USHUHUDA: Ku-date na myahudi kumebadilisha maisha yangu

Junior Rutashoborwa

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
228
210
Hi everyone in here,

Kabla ya kukutana na Linda, nilikuwa sina hamu yyte ya kuingia kwenye mahusiano, maana mahusiano yalichonifanya sitakuja kusahau kamwe!

Linda, ni binti mrembo sana, sio sura, sio shepu vyote amejaliwa. Urefu futi sita kama kitanda. Nywele zake natural ndefu mpaka mgongoni. Macho ya blue. Ana-dimpoz na zaidi napenda sauti yake ilivyotamu.

Akikutukana huwezi jua. Maana utahisi amekusifia. Sauti na maneno haviendani. Nakumbuka mwanzo wa mahusiano yetu ilinichukua muda sana kutofautisha kama amekasirika au amefurahi.

Mimi na Kinda tulikutana chuo kikuu( Oxford University). Yeye alikuwa akisoma sheria, Mimi nachukua...( Sitaji kwa sababu ya usalama wangu maana hii fani nchini tupo wawili tu mmoja ni kiongozi mstaafu). Mwanzo ilikuwa ngumu kumpata ila badae tulipendana tu.

Linda alinikubalia kwa mashariti makuu manne.
1. Nibadilishe dini. Yaan niwe myahudi
2. Nisiishi Tanzania. Yeye anataka tuishi Paris au Jerusalem.
3. Niache pombe na nisivute sigara.

Mwenzenu kwa sasa nipo kwenye mchakato wa kubadili dini. Siku hizi Jumamosi sifanyi kazi, japokuwa siendi kwenye sinagogi. (Maana sijui yalipo)

Kwa sasa ninafuraha sana. Maisha yangu ya mahusiano ni tofauti na yale ya zamani niloyokuwa na date na binti wa Kizaramo.

Mapenzi ni maisha tujitahidi sana tusikosee kuchagua mwenzi wa maisha. Maana ukikosea itakuathiri maisha yako yote.

Jambo Tanzania.
 
Back
Top Bottom