Ushuhuda namna Polisi Central wanavyopiga Pesa bila kutoa risiti

Daah pole Sana braza , huo ni uonevu wa dhahiri & shahiri
SEHEMU YA KWANZA.

Mimi nafanya shughuli zangu city centre.. Natumia usafiri wa pikipiki kuendesha shughuli zangu mjini ili kufika sehemu kwa wakati.

Kuna order iliwahi kutolewa na mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda kutoingia mjini bila kibali. Ili kutii agizo hilo huwa nakata kibali kila baada ya miezi 6 ili niweze kuendelea na shughuli zangu bila bughudha.

Picha linaanza mwezi september kwa kukamatwa nikiwa nimesimama kwenye mataa ya mnazi mmoja nikisubiri taa ziruhusu magari ,mara paap nadandiwa na mtu aliyevalia kiraia na kuchomoa ufunguo ghfla. Namuuliza kulikoni? Najibiwa leta pikipiki pembeni. Baada ya kusogea pembeni naambia achia pikipiki nauliza kwa nini? Naulizwa una bei gani nikuachie?

Duuu nikajua tapeli huyu,nikamjibu nikupe pesa kwa kosa gani? Nikaambiwa sina Leseni, nikaonesha leseni. Baada ya dakika kadhaa za mabishano anaingia mwingine ananiamuru niachie pikipiki, tukaanza kuvutana wakanizidi nguvu. Pikipiki ikachukuliwa nikaambiwa nikae nyuma. Kweli, kumbe ni askari akanipeleka hadi central , kufika tu yule aliyenikamata akasema "afandeeee huyu kosa lake mwendo kasiiii" shabashiiiii nataka kuongea nikambiwa kaa kimya unajifanya jeuri, kaa chini nyosha miguuu, duuuu nikatii sheria bila shuruti. Walikuepowengine wengiwaliokaa chini wanachukuliwa maelezo.

Baada ya muda zamu yangu ikafika nikaanza kuhojiwa. Nikaulizwa kosa nikasema sina kosa. Askari akaniambia usinipotezee muda mimi sijakukamata. Akaniambia chagua kosa niandike Mwendokasi au wrong parking, duuuh nimebisha pale mwisho a picha nikaandikiwa Wrong parking.

Baadae tukapekuliwatuakawekwa ndani wote. Tulikuwa kama 20. Tukiwa ndani tukawa tunabadilishana mawazo na madereva wenzangu. Wengi ni Bodaboda. Nikaambiwa hapa kesho asubuhi unatakiwa uandae wadhamini 2waje na barua za serikali za mitaa. Kweli kesho yake akaanza kutoka mmoja baada ya mwingine. Zamu yangu ilipofika nilidhaminiwa na mtu mmoja. Nikaachiwa kama saa 6 mchana. Nikaambiwa kesho saa 4(siku iliyofuata) nije na LESENI, KADI YA PIKIPIKI, BIMA, SUMATRANA RISITI.

Kesho nikaenda navyo vyote. Tumekaa pale asubuhi hadi mchana hakuna kinachoendelea ila naona wenzangu(wazoefu wa kukamatwa mjini) wanachukua pikipiki wanaondoka. Ikabidi na mimi nijiongeze nikamuuliza aliyetoka na pikipiki,utaratibu wa pikipiki ukoje?mbona nimeshakaguliwa lakini sioni nikiachiwa? Akaniambia Bro hapa huwa hawataki maneno wanataka pesa au uende mahakamani ukajitetee? Duuhh kusikia mahakamani nikapagawa.

Nikamuuliza wanataka kiasi gani? Nikaambiwa laki na nusu (150,000/=). Baada ya kukaa muda ikabidi na mimi niende ofisini pale kwa Afande Beka kwenye ofisi ya karibu na mwembe ili nilipe 150,000/=. sikkufanikiwa kumuona afande Beka. Nikapewa namba nimpigie askari anisaidie kuitoa pikipiki. Akaniambia bila laki na nusu pikipiki huitoi, nikamwambia laki na nusu ninayo. Akaniambia nisubiri baada ya nusu saa kwa sababu yupo mbali.

Baada ya nusu saa akanipigia simu nipeleke pesa. Nikaenda nikampa keshi 150000. Nikapelekwa kwa Afande Beka nikaaandikiwa kimemo, pikipiki nikapewa. SIUKUPEWA RISITI. NILIPOULIZA RISITI NIKAULIZWA KWANI PIKIPIKI YAKO HUJAPATA? NIKAISHIWA POZI IKABIDI NIWE MPOLE.

SEHEMU YA PILI.

Mwezi November. Picha linaanzia mataa ya kamata. Nikiwa nimesimama ktk mataa mara paap funguo zimechomlewa. Kama kawaida. Tukaenda kuwekwa kwenye karandinga karibu na roundabaout ya kuelekea sentro na mbagala. Ilipofika jioni aliletwa jamaa mmoja anashushiwa kipigo cha hatari. Alishushia sitiki za kufamtu. Kumbe yule jamaaalikua mwanajeshi ila yeye alikuwa abiria alivyoona wamerukia ufungua wa bodaboda aliyekuwa amemubeba alihisi kutaka kusababishiwa ajari, ikabidi awape adabu kidogo asikari duuh baada ya hapo walikusanyika kama wote walimshushia kipigo cha mbwa mwizi pamoja na kuwaonesha kitambulisho kama afisa wa jeshi hawakumuelewa, walimpa kipigo hadi akawa anatoa chozi kwa uchungu. Siku hiyo kama kawaida tukapelekwa central, usiku huo zilipigwa simu nyingi sana zikilenga kusaidia huyo mjeshi bila mafanikio. Siku hiyo tulikaa pale tukachuliwa maelezo hadi usiku wa saa 6. Baadae tulipelekwa mahabusu wote ,tukapekuliwa tukaingizwa chini lakini yule mjeshi alibaki kaunta tulikuja ambiwa kesho yake kuwa aliachiwa.

Kama kawaida utaratibu wa kutoka ulikuwa uleule. Nililipa 150,000/=BILA RISITI, BILA KUANDIKIWA MAKOSA MATANO ILI IENDANE NA PESA ILIYOLIPWA YA MAKOSA 5, ILA SIKU HIYO NILIANDIKIWA KOSA LA KUPITA MWENDO KASI WAKATI NIMEKAMATIWA MATAA YA KAMATA NIKIWA NATOKA POSTA.

SEHEMU YA TATU.

Baada ya pale baadhi ya madereva bodaboda walivyoona nakamatwa kizembe walinishauri nisiwe nasimama kwenye mataa. Wao huwa hawasimami kwe mataa kwa kuogopa kudandiwa na askari bila sababu za msingi. Nikaona hii imekaa poa sana. Na mimi sasa nikawa siheshimu mataa, nikiona upenyo tu napenya. Laikini hili halijanisaidia kwa sababu sasa hivi hawa askari wamejaa kila mtaa. Naambiwa wanatumia shirikishi na baadhi ya madereva bodaboda kukamata wenzao. Unaweza ukawa unatembea mara ghafla inabinywa clutch. Kwa style hii ya hovyo nimekamatwa mara 2 na mara zote hizi nilianguka chini kwa sababu ya kung'ang'aniwa clutch.

Kuna mbinu nyingine wanakublock na bajaji au na pikipiki kiasi kwamba wanaweza kukusababishia ajari. Hii mbinu nadhani imeanza baada ya kuona hatusimami tena kwenye mataa.

Picha linaanzia february. Nimekamatwa mara 5 toka february hadi jana. Kama kawaida mkamataji anaweza kukuliza kwanza una bei gani, mkimalizana anakuachia. Mara nyingi ukiwa na elfu 50, 30, 20 ya papo kwa papo unaachiwa. Kama huna pesa ya papo kwa papo ndo unafikishwa kwa pilato. Kwa afande Beka.

Angalau sasa hivi wamepunguza bei. Pale sasa hivi unaambiwa lipia makosa mawili yaani 60,000/=. Bila hiyo pesa huachiwi na chombo kinabaki polisi. NAWAONEA HURUMA BODABODA WANAOCHUKULIWA PESA ZAO BILA HURUMA KUWA WENGINE WANAENDESHA FAMILIA ZAO KWA KAZI YA BODABODA. Bodaboda na waendesha pikipiki wengine hapo mjini huo ndo mtindo wa kisasa. HII ADHA MADEREVA PIKIPIKI TUNAIPATA KWA SABABU YA TAMKO LA MH MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA.Unaweza kuwa na Kila kitu lakini ukifika pale unapigwa biti na maasikari pale utadhani umeua. Hupewi pikipiki ukaendelee na shughuli bila kulipia faini. Husikilizwi hata kidogo. Hii ni tofauti na gari unaandikiwa bill hata kama huna pesa kwa wakati huo unalipia baadae. HII HALI YA VITISHO, KUWEKWA NDANI , NA KULAZIMISHWA KULIPIA FAINI YA PAPO KWA PAPO NDO INAONGEZA RUSHWA NA HATUPEWI RISITI. PESA ZOTE ZINAISHIA PALE KWA AFANDE BAKARI BADALA YA KULIPA KWA CONTROL NAMBA AU KWA MHASIBU.

BODABODA NA MADEREVA WENGINE WA PIKIPIKI HASA WA DAR-ES-SALAAM NAO WANA FAMILIA. HUU UONEVU WA KUPIGWA FAINI KUBWAKUBWA UNAWAONGEZEA STRESS ZA MAISHA. MUDA UTAONGEA.
 
Of course kangi alijitahidi sana
Enzi za Kangi kila mwendesha pikipiki alipumua. Angalau hata ukikamatwa uliandikiwa kosa moja japokuwa napo risiti hatukupewa. kuna jamaa kanieleza huu ni mradi wa wakubwa wa kupiga pesa.
 
Hiyo itakuwa kweli maana rushwa inachukuliwa ofisini hii kitu itakuwa inajulikana
 
Ndyo maana pikipiki za mjini dar wapo kama kichiro yan hawaatuliii ni kuhaha kila sasa. Unapanda boda unaambiwa pesa ya chenji ipo. Ukisema upo ukifikishwa yan unatoa pesa na kuruka fasta then anachora asikamatwe.

Ushaur wangu kwanza bodaboda mnatakiwa mshikamane kwa hili. Unganeni tafteni nini cha kufanya. Hata mkikubaliana kuwa mnashirikiana endapo utaona mtu bila sare za jeshi la police akikukamata mnampa kipondo. Maaan hii ni hatari et mtu hana hata sare frm no where anakuja kukukamata...kama jambazi je?

Achani ujinga.

Alafu kwanini mnapoambiwa kuwa mtapelekwa mahakamani mnaogopa. Mimi ni dreva nimekutana na mkasa kibao ya hawa jamaa. Tunafikishanaga central sana. Na huwa wanajikuta wananiacha bila kuwapa hata mia. Mahakaman kinachotakiwa huwa ni ushahidi huwezi kudraw kesi bila ushahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefuatilia Uzi huu tangu Jana na nimevutiwa na maelezo ya mtoa hoja na wengine kadhaa waliotoa shuhuda zao.
Suala hili limekuwa likielezwa Mara kwa Mara lakini kama ilivyo ada nchi hii, hili ni Mali ya watawala.
Kwa maelezo haya kama ingekuwa amesemwaheshimiwa sana, hatua zingechukuliwa na pengine tungejulishwa kuwa Fulani anashikiliwa kwa tuhuma kadhaa.
Mara nyingi katika zama hizi polisi wameondokana na ile dhana yao ya awali kuwa hawafanyii kazi mambo ya mitandao kwan hats wao wanachokitengo kinachoshughulikia masuala haya.
Imekuwaje hadi sasa, hakuna taarifa inyotolewa juu ya tuhuma za akina beka ambao bila shaka hapo " sentro" huyo ni kigogo wa kubambika kesi tena za ajabu kuwa pikipiki imekutwa wrong parking.
Tunahitaji kusikia hatua zikichukuliwa hata zile za kuzuga kuwa uchunguzi unaendelea..

Nimewasoma watu wakidai kuwa taarifa itolewe takukuru. Lakini hawa jamaa wao huko ofisini huwa wanafanya nini? Au ndo kusubiri mpaka waagizwe kuchunguza fedha za vyama vya ushirika?
 
Viongozi wenye dhamana, haya malalamiko na mengine mengi ndiyo yalisababisha watu kuchangia dhamana ya uongozi wa Chadema utoke Jela.

Huu ni ufa mkiuacha mtakuja kulala nje ukuta utakua umeshaanguka chini.
 
Kuna siku nilikuwa nawahi zangu bandarini asubuhi na usafiri ulikuwa wa tabu sana, kipindi hicho naishi zangu Temeke, hivyo nikaona nimchukue bodaboda nikamtia 5000 ili aniwahishe kufika Mivinjeni hao jamaa wako pembeni na kumsimamisha dereva bodaboda wangu, ile sijashuka kuna jamaa kavaa kiraia nae akaja kwenye pikipiki ili achomoe funguo, pale pale nami nikapeleka mkono wangu kwa kasi na kumbinya vidole vyake (Mwili wangu upo kimazoezi/hivyo nipo fiti). Nikamuuliza yule jamaa huku nambinya "kwanini unachomoa funguo na wewe ni nani" jamaa hakuwa na jibu zaidi ya maumivu na kumwita askari mmoja mwenye nyota mbili, alimwita kwa jina la inspekta. Hapo hapo nami nikapata pa kuanzia ile huyo inspekta kufika tu, nikamwambia "hivi ndivyo mnavyowafanyia watu. Basi yule inspekta alionesha kubabaika kidogo na kuniambia "tunawafanyia hivi kwasababu wengine huwa wanakimbia. Nikamuuliza sasa kosa lake ni lipi hadi mumchomolee funguo. Akaniambia wanafanya hivyo ili asikimbie. Nikamwambia tukae pembeni ili nijue wanataka kumfanya nini. Basi pale yule Inspekta akaonda huku akimwita sajenti mmoja hivi ili aje am attend yule boda boda. Nikawa niko pembeni nawasikilizia huku nikatoa simu yangu na kumpigia jamaa ambae ni askari na kumwomba namba ya RTO huku nikiongea kwa sauti. Kumbe yule inspekta ananisikilizia. yule jamaa kwenye simu akanijibu hana namba ya RTO ila nika act kumwambia kwa sauti "sawa nampigia sasa huyo RTO" ILE KUKATA SIMU TU akaja yule inspekta na kutwambia tuondoke.

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
 
Kwa taarifa tu Mkuu, hili tamko lilikuja kuwadhibiti bodaboda waliounga mkono ukawa 2015 Mara tu baada ya uchaguzi. Walikuwa wanakula ccm wanalala ukawa. Ndo maana unaona unaona Magu hajawahi kuwazungumzia bodaboda tangu aingie ikulu. Anaamini bodaboda walihatarisha kiti chake. Bodaboda sio wajinga.
Magu itabidi awatumie tu bodaboda maana kwenye Kampeni wapo vizuri kwenye amsha amsha msururu wa Bodaboda Mia Moja lazima uvutie watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEHEMU YA KWANZA.

Mimi nafanya shughuli zangu city centre.. Natumia usafiri wa pikipiki kuendesha shughuli zangu mjini ili kufika sehemu kwa wakati.

Kuna order iliwahi kutolewa na mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda kutoingia mjini bila kibali. Ili kutii agizo hilo huwa nakata kibali kila baada ya miezi 6 ili niweze kuendelea na shughuli zangu bila bughudha.

Picha linaanza mwezi september kwa kukamatwa nikiwa nimesimama kwenye mataa ya mnazi mmoja nikisubiri taa ziruhusu magari ,mara paap nadandiwa na mtu aliyevalia kiraia na kuchomoa ufunguo ghfla. Namuuliza kulikoni? Najibiwa leta pikipiki pembeni. Baada ya kusogea pembeni naambia achia pikipiki nauliza kwa nini? Naulizwa una bei gani nikuachie?

Duuu nikajua tapeli huyu,nikamjibu nikupe pesa kwa kosa gani? Nikaambiwa sina Leseni, nikaonesha leseni. Baada ya dakika kadhaa za mabishano anaingia mwingine ananiamuru niachie pikipiki, tukaanza kuvutana wakanizidi nguvu. Pikipiki ikachukuliwa nikaambiwa nikae nyuma. Kweli, kumbe ni askari akanipeleka hadi central , kufika tu yule aliyenikamata akasema "afandeeee huyu kosa lake mwendo kasiiii" shabashiiiii nataka kuongea nikambiwa kaa kimya unajifanya jeuri, kaa chini nyosha miguuu, duuuu nikatii sheria bila shuruti. Walikuepowengine wengiwaliokaa chini wanachukuliwa maelezo.

Baada ya muda zamu yangu ikafika nikaanza kuhojiwa. Nikaulizwa kosa nikasema sina kosa. Askari akaniambia usinipotezee muda mimi sijakukamata. Akaniambia chagua kosa niandike Mwendokasi au wrong parking, duuuh nimebisha pale mwisho a picha nikaandikiwa Wrong parking.

Baadae tukapekuliwatuakawekwa ndani wote. Tulikuwa kama 20. Tukiwa ndani tukawa tunabadilishana mawazo na madereva wenzangu. Wengi ni Bodaboda. Nikaambiwa hapa kesho asubuhi unatakiwa uandae wadhamini 2waje na barua za serikali za mitaa. Kweli kesho yake akaanza kutoka mmoja baada ya mwingine. Zamu yangu ilipofika nilidhaminiwa na mtu mmoja. Nikaachiwa kama saa 6 mchana. Nikaambiwa kesho saa 4(siku iliyofuata) nije na LESENI, KADI YA PIKIPIKI, BIMA, SUMATRANA RISITI.

Kesho nikaenda navyo vyote. Tumekaa pale asubuhi hadi mchana hakuna kinachoendelea ila naona wenzangu(wazoefu wa kukamatwa mjini) wanachukua pikipiki wanaondoka. Ikabidi na mimi nijiongeze nikamuuliza aliyetoka na pikipiki,utaratibu wa pikipiki ukoje?mbona nimeshakaguliwa lakini sioni nikiachiwa? Akaniambia Bro hapa huwa hawataki maneno wanataka pesa au uende mahakamani ukajitetee? Duuhh kusikia mahakamani nikapagawa.

Nikamuuliza wanataka kiasi gani? Nikaambiwa laki na nusu (150,000/=). Baada ya kukaa muda ikabidi na mimi niende ofisini pale kwa Afande Beka kwenye ofisi ya karibu na mwembe ili nilipe 150,000/=. sikkufanikiwa kumuona afande Beka. Nikapewa namba nimpigie askari anisaidie kuitoa pikipiki. Akaniambia bila laki na nusu pikipiki huitoi, nikamwambia laki na nusu ninayo. Akaniambia nisubiri baada ya nusu saa kwa sababu yupo mbali.

Baada ya nusu saa akanipigia simu nipeleke pesa. Nikaenda nikampa keshi 150000. Nikapelekwa kwa Afande Beka nikaaandikiwa kimemo, pikipiki nikapewa. SIUKUPEWA RISITI. NILIPOULIZA RISITI NIKAULIZWA KWANI PIKIPIKI YAKO HUJAPATA? NIKAISHIWA POZI IKABIDI NIWE MPOLE.

SEHEMU YA PILI.

Mwezi November. Picha linaanzia mataa ya kamata. Nikiwa nimesimama ktk mataa mara paap funguo zimechomlewa. Kama kawaida. Tukaenda kuwekwa kwenye karandinga karibu na roundabaout ya kuelekea sentro na mbagala. Ilipofika jioni aliletwa jamaa mmoja anashushiwa kipigo cha hatari. Alishushia sitiki za kufamtu. Kumbe yule jamaaalikua mwanajeshi ila yeye alikuwa abiria alivyoona wamerukia ufungua wa bodaboda aliyekuwa amemubeba alihisi kutaka kusababishiwa ajari, ikabidi awape adabu kidogo asikari duuh baada ya hapo walikusanyika kama wote walimshushia kipigo cha mbwa mwizi pamoja na kuwaonesha kitambulisho kama afisa wa jeshi hawakumuelewa, walimpa kipigo hadi akawa anatoa chozi kwa uchungu. Siku hiyo kama kawaida tukapelekwa central, usiku huo zilipigwa simu nyingi sana zikilenga kusaidia huyo mjeshi bila mafanikio. Siku hiyo tulikaa pale tukachuliwa maelezo hadi usiku wa saa 6. Baadae tulipelekwa mahabusu wote ,tukapekuliwa tukaingizwa chini lakini yule mjeshi alibaki kaunta tulikuja ambiwa kesho yake kuwa aliachiwa.

Kama kawaida utaratibu wa kutoka ulikuwa uleule. Nililipa 150,000/=BILA RISITI, BILA KUANDIKIWA MAKOSA MATANO ILI IENDANE NA PESA ILIYOLIPWA YA MAKOSA 5, ILA SIKU HIYO NILIANDIKIWA KOSA LA KUPITA MWENDO KASI WAKATI NIMEKAMATIWA MATAA YA KAMATA NIKIWA NATOKA POSTA.

SEHEMU YA TATU.

Baada ya pale baadhi ya madereva bodaboda walivyoona nakamatwa kizembe walinishauri nisiwe nasimama kwenye mataa. Wao huwa hawasimami kwe mataa kwa kuogopa kudandiwa na askari bila sababu za msingi. Nikaona hii imekaa poa sana. Na mimi sasa nikawa siheshimu mataa, nikiona upenyo tu napenya. Laikini hili halijanisaidia kwa sababu sasa hivi hawa askari wamejaa kila mtaa. Naambiwa wanatumia shirikishi na baadhi ya madereva bodaboda kukamata wenzao. Unaweza ukawa unatembea mara ghafla inabinywa clutch. Kwa style hii ya hovyo nimekamatwa mara 2 na mara zote hizi nilianguka chini kwa sababu ya kung'ang'aniwa clutch.

Kuna mbinu nyingine wanakublock na bajaji au na pikipiki kiasi kwamba wanaweza kukusababishia ajari. Hii mbinu nadhani imeanza baada ya kuona hatusimami tena kwenye mataa.

Picha linaanzia february. Nimekamatwa mara 5 toka february hadi jana. Kama kawaida mkamataji anaweza kukuliza kwanza una bei gani, mkimalizana anakuachia. Mara nyingi ukiwa na elfu 50, 30, 20 ya papo kwa papo unaachiwa. Kama huna pesa ya papo kwa papo ndo unafikishwa kwa pilato. Kwa afande Beka.

Angalau sasa hivi wamepunguza bei. Pale sasa hivi unaambiwa lipia makosa mawili yaani 60,000/=. Bila hiyo pesa huachiwi na chombo kinabaki polisi. NAWAONEA HURUMA BODABODA WANAOCHUKULIWA PESA ZAO BILA HURUMA KUWA WENGINE WANAENDESHA FAMILIA ZAO KWA KAZI YA BODABODA. Bodaboda na waendesha pikipiki wengine hapo mjini huo ndo mtindo wa kisasa. HII ADHA MADEREVA PIKIPIKI TUNAIPATA KWA SABABU YA TAMKO LA MH MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA.Unaweza kuwa na Kila kitu lakini ukifika pale unapigwa biti na maasikari pale utadhani umeua. Hupewi pikipiki ukaendelee na shughuli bila kulipia faini. Husikilizwi hata kidogo. Hii ni tofauti na gari unaandikiwa bill hata kama huna pesa kwa wakati huo unalipia baadae. HII HALI YA VITISHO, KUWEKWA NDANI , NA KULAZIMISHWA KULIPIA FAINI YA PAPO KWA PAPO NDO INAONGEZA RUSHWA NA HATUPEWI RISITI. PESA ZOTE ZINAISHIA PALE KWA AFANDE BAKARI BADALA YA KULIPA KWA CONTROL NAMBA AU KWA MHASIBU.

BODABODA NA MADEREVA WENGINE WA PIKIPIKI HASA WA DAR-ES-SALAAM NAO WANA FAMILIA. HUU UONEVU WA KUPIGWA FAINI KUBWAKUBWA UNAWAONGEZEA STRESS ZA MAISHA. MUDA UTAONGEA.
Pole sana, kwa majanga yaliyokukuta, polisi wetu na mabosi wao ni tatizo kubwa na wao ndo chanzo kikubwa cha ajali maeneo ya mijini
 
Kuna siku nilikuwa nawahi zangu bandarini asubuhi na usafiri ulikuwa wa tabu sana, kipindi hicho naishi zangu Temeke, hivyo nikaona nimchukue bodaboda nikamtia 5000 ili aniwahishe kufika Mivinjeni hao jamaa wako pembeni na kumsimamisha dereva bodaboda wangu, ile sijashuka kuna jamaa kavaa kiraia nae akaja kwenye pikipiki ili achomoe funguo, pale pale nami nikapeleka mkono wangu kwa kasi na kumbinya vidole vyake (Mwili wangu upo kimazoezi/hivyo nipo fiti). Nikamuuliza yule jamaa huku nambinya "kwanini unachomoa funguo na wewe ni nani" jamaa hakuwa na jibu zaidi ya maumivu na kumwita askari mmoja mwenye nyota mbili, alimwita kwa jina la inspekta. Hapo hapo nami nikapata pa kuanzia ile huyo inspekta kufika tu, nikamwambia "hivi ndivyo mnavyowafanyia watu. Basi yule inspekta alionesha kubabaika kidogo na kuniambia "tunawafanyia hivi kwasababu wengine huwa wanakimbia. Nikamuuliza sasa kosa lake ni lipi hadi mumchomolee funguo. Akaniambia wanafanya hivyo ili asikimbie. Nikamwambia tukae pembeni ili nijue wanataka kumfanya nini. Basi pale yule Inspekta akaonda huku akimwita sajenti mmoja hivi ili aje am attend yule boda boda. Nikawa niko pembeni nawasikilizia huku nikatoa simu yangu na kumpigia jamaa ambae ni askari na kumwomba namba ya RTO huku nikiongea kwa sauti. Kumbe yule inspekta ananisikilizia. yule jamaa kwenye simu akanijibu hana namba ya RTO ila nika act kumwambia kwa sauti "sawa nampigia sasa huyo RTO" ILE KUKATA SIMU TU akaja yule inspekta na kutwambia tuondoke.

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
Chai na ugali..kwa pamoja, shibe YAKE hunyanyuki bila winch!!!
 
Sina kesi upande wa bodaboda ila hawa jamaa wakikumata wanakupiga sachi kwanza.. Simu pesa ,saa na cheni wanavichukua wao..kaunta ukiandikisha wanasema tunaandika vitu tulivyopokea kutoka kwako..

Ukitoka ukiwa unafuatilia vitu vyako wanataka upeleke risiti ya vitu walivyokuchukulia .. Ukiwapa kopi ya risiti hawataki wanataka original.. Ukitoa original sahau kupata Mali yako wanaanza upya na kesi yako.. Utaambiwa mbona huripoti kila siku kesi yako bado haijaisha...ili mradi tu usidai Mali yako

Ukienda kwa mkuu wa kituo anamwita askari anaongea nae afu hamna chochote kinachoendelea..huu mchezo uko Arusha pale central..

So sad kwa wenye dhamana ya usalama wetu na Mali zetu ...japo kuna wachache wanafanya kazi zao kwa weledi na kufuata maadili ya kazi yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilikuwa nawahi zangu bandarini asubuhi na usafiri ulikuwa wa tabu sana, kipindi hicho naishi zangu Temeke, hivyo nikaona nimchukue bodaboda nikamtia 5000 ili aniwahishe kufika Mivinjeni hao jamaa wako pembeni na kumsimamisha dereva bodaboda wangu, ile sijashuka kuna jamaa kavaa kiraia nae akaja kwenye pikipiki ili achomoe funguo, pale pale nami nikapeleka mkono wangu kwa kasi na kumbinya vidole vyake (Mwili wangu upo kimazoezi/hivyo nipo fiti). Nikamuuliza yule jamaa huku nambinya "kwanini unachomoa funguo na wewe ni nani" jamaa hakuwa na jibu zaidi ya maumivu na kumwita askari mmoja mwenye nyota mbili, alimwita kwa jina la inspekta. Hapo hapo nami nikapata pa kuanzia ile huyo inspekta kufika tu, nikamwambia "hivi ndivyo mnavyowafanyia watu. Basi yule inspekta alionesha kubabaika kidogo na kuniambia "tunawafanyia hivi kwasababu wengine huwa wanakimbia. Nikamuuliza sasa kosa lake ni lipi hadi mumchomolee funguo. Akaniambia wanafanya hivyo ili asikimbie. Nikamwambia tukae pembeni ili nijue wanataka kumfanya nini. Basi pale yule Inspekta akaonda huku akimwita sajenti mmoja hivi ili aje am attend yule boda boda. Nikawa niko pembeni nawasikilizia huku nikatoa simu yangu na kumpigia jamaa ambae ni askari na kumwomba namba ya RTO huku nikiongea kwa sauti. Kumbe yule inspekta ananisikilizia. yule jamaa kwenye simu akanijibu hana namba ya RTO ila nika act kumwambia kwa sauti "sawa nampigia sasa huyo RTO" ILE KUKATA SIMU TU akaja yule inspekta na kutwambia tuondoke.

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
Kufika mbele yule bodaboda akaniambia kuwa nimemsave sana maana kwa jinsi ilivyo zingemtoka hata 30,000 asubuhi tu hiyo.

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
 
Back
Top Bottom