa kuwa haitawezekana huyo binti kujiunga na sekondari kwani Report zilishafika kuwa huyo binti ni Mjamzito na sasa amezaa. Kipindi hicho mimi nilikuwa bado sijamaliza masomo yangu ya chuo kikuu.
Kutokana na hali ngumu za kimaisha za wazazi wake (marehemu kaka yangu) binti alisukumiwa kwa mwanaume aliyemtia mimba.
Mimi baada ya kumaliza Chuo Kikuu (After 2YEARS) na kupata ajira serikalini, nilirudi home, nikaenda kwa ndugu wa huyo kijana anayeishi na binti yetu, nikaitisha kikao kwa Mwenyekiti wa mtaa.
Nilipiga mkwara wa kufa mtu, nikamnyanyua binti yetu, tukawakabidhi mjukuu wao, mimi nikaondoka na binti yetu (Mtoto wa marehemu kaka).
Nilimpeleka private school, akafanya mtihani wa kuingia form one, akapata marks za kumuingiza kidato cha kwanza kwenye hiyo Private school.
Kwa sasa binti hushika namba 5-6 Kati ya wanafunzi 150 darasi mwao.
Hivyo Rais huko kwenye shule zako wewe zuia tu, sisi watoto tutahangaika nao PRIVATE SCHOOL na watapata haki yao ya kitaaluma na mwisho watakuja kuwa viongozi wa nchi hii.
Nawasilisha.