Miaka kadhaa iliyopita nilileta posts nikiomba ushauri jinsi ya kukabiliana na hali ya kutokuwa na mtoto katika ndoa yangu kwa miaka kadhaa. Niliwashukuru, na naendelea kuwashukuru walionipa matumaini. Namshukuru Mungu kwani hatimaye, mapema mwaka huu mimi na mke wangu tulijaaliwa mtoto...
Kwa asilimia 100 naamini Mungu ndiye aliyetenda miujiza. Kama Mungu alitumia mkono wa mwanadamu pia katika hilo, basi naomba nimtaje Dr Kibona (simjui jina la pili) wa Dar. Ingawa mwanzoni tulimpuuzia Dr huyu anayetumia vidonge vya miti shamba, lakini baadaye (pengine kwa kuongozwa na Mungu), mke wangu alikuja kufuata ushauri na kwenda kumtembelea, na ingawa mimi nilitakiwa pia niende kuchekiwa na kupewa dawa, sikufanya hivyo (pengine kukata tamaa? sijui)...
Sitaki kueleza mengi, lakini waliomshauri mke wangu kwenda huko, walishuhudia kuwa wanandoa wengi walifanikiwa baada ya kutumia vidonge kutoka kwa huyu jamaa. Na hapa ninapoandika, marafiki zetu wawili (ndoa mbili tofauti), ambao tuliwashauri waende kwa Dr huyu, baada ya mke wangu ku-conceive, nao walifanikiwa, mmoja ameshajifungua na mwingine ana ujauzito mchanga siku miezi kama mitatu baada ya kuanza kutumia dawa...
Kwa bahati mbaya sijui hasa ofisi yake, lakini najua clinic yake ipo Dar, maeneo ya Ubungo au Shekilango ( I am not sure). Kwa ambao wana tatizo na wanadhani wako tayari kutest hiyo option, wajaribu.
Asanteni...