Ushuhuda: Mchemsho niliokunywa, haikupita nusu saa nikawa fresh mpaka nikawa naona furaha ya kupumua

Ushauri:

Dawa izo za tangawizi na malimao mtumie kwa kiasi.

Wanasema anything in excess is harmful.

Kuna mtu tayari anahaingaika na matatizo ya koo...ametumia tangawizi nyingi
 
Corona imeleta kizaazaa asee mifumo yote ya maisha imevurugika halafu maisha nayo yanazidi kuwa magumu inshort tumeisha Ni muda wa kutubu na kusali sana
miaka hii tunaangalia kwenye filamu wanaume wakikazana na kuona kawaida, Mungu amelikataza hili katika dini zote lakini kuna baadhi ya madhehebu wameanza kufungisha ndoa watu wa jinsia moja. Mungu yupo aisee
 
Habari watanzania na wanaafrika mashariki kwa ujumla.

Nimeona tushare namna mbalimbali tulivyopambana na hii nimonia inayobadilikabadilika kwa lengo la kushtuana ili wengine nao wajifunze.

Naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi, lakini shuhuda za wengine ni muhimu pia. Huu ugonjwa nilianza kuusikia sana mwezi ule wa 3 mwaka jana lakini sikutilia maanani mpaka tuliposimamishwa kazi kwa wachina kwenye kampuni ya ujenzi kwa sababu ya hili gonjwa ndipo nikaanza kuwa na hofu, ukizingatia kipindi hicho watu wengi walizingatia mwongozo uliotolewa wa kila mtu kuchukua hatua ya kutumia vitakasa mikono pamoja na kuvaa barakoa.

Tulisimamishwa kazi nikakaa nyumbani na familia mpaka mwezi wa 5 ndipo mwanangu akaanza kuugua kikohozi kikavu kiasi kwamba alikohoa mpaka akawa amedhoofu... Nilimpeleka hospitali akaonekana hana ugonjwa wowote ikabidi apewe dawa za kikohozi tu ambazo zilimsaidia akapona.

Wakati mwanangu anatumia dawa kikanishika mimi na mke wangu pia lakini hatukwenda hospital bali tulipona bila kutumia dawa.
Hivyo awamu ya kwanza ikapita ambapo iliambatana na kuumwa kichwa, kukohoa kusiko na mafua, kupoteza ladha na harufu.

Awamu ya pili ilinikuta mwenyewe maana mke na mtoto walisafiri. Awamu hii ilikuwa mwezi wa 11 mwanzoni ambapo yalianza mafua ya ghafla mara kesho yake nikaamka nipo hovyo, joto la mwili limepanda na kichwa kikawa kinauma. Nilivunga tu nikaona nitapona maana nina kawaida siendi hospital mpaka nizidiwe... Siku ya pili nikawa nimezidiwa zaidi alafu nikawa naumwa kila mahali alafu maeneo ya kiunoni kukawa kumekufa ganzi, miguu ikawa inauma hatari na kichwa kikawa kinauma, koo likawa limevimba alafu kavu kinoma huku naharisha!

Hofu ikatanda nikawa nakula malimao na pombe kali nikawa nawaza kesho lazima niwahi hospital. Kesho yake nilizidiwa zaidi nikawahi hospitali asubuhi nikamweleza doctor hali yangu, akashtuka akakaa mbali kidogo tukawa tunahojiana mwisho akaniambia nikafanye vipimo chumba cha pili.

Nilichukuliwa vipimo vya damu, mkojo, kinywani niliangaliwa kukaonekana kuna dalili ya vidonda alafu kumevimba, nikapimwa kifua lakini majibu yakaonesha nina typhoid tu.

Niliandikiwa dawa nyinginyingi ambazo sikuzielewa bahati mbaya nikawa sina hela ya kutosha maana hela niliyokuwa nayo iliishia kwenye vipimo nikabaki na buku tano tu, ila nilipotaka kuondoka bila dawa daktari akaniuliza una Tsh ngapi nikamjibu nina Tsh 5,000, akanipa azuma kipaketi kimoja akanitaka niendelee kutumia alafu nikanunue dawa ningine zilizobaki.

Nilipofika home nikameza kwa utaratibu wa daktari kesho yake nikaamka vizuri kabisa nikawa nimebaki na mafua tu... Nikaendelea na ile azuma bila kununua dawa nilizoelekezwa mpaka nikapona kabisa na haikuchukua hata wiki.

Awamu ya tatu ndio hii iliyonishika juzi kati hapa mwanzo wa mwezi huu wa pili! Hii ilianza na mafua tena lakini ni kali kuliko zote maana nilifika hatua mpaka kupumua ikawa napumua kwa shida. Yalianza mafua mchana, usiku nikawa na dalili za malaria, asubuhi ya saa kumi na moja nikawa napata tabu hadi nikawa napumua kwa mdomo pamoja na pua/yaani ilibidi nilale chali alafu nikaacha mdomo wazi maana niliona pua hazitoshi!

Pamoja na kuacha mdomo wazi bado pumzi zilikuwa hazitoshi alafu nikawa nikipumua nasikia kifua kinakoroma kwa ndani.
Nikawasha marijuana nikavuta lakini wapi... Kutokana na tanzia nilizokuwa nazisoma humu Jamiiforums, moja kwa moja nikawaza hii ni zamu yangu!

Kadri nilivyokuwa nawaza itakuwaje ndivyo hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya maana mpaka kufika saa kumi na mbili asubuhi nilikuwa nikipumua nasikia kifua kinapiga mluzi kabisa.

Nikaamka nikakaa huku mwili wote ni mzito kama jabali.
Wakati nawaza nikakumbuka kuna habari niliisoma humu sikumbuki aliileta nani, ambapo ilikuwa inaongelea ule mchanganyiko wa NIMR.

Kwa kuwa kazi yangu nauza matunda na viungo mbalimbali/genge la matunda), niliamka muda huohuo nikawahi kibandani nikakusanya matirio ambapo ni;

Malimao mawili

Kitunguu saumu kimoja kikubwa

Tangawizi yenye kitu kama g100 pamoja na kitunguu maji cha wastani chekundu.

Kitu nilichokuwa sina kibandani ni pilipili kichaa ambazo kwa mujibu wa NIMR zinatakiwa pia ziwemo.

Baada ya kuchukua vitu hivyo nikarudi magetoni nikavikwangua kwenye kikwangulio kwa kuwa sina Brenda, nikaweka maji nusu lita alafu nikakamulia humo Malimao nikachemsha.

Baada ya dakika chache nikaepua nikachuja alafu nikanywa karibia nusu ya chupa alafu nikafanya vimazoezi vidogovidogo kama kurukaruka, kurusha ngumi, kujinyooshanyoosha na baada ya hapo nikatulia.

Hamuwezi kuamini haikupita nusu saa nikawa fresh mpaka nikawa naona furaha ya kupumua.
Nilikuwa mwepesi kabisa kichwa kikapoa, mwili ukawa fresh nikawa nimebaki na mafua tu ambayo nayo yalianza kukauka kesho yake. Kumbuka huu mchemsho nilikunywa tena mchana kidogo, jioni kidogo na usiku nikamalizia.

Mpaka muda huu ninavyoandika hapa mimi ni mzima kabisa ila sijui itakaporudi itakuwa na nguvu kiasi gani.

Nilichojifunza kwenye huu ugonjwa ni kwamba una tabia ya kurudi kwa nguvu zaidi au kwa dalili za ziada.

Naomba kwa waliougua wakapona waweke shuhuda zao ili wengine wajifunze pia... Haijalishi umepona kwa dawa zipi, ziwe za hospitali au za kienyeji, wewe weka tu huwezi kujua utaokoa wangapi.

Kumbuka huu ugonjwa kila unaempata unakuwa na dalili za tofautitofauti japo kuna dalili za msingi ambazo hufanana kwa wote.
Nasema hivyo kwa sababu hapa mtaani kuna ambao nimeona wakipatwa na huu ugonjwa sauti inapotea kabisa mpaka ukiongea nao wanaongea kwa ishara tu.
Hongera kwa kutoboa, shukrani kwa kushare pia!!
 
Ushauri:

Dawa izo za tangawizi na malimao mtumie kwa kiasi.

Wanasema anything in excess is harmful.

Kuna mtu tayari anahaingaika na matatizo ya koo...ametumia tangawizi nyingi
Mkuu hata maji ni uhai kwa binadamu lkn ukizidisha ni shida
Hata dawa za hosptari zina dozi kulingana na umri wa mgonjwa kilo za mgonjwa historia ya ugonjwa nk
Na zaidi zina side effect
Vyivyo hivyo kwenye limao na tangawizi
Luck ni kuwa tangawizi na limao ni faida 99% ya nutrition zake
Hvyo hakuna side effect zenye madhara kwa kiasi kikubwa
Hvyo unavyosikia watu wanakunywa mchanganyiko wa tangawizi na limao sio wanajinywea utaratibu kikombe kimoja cha chai kutwa mara tatu au 2

Hivi kwa mfano mnavyopinga kuhusu hii tiba toeni ushauri tutumie nini ?
AZITHROMYCIN au AMOXICILIN Ama

Ebu tutajieni dawa 1 tu waliothibitisha WHO inatibu hao VIRUS au yoyote mnayoijua inatibu hawa wadudu
 
Kwa maelezo yako hizi dawa za kienyeji zinavubaza hazitibu?
 
Mimi sijapinga mkuu. Nawatahadharisha tu watumie kwa kiasi.

Mana kuna watu wanaona kadri ukitumia tangawizi na malimao kwa wingi na kila wakati ndio utapona mara moja. Wakati wanaweza kusababisha matatizo mengine ya kiafya.

Ni vizuri kutumia. Na hasa tangawizi lkn kwa kiasi na portions ndogondogo.
 
Nilichogundua kwenye hii thread ni kuwa; mleta uzi hatofautiani na mchangia mada wa kwanza, inawezekana vipi mchangia mada wa kwanza akacomment yenye sentensi nyingi namna hiyo kama siyo aliiandika hii mada kabla(copy & paste)...!!
Kwa huo muda aliotumia kucomment ingekuwa tayari mdau mwingine kashacomment tayar na kuwa wa kwanza hapo juu kwa member waliochangia mwanzoni kabisa.

Nyie mpango wenu ni kupotosha wananchi, either iwe ni kisiasa au sababu zenu nyingine mnazojua nyie.
RAI: Mbinu mnazotumia kwa mtu mwenye ueledi ni rahisi kugundua
Mwemyewe nimestuka hii ishu
 
Kwa maelezo yako hizi dawa za kienyeji zinavubaza hazitibu?
Na hakuna dawa mpaka sasa inayotibu CORONA VIRUS
dawa tunazo tumia hizi MCHANGANYIKO WA tangawizi limau nk hata zinazotumika MAHOSPTARI zinatibu Makari au matokeo ya MASHAMBURIZI ya CORONA km hvyo mashamburizi mfumo wa hewa kichwa kikari homa mafua tonses nk
Kwa mfano INDIA wao wanatumia klolokwini kuwatibu wagonjwa wa CORONA inawasaidia baadhi lakini si tiba sahihi wengne wakitumia klolokwini ndio wanadanja kabisa
Mpk WHO ikapiga marufuku klolokwin

Hakuna dawa iliyothibitishwa au thibitila ama yenye ushaidi inaua VIRUSI vya CORONA
Zaidi ya KINGA ZA MWILI wetu kupambana na hivyo vidudu

Kwa hvyo mkuu tule vizuri vyakura vya kuchoche kinna mwili kujenga mwili yaan tupate mro kamiri tufanye mazoezi na kubwa unapohisi dalili kuchukua hatua mapema ya kuimalisha kinga ili iwe madhubuti katika kupambana na hivi VIDUDU
 
Huo mchanganyiko unasaidia kutibu mafua makli, nimekuwa nikiutumia kwa miaka mingi. Tofauti ni kwamba kwenye mchanganyiko wangu wa kutibu mafua makali pamoja na hizo tangawizi, limao, vitunguu huwa naongeza na karoti moja kubwa
Mchanganyiko wa kutibu mafua makali huwa sichemshi bali nasaga tu tangawizi, kitunguu na karoti pamoja na limao bila kumenya maganda, baada ya kusaga nakamua na kupata juisi nzito ambayo nakunywa kijiko kimoja cha chakula kutwa mara tatu
Hata uwe na mafua makali vipi mchangantiko huu unakausha
Ukiangalia hapo kwenye huo mchanganyiko unakuta umepata virutubisho vinavyoimarisha kinga ya mwili. Vitunguu vinakupatia zinc, limao lina vitamin C kwa wingi, kwenye katoti unapata Vitamin A, hapo kinga inakuwa juu mawinguni
 
Asante sana... Nimejifunza jambo jipya
 
Back
Top Bottom