sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,014
Kila shule na kila faculty vyuoni ina hawa viumbe wanaitwa vipanga; ni watu ambao wanafanya vizuri sana darasani aidha kwa kutumia jitihada kubwa ama uwezo mkubwa wa akili waliojaaliwa.
Tatizo sio kuwa kipanga, tatizo ni kuwa kipanga jeuri, ni wale watu wanaofanya vizuri darasani na kuona kwao tayari washapita mtihani wa maisha, yaani ni wale type za kuringa, zenye kujitenga pamoja na vipanga wenzao, wanaonyima watu chabo kwenye mitihani n.k
Sasa navyosoma zamani kulikuwa kuna huyu bwana alikuwa na tabia hizi na kiukweli kwake namba yake ilikuwa ni moja tu, yani alikuwa na tabia kama hizo nilizotaja, Chuoni assignment zake, notes zake za summary, n.k alikuwa anatunyima na hata kuwaita wazi wazi wasio na uwezi darasani ni vilaza.
Nimekodisha frem sehemu flani nimeweka binti awe anauza maana mimi muda mwingi nipo kazini, sasa kuna rafiki yangu tunaefanya nae kazi akavutiwa kufungua biashara ya kipati cha ziada, nikamshauri achukue fremu eneo lile nililopo maana ni pazuri, basi taratibu zikafanyika na rafiki yangu akafungua stationery kubwa tu.
Leo nlipotoka kazini nilienda dukani kwangu kuhesabu mzigo lakini pia lengo kuu nilikuwa na shauku kubwa ya kuona mradi wa huyu rafiki yangu maana leo ndio rasmi alianza kuuza.
Kufika pale nikapigwa na butwaa, nikaona kijana wa kazi pale ni yule kipanga, kiukweli nilihisi nmechanganya sura maana nilijua jamaa atakuwa huko kwenye vitengo vya juu au kufundisha vyuoni.
Nlimwita jina akaitikia nikajua hapa sijakosea ni yeye, basi ndio nikamkumbusha ndo akanijua akaniambia kafungua steshonari yeye, mimi nikawa namchora tu mbona ananidanganya, rafiki yangu akafika akamtambulisha huyo ndio kijana wake wa kazi, dah basi kwa kipanga ikawa aibu tupu.
Wakati wanafunga tukaagana na yule rafki yangu na mimi nikafunga maana dada wa kazi alikuwa kaniacha, nikamkuta njiani kipanga nikamwambia apande kama anajitaji lifti yeye akasema anasubiri mtu.
Usiku huu namcheki WhatsApp, nmemtumia message hadi sasa kaisoma ila hajajibu