USHUHUDA: Hii ndiyo michezo hatarishi ya Kampuni ya Mafuta ya Oilcom

FUHRER

Member
May 29, 2013
87
644
Juzi nimefungua uzi wenye kichwa cha habari, "USHUHUDA: Jinsi kampuni za mafuta zinavyokwepa ushuru" nikatoa mfano mmoja wa kampuni ya OILCOM inavyokwepa ushuru. Kuna watu wameni-inbox vitisho.

Sasa natoa mfano mwingine wa OILCOM hiyohiyo.

Baada ya gas ya songosongo kuanza kuchakatwa (Gas processing). Kampuni ya OILCOM ilipata tender ya kununua Naptha ambayo ni byproduct ya gas processing. Hii naptha ni mojawapo ya condensate katika Natural Gas Liquids (NGL) ambazo huwa zina-liquify katika surface separator.

Kwa wasioijua hii Naptha ni ile thinner inayotumika kuchanganyia rangi. Sasa hii naptha inatumika katika viwandani kutengenezea Rangi. Sasa OILCOM ndio Dealer mkubwa wa hiyo naptha pale songosongo. Huwa anapeleka meli pale Songosongo na kupakia mzigo wa kutosha na kuja kuushusha kwenye depot yake pale kurasini. Kwa mkataba wake OILCOM ni kwamba anaiuza kwenye viwanda vya rangi vya hapa nchini na nyingine ana-export nje ya nchi.

Anachokifanya kwenye depot yake pale kurasini ni kui-blend na Petrol (PMS) kwa ratio nzuri na kuongeza na Octane boosters ili afikie viwango vinavyohitajika vya AKI (Anti Knocking Index) na anatuuzia kwenye service station zake kama petrol.

Parameter anayoi-monitor kwenye hii petrol anayotu-blendia ni hiyo OCTANE number tu kwa sababu anajua kuwa akikosea hiyo atauwa injini za magari yote yanayotumia petrol na effect yake watu wataiona immediately wakijaza kwenye station zake.

Parameter nyingine kama oxygen content na vapour pressure hashuguliki nazo kwakuwa effect zake zipo kwenye ulaji wa mafuta wa injini na kutoa moshi. (Effects of low and high oxygen content)

Hii petrol yenye naptha ya songosongo tumeuziwa kwa muda mrefu sana na wakuu wanajua kuanzia EWURA hadi TRA. Yupo afisa mmoja wa TRA wa kitengo cha mafuta ambaye alikuwa ndio kama Resident Custom Officer pale Oilcom anaitwa GEORGE, yeye ndio alikuwa kiunganishi wa OILCOM kwenye haya magumashi.
 
Juzi nimefungua uzi wenye kichwa cha habari, "USHUHUDA: Jinsi kampuni za mafuta zinavyokwepa ushuru" nikatoa mfano mmoja wa kampuni ya OILCOM inavyokwepa ushuru. Kuna watu wameni-inbox vitisho.

Sasa natoa mfano mwingine wa OILCOM hiyohiyo.

Baada ya gas ya songosongo kuanza kuchakatwa ( Gas processing). Kampuni ya OILCOM ilipata tender ya kununua Naptha ambayo ni byproduct ya gas processing. Hii naptha ni mojawapo ya condensate katika Natural Gas Liquids (NGL) ambazo huwa zina-liquify katika surface separator. Kwa wasioijua hii Naptha ni ile thinner inayotumika kuchanganyia rangi. Sasa hii naptha inatumika katika viwandani kutengenezea Rangi. Sasa OILCOM ndio Dealer mkubwa wa hiyo naptha pale songosongo. Huwa anapeleka meli pale songosongo na kupakia mzigo wa kutosha na kuja kuushusha kwenye depot yake pale kurasini. Kwa mkataba wake OILCOM ni kwamba anaiuza kwenye viwanda vya rangi vya hapa nchini na nyingine ana-export nje ya nchi.

Anachokifanya kwenye depot yake pale kurasini ni kui-blend na Petrol (PMS) kwa ratio nzuri na kuongeza na octane boosters ili afikie viwango vinavyohitajika vya AKI (Anti Knocking Index) na anatuuzia kwenye service station zake kama petrol.
Parameter anayoi-monitor kwenye hii petrol anayotu-blendia ni hiyo OCTANE number tu kwa sababu anajua kuwa akikosea hiyo atauwa injini za magari yote yanayotumia petrol na effect yake watu wataiona immediately wakijaza kwenye station zake.

Parameter nyingine kama oxygen content na vapour pressure hashuguliki nazo kwa kuwa effect zake zipo kwenye ulaji wa mafuta wa injini na kutoa moshi. (Effects of low and high oxygen content)
Hii petrol yenye naptha ya songosongo tumeuziwa kwa muda mrefu sana na wakuu wanajua kuanzia ewura hadi TRA. Yupo afisa mmoja wa TRA wa kitengo cha mafuta ambaye alikuwa ndio kama Resident custom officer pale oilcom anaitwa GEORGE, yeye ndio alikuwa kiunganishi wa OILCOM kwenye haya magumashi
Daaaa hiii tanzania ni vichekesho,wakati wenzetu uganda wanajiandaa kuanza kutengeneza magari kwa ajili ya matumizi yao na kuuza nje ya nchi,tanzania tunahangaikia jinsi ya kuchakachua mafuta
 
Siku ile nilikwambia uwe makini, na Leo nakusisitiza Ndg yangu uwe Makini.. Taarifa hizi Ni nyeti kuliko hata nyeti tulizonAzo...

Zamani tulikua na petrol inAkua Kama Nyekundu, sikuhizi petrol Kama Mafuta ya taa Kumbe Ni feki, Dah.. Haya Maisha hAya!!!

Mkuu yeyote akikujua PM na msg ya kitisho weka ID Yake hapa hadharani tuwajue walanguzi na wahujumu uchumi..

Mwisho Kabisa... Kuwa makini na mienendo yako popote uendapo, matajiri wanamkono mrefu!!!

Mungu anaeishi Akulinde siku zote za Maisha yako hapa chini ya jua.
 
Back
Top Bottom