G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Nilijiuliza inakuwaje ana mafua makali namna hiyo na kikohozi wakati huu wa joto kali! Tukio lilianza siku ya ijumaa iliyopita. Nikadhani masihara. Jumamosi jioni naona mambo yanazidi kuwa magumu. Huku nawaza sana inakuwaje hali ile wakati huu wa joto kali? akaenda akachoma sindano ya kufanya kifua kiachie!
Jumapili mchana hali bado ikazidi kuwa tete akaenda akawekewa mashine ya kupumulia inayotoa mvuke. Kidogo hali ikatengamaa. Jumatatu anaamka mambo bado magumu. Ikalazimu akawekewe tena mashine hiyo ndani ya hospitali nyingine na kupewa dawa kali za kutuliza maumivu. Hali yake kwa sasa ni nzuri ila ndiyo bado anakohoa na mafua.
Sijui na bado nawaza kilichopelekea mafua na kikohozi kile kipindi hiki cha joto kali!
Kama lipo tatizo basi serikali ituambie ukweli tuu! Mimi naandika huu ujumbe ninauguza na niliyoyaandika hapa yametokea kwa huyo mzazi mwenzangu!