USHUHUDA: Nilinyang'anya binti aliezalishwa kwa mwanaume na sasa she is among the best students

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,526
2,000
This is a true story:
Mimi ninasomeja mtoto wa Marehemu kaka yangu, binti huyo sasa yupo form three (shule siitaji). Huyu binti yetu alipewa ujauzito akiwa darasa la saba mwishoni.

Matokeo yalipotoka alikuwa amefauru kwenda sekondari ya serikali, hivyo alishindwa kwenda kujiunga na masomo maana mimba ilikuwa kubwa.

Alipojifungua, wazazi wake walijaribu kufuatilia ile nafasi kwa Mkuu wa Shule, lakini Mkuu wa shule alikataa kuwa haitawezekana huyo binti kujiunga na sekondari kwani Report zilishafika kuwa huyo binti ni Mjamzito na sasa amezaa. Kipindi hicho mimi nilikuwa bado sijamaliza masomo yangu ya chuo kikuu.

Kutokana na hali ngumu za kimaisha za wazazi wake (marehemu kaka yangu) binti alisukumiwa kwa mwanaume aliyemtia mimba.

Mimi baada ya kumaliza Chuo Kikuu (After 2YEARS) na kupata ajira serikalini, nilirudi home, nikaenda kwa ndugu wa huyo kijana anayeishi na binti yetu, nikaitisha kikao kwa Mwenyekiti wa mtaa.

Nilipiga mkwara wa kufa mtu, nikamnyanyua binti yetu, tukawakabidhi mjukuu wao, mimi nikaondoka na binti yetu (Mtoto wa marehemu kaka).

Nilimpeleka private school, akafanya mtihani wa kuingia form one, akapata marks za kumuingiza kidato cha kwanza kwenye hiyo Private school.

Kwa sasa binti hushika namba 5-6 Kati ya wanafunzi 150 darasi mwao.
Hivyo Rais huko kwenye shule zako wewe zuia tu, sisi watoto tutahangaika nao PRIVATE SCHOOL na watapata haki yao ya kitaaluma na mwisho watakuja kuwa viongozi wa nchi hii.

Nawasilisha.
 

Mhakiki

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
1,901
2,000
Niliwahi sikia moja ya mawaziri alipata mimba.Angeachishwa shule leo asingetutumikia watanzania.Tuwaache wasome kwani sote tu wazazi wa wahanga niliwahi sikia moja ya mawaziri alipata mimba.Angeachishwa shule leo asingetutumikia watanzania.Tuwaache wasome kwani sote tu wazazi wa wahanga hawa.
 

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,189
2,000
Ameongea kwa mihemko tu watu wanakufa hukko kibiti unakuja na stor za mimba
Eti huwez kusomesha wazazi, huez kutatua tatizo.hilo kwa vitisho
 

Jabman

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,010
2,000
Rais amesema ukweli japo unauma. Ukiruhusu wazazi waendelee na masomo,shule za Kata wote watazaa bado form two.

Angeongezea kuwa, anayebeba mimba akajifungulie gerezani.
Tuache uoga tulee watoto wetu kwa maadili mema. Dini zote haziruhusu upuuzi huu.

Ikitokea bahati mbaya basi tufanye kama mleta maada.
 

Siyabonga101

JF-Expert Member
Mar 8, 2016
2,426
2,000
Na ndio Mh. Rais alichokieleza; muwapeleke PRIVATE SCHOOLS au muwajengee shule hizo ili wasije kuwaharibu watoto wengine huku kwenye shule za Serikali. Nashangaa kuna watu wazima na akili zao timamu wanaunga mkono mabinti wanaopata mimba shuleni kurudishwa kuendelea na masomo baada ya kujifungua!!! Mnajua madhara ya hili suala zima!? Au mnaongea kwa kuwa kauli imetolewa na mbaya wenu (Wezi na wahujumu)!!???
 

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,597
2,000
Kweli wakasaidiane na kasela kake jela. Nimekupa like mubashara kabisa

Rais amesema ukweli japo unauma. Ukiruhusu wazazi waendelee na masomo,shule za Kata wote watazaa bado form two.

Angeongezea kuwa, anayebeba mimba akajifungulie gerezani.
Tuache uoga tulee watoto wetu kwa maadili mema. Dini zote haziruhusu upuuzi huu.

Ikitokea bahati mbaya basi tufanye kama mleta maada.

Kweli wakasadiane na kisela chake huko jela
 

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,189
2,000
Hatusemi kuwa akipata mimba hawezi kufaulu, no....Anaweza kufaulu vizuri tu.....

So endeleeni kuwasomesha shule zenu, na jengeni shule zaidi za kuwasomesha hao wakina mama.....Kwa serikalini ni HAPANA..Fullstop
Ni sawa tu kwanza huko shule za serikal kuna nini mnachofanya, hivi mnaweza mkasimamisha vichwa na kusema mna shule za serikal za kujivunia ? Shule nying bado watoto wanakaa kwenye mawe na madarasa ni vijumba vya nyasi na choo ni kimoja wanashea walimu a wanafunzi, shule nyingine ni mwalimu mmoja ndo anafundisha
 

lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,088
2,000
Wewe siyo wa kwanza au wa mwisho kusomesha mtoto mzazi. Wengi tu wanasoma na wataendelea kusoma.
Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza maadili, shule za watoto siyo kwa ajili ya wazazi.
Hakuna kipingamizi kwa msichana aliyepata mimba kuendelea na elimu kwa utaratibu wake, lakini siyo kurudishwa alikokuwa kabla.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom