Ushuhuda: Leo nimekutana na kipanga jeuri wa darasani. Kweli hakuna uhusiano wa uwezo darasani na wa maisha halisi

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,014
Kila shule na kila faculty vyuoni ina hawa viumbe wanaitwa vipanga; ni watu ambao wanafanya vizuri sana darasani aidha kwa kutumia jitihada kubwa ama uwezo mkubwa wa akili waliojaaliwa.

Tatizo sio kuwa kipanga, tatizo ni kuwa kipanga jeuri, ni wale watu wanaofanya vizuri darasani na kuona kwao tayari washapita mtihani wa maisha, yaani ni wale type za kuringa, zenye kujitenga pamoja na vipanga wenzao, wanaonyima watu chabo kwenye mitihani n.k

Sasa navyosoma zamani kulikuwa kuna huyu bwana alikuwa na tabia hizi na kiukweli kwake namba yake ilikuwa ni moja tu, yani alikuwa na tabia kama hizo nilizotaja, Chuoni assignment zake, notes zake za summary, n.k alikuwa anatunyima na hata kuwaita wazi wazi wasio na uwezi darasani ni vilaza.

Nimekodisha frem sehemu flani nimeweka binti awe anauza maana mimi muda mwingi nipo kazini, sasa kuna rafiki yangu tunaefanya nae kazi akavutiwa kufungua biashara ya kipati cha ziada, nikamshauri achukue fremu eneo lile nililopo maana ni pazuri, basi taratibu zikafanyika na rafiki yangu akafungua stationery kubwa tu.

Leo nlipotoka kazini nilienda dukani kwangu kuhesabu mzigo lakini pia lengo kuu nilikuwa na shauku kubwa ya kuona mradi wa huyu rafiki yangu maana leo ndio rasmi alianza kuuza.

Kufika pale nikapigwa na butwaa, nikaona kijana wa kazi pale ni yule kipanga, kiukweli nilihisi nmechanganya sura maana nilijua jamaa atakuwa huko kwenye vitengo vya juu au kufundisha vyuoni.

Nlimwita jina akaitikia nikajua hapa sijakosea ni yeye, basi ndio nikamkumbusha ndo akanijua akaniambia kafungua steshonari yeye, mimi nikawa namchora tu mbona ananidanganya, rafiki yangu akafika akamtambulisha huyo ndio kijana wake wa kazi, dah basi kwa kipanga ikawa aibu tupu.

Wakati wanafunga tukaagana na yule rafki yangu na mimi nikafunga maana dada wa kazi alikuwa kaniacha, nikamkuta njiani kipanga nikamwambia apande kama anajitaji lifti yeye akasema anasubiri mtu.

Usiku huu namcheki WhatsApp, nmemtumia message hadi sasa kaisoma ila hajajibu
 
Mara nyingi stori kama hizi huwa zinatoka kwa watu waliofeli masomo yao darasani au waliokuwa hazichaji kichwani na huwa faraja yao pekee ni kusubiri kipanga mmoja apigwe na maisha warudi kusema 'yako wapi sasa'!

Lakini wanasahau kwamba ukiwa na cheti au akili, hela bado una nafasi ya kuitafuta. Lakini hata kama una hela, kama hazichaji kichwani bado haziwezi kuja na hauwezi kuzitafuta akili kwa hela zako
 
Ni maisha tu mkuu. Huwezi jua mpaka amefikia hatua hiyo ya stationary nini kimempata. Sitaki niseme mengi ila usimseme vibaya hata kwa boss wake(rafiki yako). Hayo mengine vyuoni inakuwa utoto tu hasa kwa wale wanaotoka fresh from school wanakuwa wanakaushindani na akili za secondary, mwaka wa 3 au 2 second term ndiyo huwa wanakomaa na kuacha mashindano.
 
Hakuna maisha nayapenda Kama kujishusha mbele ya jamii, wale kazi zao zinazodharaulika ndio huwa nawafanya marafiki nawasalimu kwa ukarimu, Basi najisikia amani sana.

Una nyodo na jeuri ya shibe, ukishiba leo kumbuka kuna aliyekosa hata ngumi moja ya hicho chakula, kesho giza rafiki yangu usije kuona aibu tu.

Huyo mate wako ni kiburi, ingekuwa Ni Mimi ningechangamka na ningepanda lift ili tu kukuonyesha kuwa najikubali na hali yangu.
 
Wewe ni mjinga hata kudanganya hujui !
IQ yako ndogo sana! Mtu mliyesoma naye darasa moja obviously atakuwa age mate wako!
Sasa ulivyom-address na huyo rafiki yako alivyom- address kijana wake wa kazi kwako obviously hakuna uhalisia wowote! Hizi ni story za vil.aza kutungia vil.aza wenzao
Stori nzuri sana hizi huku ukishushia na ka haileee
 
Wewe ni mjinga hata kudanganya hujui !
IQ yako ndogo sana! Mtu mliyesoma naye darasa moja obviously atakuwa age mate wako!
Sasa ulivyom-address na huyo rafiki yako alivyom- address kijana wake wa kazi kwako obviously hakuna uhalisia wowote! Hizi ni story za vil.aza kutungia vil.aza wenzao
Nina 29 yeye ana 28 sisi ni wazee??
 
Wa kwanza atakuwa wa mwisho, na wa mwisho atakuwa wa kwanza. Tatizo watu wanaokuwa wa kwanza hivyo wanaingia kiburi mapema katika umri mdogo, ila game ya maisha mwenye kiburi LAZIMA ASHINDWE.

Huoni bado ana kiburi hadi leo na anashindwa kukubaliana na hali na kuwa mkweli na muwazi? Mwambie rafiki yako ASIMWAMINI SANA HUYO JAMAA, ANAWEZA HATA KUMWIBIA KILA KITU. Sio suala la kumharibia, lakini ameshajiharibia na sasa ni kumlinda rafiki yako na biashara yake.
 
Ukipanga ni muhimu ukiwa shuleni, chuo. Ila sio lazima uwe jeuri.

Watu Kama Freddy vunja bei, Au Mark zuckerberg, sidhani Kama walikuwa vilaza shuleni.

Ni tatizo la nchi yetu tu, wale vipanga wa Darasani ukiwapa nafasi kwenye vitengo maalum, Kama IT, finance, Kilimo, tafiti, Security hufanywa Maajabu. Hata kwa wenzetu majuu,wasomi kutoka Ivy league,(yale university,nk)hupewa kipaumbele kwenye nafasi nyeti.
 
Wewe muongo na uongo wako hujaupangilia maana kama amepigika kweli atakuwa mzee kuliko wewe kimuonekano. Hivyo rafiki yako hawezi kumwita kijana wake bali mzee wake
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom