USHUHUDA: Nilinyang'anya binti aliezalishwa kwa mwanaume na sasa she is among the best students

Kiufupi raisi anamaanisha kuwa binti akipata mimba nisawa na kuwa amedisco....chuo anaweza omba mwaka mwingine chuo kingine ila si cha serikali ambako yeye analipa 100% school fees plus other costs
 
This is a true story:
Mimi ninasomeja mtoto wa Marehemu kaka yangu, binti huyo sasa yupo form three (shule siitaji). Huyu binti yetu alipewa ujauzito akiwa darasa la saba mwishoni.

Matokeo yalipotoka alikuwa amefauru kwenda sekondari ya serikali, hivyo alishindwa kwenda kujiunga na masomo maana mimba ilikuwa kubwa.

Alipojifungua, wazazi wake walijaribu kufuatilia ile nafasi kwa Mkuu wa Shule, lakini Mkuu wa shule alikataa kuwa haitawezekana huyo binti kujiunga na sekondari kwani Report zilishafika kuwa huyo binti ni Mjamzito na sasa amezaa. Kipindi hicho mimi nilikuwa bado sijamaliza masomo yangu ya chuo kikuu.

Kutokana na hali ngumu za kimaisha za wazazi wake (marehemu kaka yangu) binti alisukumiwa kwa mwanaume aliyemtia mimba.

Mimi baada ya kumaliza Chuo Kikuu (After 2YEARS) na kupata ajira serikalini, nilirudi home, nikaenda kwa ndugu wa huyo kijana anayeishi na binti yetu, nikaitisha kikao kwa Mwenyekiti wa mtaa.

Nilipiga mkwara wa kufa mtu, nikamnyanyua binti yetu, tukawakabidhi mjukuu wao, mimi nikaondoka na binti yetu (Mtoto wa marehemu kaka).

Nilimpeleka private school, akafanya mtihani wa kuingia form one, akapata marks za kumuingiza kidato cha kwanza kwenye hiyo Private school.

Kwa sasa binti hushika namba 5-6 Kati ya wanafunzi 150 darasi mwao.
Hivyo Rais huko kwenye shule zako wewe zuia tu, sisi watoto tutahangaika nao PRIVATE SCHOOL na watapata haki yao ya kitaaluma na mwisho watakuja kuwa viongozi wa nchi hii.

Nawasilisha.

Nina ushahidi wa Binti aliyepata Mimba form one leo ana Masters ya Economics na muajiriwa na alupasua form four alipata Div.1 na form six Div.

Kupata mimba siyo kosa,watoto kuzaa mtoto na kumuacha kwenye mazingira ya umasikini na ufukara ndiyo dhambi.
 
Sishangai binti wa sekondari kupata mimba. Panya mwenye umri wa miezi tisa anakuwa ameshazaa watoto wa kutosha, ng'ombe mwenye umri wa miaka minne anakuwa ameshazaa watoto wa kutosha, sembuse binadamu mwenye umri wa miaka 14?
Njia bora zaidi ya kuwakinga watoto wetu wa kike ni kuwapeleka shule za bweni. By the time wanakuja kubumbuluka wanakuwa wamemaliza form six, sasa huko hata wakipata mimba watajijua wenyewe... Au basi kuwe na agizo la hao mabinti waliokwisha anza ngono zembe kupewa vidonge vya uzazi ili wasishhike mimba, kinyume na hapo, hawa mabinti wataendelea tu kuzalishwa...
 
Kiufupi raisi anamaanisha kuwa binti akipata mimba nisawa na kuwa amedisco....chuo anaweza omba mwaka mwingine chuo kingine ila si cha serikali ambako yeye analipa 100% school fees plus other costs
Anatoa fedha zake mfukoni kulipia hizo gharama? Mkumbushe kuwa hizo ni KODI ZETU tunazo lipa siyo mshahara wake unaotumika, sawa?!
 
sijawahi ona commander in chief mjinga kiasi hiki...what if kama mtoto alibakwa and wasn't her fault? je haki yake ndo imepotea hivyo? ama kweli..kuzeeka haimanishi kuwa na busara!
 
Ukicheka na nyani utavuna mabua. Endelea vivyo hivyo.

I am with my, President Dr. Magufuli for this decision.

Mnafiki kama wewe lugha ya kejeli kama hii angeisema Lissu leo mngekesha hapa kulaani kwamba hana utu na cdm ni chama kisichojali elimu kwa upande wa watoto wa kike.
 
Ndio maana mmeambiwa fungueni shule zenu muwapeleke kusoma hao wazazi lakini sio shule za serikali umeelewa.

Kwa taarifa yako kumpeleka mtoto wako shule ya serekali ni kutokana na hela kupiga chenga, kinyume na hapo kumpeleka mtoto wako shule ya serekali ni kwenda kushusha uwezo wake wa kielimu. Kama huamini angalia kama kuna kiongozi yoyote wa serekali mwenye kipato kinachozidi milioni moja kwa mwezi kama anapeleka m/watoto wake kwenye hizo shule za umma. Wewe imbishwa wimbo wa uzalendo wenzako wanakwenda sokoni kununua matikiti kwa kutumia VX la umma.
 
Ukicheka na nyani utavuna mabua. Endelea vivyo hivyo.

I am with my, President Dr. Magufuli for this decision.
With your grammer..sina uhakika kama hata shule unayotaka wenzio wesienda wewe ulienda..!
 
Vitabu vya dini vinasemaje juu ya hilo?? Ndani ya ndoa linaitwa TENDO LA NDOA ,nje ya hapo ni Zinahaa
 
Back
Top Bottom