USHUHUDA: Haya ndio maendeleo niliyoyapata kupitia JamiiForums

Safi sana Nadiriki kusema JF ni zaidi ya chuo kikuu!mimi nimefaidika sana na JF
 
Kwanza kabisa nitaaendelea kupiga salute kwa Maxence Melo na cabinet nzima waliokaa wakaleta hii mambo,pamoja na member wote waliojiunga na jukwaa hili.
For sure i salute you guys and i wish you well...

Nakumbuka nimejiunga jamiiforum tarehe 11 mwezi wa 3 mwaka 2013 hapo awali nilikuwa nje ya uwanja sikuwa nachangia chochote lakini baada ya kujiunga rasmi hakika nilinufaika sana na haya ndo maendeleo ambayo niliyapata kutoka jamii forum.

1.NILIANZA BIASHARA YA KUUZA NGUO,VIPODOZI NA UREMBO NIKIVITOA UGANDA.

Biashara hii niliianza rasmi baada ya kupata detail nyingi ambazo nilizipata kupitia wadau walioeleza juu ya unafuu wa bei za vitu mbalimbali nchini uganda hii ilinishawishi niweze kusafiri mpaka uganda nikiwa sina mwenyeji yoyote wa kunipokea na hii safari niliifanya kwa ajili ya kwenda kuziona hizo fursa zilizopo uganda kama ujuavyo mwanaume jasiri popote unajilipua wapambanaji tunasema coast to coast,kila angle ya dunia pesa ilipo unaifaata.

Sasa basi huu ulikuwa mwaka 2014 mwanzoni tu baada ya kupitia nyuzi nyingi zilizoletwa na wadau hapa jf juu ya jinsi gani unaweza kusafiri baadhi ya nchi jirani,za mbali na ukafika na kujifunza na pia ukaziona fursa mbalimbali achilia mbali zilizopo nchini kwetu.
Binafsi niliona nianze na uganda kwa sababu nyingi ikiwemo ni nchi jirani sana,pesa yake ipo chini sana kuliko ya kwetu pia bidhaa nyingi ni cheap ukulinganisha na za hapa nchini nazani ndio hicho ndo kilinisukuma zaidi.

Kabla ya safari niliaandaa vitu vifuatavyo
>Passport ya kusafiria ambayo unaipata uhamiaji(migration)
Hapa zipo za aina mbili kuna ya muda mfupi(temporary passport) yaani ya karatasi ambayo unaipata kwa shilingi elfu 10000/=tu,
na ya muda mrefu(miaka kumi) hii ni ya kitabu mabaharia wanaiita kadi ya CCM unaipata kwa shilingi elfu 50,000/=tu.

View attachment 531298
Hizi zote zinapatikana ofisi za uhamiaji kwa dsm unaweza kufika kurasini.

View attachment 531350
Nyamayiba bus terninal kampala

>Yellow fever card
Hii unaweza kuipata mpakani mwa nchi au kuna vituo ambavyo hutoa chanjo pamoja na kadi

1. Hospital ya Mnazi mmoja ya jijini Dsm, wanatoa hiyo huduma kwa TZS 55,000 (Elfu Hamsini na tano);

2. Holili Mkoani Kilimanjaro TZS 20,000 (Elfu Ishirini);

3. Azam Marines pale Posta - Dsm wanatoza TZS 20,000

4. JN & K International Airports wanatoza 40 USD
Bei zinatofautiana sana ila huwa nahisi huwa kuna ufisadi unafanyika serikali iliangalie hili by the way sijaja kwa maada hii.
yellow-640x480.jpg

>Pesa ya kusafiria ikiwemo ya kukizi mahitaji mbalimbali ukiwa safarini
Mimi binafsi safari yangu ya kwanza kwenda uganda niliamua kutumia basi from Dar es salaam to Uganda(kampala) nauli ilikuwa kama elfu 90,000/=tu pamoja na chakula njiani.

SAFARI INAANZA YA KWENDA UGANDA.
Safari ilianza alfajiri kutoka ubungo tukitumia bus la kampuni ya TAQWA wakati naingia ndani ya basi nilijua nimepanda na wabongo wengi kwani colour nyeupe zilikuwa chache kwenye siti yangu tangu tunaanza safari nilikuwa nimekaa na dada mmoja hivi wa makamo.
Nilivyokuwa naingia ndani ya bus awali nilijua yule dada ni mbongo kwani nilivyompa hii akauchuna.
Ilikuwa hivi maongezi yetu.
Mimi...Dada mambo
Yeye...Akaitikia kwa kichwa
Mimi..Sikutaka kuhoji sana nikaweka headphone masikioni nikaachana nae nilijua ndo wale wale wa hapa kwetu wenye mashauzi kibao wakati mimi sijaanza safari kwa ajili ya kwenda kutafuta milupo.
Ok fine, safari ikaendelea ila wakati tupo ndani ya safari niligundua wabongo waliokuwemo ndani ya bus wengi wao walikuwa wanawake na baadhi wa nchi tofauti lugha iliyokuwa inatamba ni kiswahili na kiingereza.
Yule dada njia nzima alikuwa anatapika mpaka nikamuonea huruma bahati nzuri nilitembea na dawa za kuzuia kutapika (phenagan) nikampatia akanywa ndio akapata unafuu ndo nikaja kugundua anatokea zambia baada ya yeye kuniongelesha kwa lugha ya malkia na hapo ndo story zilipo anzia.
Tulipofika manyoni tukashuka kuchimba dawa na kupata chakula cha mchana mimi nilichukua keki,biskuti na maji makubwa yule dada alishuka kuchimba dawa na akarudi ndani ya gari nikajua pengine mfukoni hana kitu nikamchukulia juice nikampa.

Tulifika kahama saa tatu usiku tukalala pale siku iliyofuata tukaendelea na safari nakumbuka tulifika bukoba saa 8 mchana tuakapata chakula cha mchana na pale ndio nilitoa pesa yangu iliyokuwa mpesa wakati wakutoa nilisahau kuwa kiwango cha mwisho kutoa pesa kwa siku ni milioni moja hivyo nilivyotaka kutoa tena ikagoma ikabidi niombe msaada wa yule wakala nimurushie yeye milioni nyingine ili atoe yeye nashukuru mungu ikawezekana nikawa na milioni mbili mfukoni.
Siwez kusema uongo wakati naanza safari nilijiona mjanja kwani pesa zilikuwa sehemu salama lakini baada ya kuzitoa nilianza kujiaona mimi fara na hii ilinigharimu kwa sababu sikuwa na MASTER CARD yaani ningeweza kutoa pesa kwenye ATM hata kama ningefika Uganada.
Nakumbuka kuna mdau mmoja aliniambia Uganda Mpesa unapata lakini ni bora ukatolea mpakani au bukoba kwa kupunguza usumbufu lakini pia alinipa tahadhari kutoa pesa kwa mawakala waliopo mpakani ni riski kwani wengi wao huwa wanawachanganyia na pesa bandia na pengine unaweza pewa pesa pungufu kutokana na uharaka wa kuogopa kuachwa na bus.
By the way tulipofika mpakani hapo ndio nilipo badirisha pesa ya bongo kuwa ya uganda nakumbuka kipindi hicho ilikuwa inarange kwenye 1.62... hivyo nilichukua kama milioni tatu na ushee za uganda.
BUSIA.JPG

Mtukula border
Bd-TanzaniaBoarder.JPG.jpg

Kwenye saa 3 usiku tukafika jijini kampala Nyamayiba bus terminal yule dada alikuwa nimwanafunzi wa kampala international university tuliachana kila mtu na njia yake tukaishia kubadilishana contanct.Ila nilichokigundua wanawake wa kibongo ni wapambanaji kwa maana walikuwa wanaongezeka tunapokuwa tunafika kila kituo kila mmoja ukimuuliza anafaata mishe gani uganda anakwambia anamiaka anafanya biashara kutoa uganda kuleta tz.
View attachment 531350
Nyamayiba bus terminal uganda.

Nilivyoshuka tu kwenye bus nikatoka nje ya stendi nikachukua bodaboda kuelekea kampala galaxy guest(hotel) nauli nililipa kama elfu mbili ya kiganda.
Hoteli hii ina mazingira mazuri na pia ipo katikati ya jiji la kampala si hivyo tu wahudumu wake wana kuzungumza kiswahili vizuri.
Kilichonifanya nichukue hii hoteli ingenisaidia kufanya mizunguko yangu na kufika sehemu ambayo nilifikia kwa urahisi ikizingatiwa nihitaji kubeba mizigo hivyo ingeniwia ugumu kama ningechukua hoteli pembeni ya kidogo.

View attachment 531354

View attachment 531355

GALAXY HOTEL
Hapa nililipia shilingi elfu 40,000/=ya kiganda ila pia kulikuwa vyumba vya bei ya juu zaidi binafsi sikutaka kulalachumba cha bei ya juu kwa sababu sikwenda kwa ajili ya starehe bali kusaka mkwanja.
Nilivyofika chumbani nikaoga nikashuka chini kuna resaurant nikapata matoke na kuku nikarudi juu kulala.

Saa kumi tu makelele jiji limepamba moto watu wameshaanza kujichanganya sikutaka kutoka mapema lakini kwenye saa 4 hivi nilianza kutembelea sehemu mbalimbali za masoko,nilianza na na masoko ya nguo pale owino market
DSC01993-700x394.jpg

img_5842.jpg

Owino market,gazaland market,nakasero na sehemu nyingi sana nilizungukia kufanya window shoping ila kitu nilichokingundua waganda wakikugundua mgeni wanakupiga bei kali sana ila ukilia sana wanashuka wanakuuzia bei halisi.
Siku ya kwanza nilizunguka tu sikununua chochote ila kesho yake ndo nikanunua mzigo kama wa million 1 tu then siku iliyofaata nikamalizia.
Siku iliyofaata nikalizungukia jiji kujionea vitu mbalimbali baada ya siku iliyofuaata nikarudi bongo daresalama.
Safari hii nilijifunza mengi sana ila pia ilinitia ujasiri kumbe popote angle ya dunia unaweza kufika endapo utakuwa na pesa.
Hii biashara nimedumu nayo kwa muda flani nikienda nchi tofauti baadae nikaipiga chini baadaa ya mzee jpm kuuanza kukaza uzi TRA wakakaza border
View attachment 531375

NIKAHAMIA KWENYE KILIMO KWANZA

Baada ya mzee magu kuchafua hali ya hewa mtoto wakiume kupitia hapa hapa jf nikapitia nyuzi mbalimbali zinazohusu kilimo nikapata picha nikatafuta mashamba nikaaingia shambani.
Zaidi nilipiga kilimo cha mpunga kwa soko ambalo nilikuwa nimetarget.
13307299_886198228156898_2168499460134548623_n.jpg

Nilipiga kama gunia 78 za mbuga kwa heka 4 siyo kwamba nilikuwa nateleza tu nilipitia changamoto nyingi sana ikiwemo kubadilika kwa hali ya hewa,bei kushuka n.k
12741905_830995667010488_5735067628463887275_n.jpg
10343518_830991670344221_9190998100058749668_n.jpg

3521_830987453677976_8003351208818993418_n.jpg

Mwanaume kazini
12741991_830998967010158_5002817379067077706_n.jpg

12743946_830998873676834_6509049157103976391_n.jpg

Kiufupi nimepata maendeleo mengi na vitu vingi sana vya kunifunza kupitia hapa jf nimeandika
huu uzi ni site na mafundi naezeka kibanda changu cha tatu sasa nikaona nishee na ndugu zangu mambo ambayo yatawatia hasira juu ya maisha na jinsi gani jf inaweza kukusaidia na sikukalia porojo za udaku na siasa ambazo zitatutia uvivu wa kusaka pesa.

View attachment 531298 View attachment 531350 View attachment 531354 View attachment 531355 View attachment 531375 View attachment 531298

Naomba tupeane kila mdau jinsi gani jf imemsaidia hii pia itasaidia wadau wengine kufaaya nyayo za maendeleo
Natamani sana vingi nivielezee ili sote tupeane mwanga juu ya haya maisha.

November nimepanga nisafiri kwenda botswana kunafursa naenda kuichungulia nikifanisha nitaleta mrejesho hapa jamvini ili twende tukawanyanganye tonge wabotswana lengo ni kugawana riziki.
Ukweli ni kwamba jf itabaki kuwa sehemu yangu ya maisha naninawalaani wote wanaotaka jf ifungwe.

Mwenyezi mungu wabariki sana.....
Kilimo kinalipa kuanzia heka 5 chini ya hapo ni hasara
 
Feedback plz
 
Back
Top Bottom