Ushuhuda binafsi: Awamu ya tano niliishi kwa hofu

Sio muumini wa kusoma maandiko marefu lakn nimejitahidi kumaliza.

Siku zote mtu muoga ni mnafiki, mnafiki ni adui wa mkweli, umeishi kwa hofu na utaendelea kuishi kwa hofu sababu ni mnafiki.

Mambo ya watu kufa, kukimbia nchi zao, kuwekwa ndani yameanza hata kabla uhuru na yameendelea kuwepo na yataendelea kuwepo mpaka wanafiki watakapoisha.
Ulikua mnufaika wa mfumo wewe sio bure, hizo zama za uovu kushika hatamu tulikua haturuhusiwi hata kupiga story za nchi yetu kwenye daladala unaweza kujikuta unashuka na pongo kwenda kwa chemba zao
 
Lissu ndio mwanamume pekee aliemuweza dictator Ila asingekimbia baada ya uchaguzi angemsambaratisha. Baada ya kuona usaliti WA kina Ndugai nimeamini Lissu alikuwa anapewa taarifa hata na watu ambao Sisi tuliamini wanamchukia Lissu kumbe hofu ya kuuwawa ilikuwa imewatawala, Walimuadabisha Lissu ili waendelee kupumua. Asante Sana MUNGU.
 
USHUHUDA BINAFSI: AWAMU YA TANO NILIISHI KWA HOFU.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Nikiri wazi kuwa, licha ya kuwa mimi sio mwoga lakini siwezi ongopa kuwa sina hofu au wasiwasi. Hakuna binadamu asiye na mashaka, hofu na wasiwasi, labda kutofautiana kiwango cha hayo.

Moja ya mambo ninayoyapenda kwa kiwango cha juu kabisa basi ni "Kuandika na kusoma" mambo mbalimbali. Tangu nikiwa mtoto mdogo nilipenda sana mambo hayo. Kuandika kwangu ni kama mchezo, kusoma kwangu ni kama starehe. Haiwezi kupita siku pasipo kuandika chochote na kusoma. Ingawaje, nilipokuwa nasoma, nilikuwa sipendi kuanzika Notes za darasani, sio ajabu kunikuta katika adhabu za wanafunzi wasio andika notes kila mara. Hata hivyo nilikuwa na daftari moja kubwa ambalo nilikuwa naandikia somo la Hisabati, Fizikia, Kemia na Biology. Hata hivyo sio lengo langu kueleza haya.

Kama nitaulizwa, nini utakumbuka kwenye awamu ya tano, basi jibu langu ni "HOFU"

Kwangu awamu ya tano ilikuwa awamu iliyoninyima amani. Nilikuwa mtu wa hofu sana. Pengine ukajiuliza hofu hiyo ilisababishwa na nini?

Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa, mimi hobby yangu ni "KUANDIKA" na "KUSOMA" basi kama mnavyojua kitu upendacho kukifanya huwezi kukizuia hata ufanyeje kwani kukizuia ni kuyafanya maisha kuwa magumu. Nilikuwa naandika makala za hapa na pal, zipo za kijamii, kiuchumi, kisiasa, riwaya, mashairi, na maandiko ya kitoto, yakizee, maandiko ya kusadikika basi ilimradi akilli yangu itakavyonituma.

Katika maandiko yangu mara nyingi nalenga kuijenga jamii, kuifundisha na kuielimisha. Kuikosoa, kuikemea na kuiburudisha. Mara zingine naandika bila dhamiri, naandika kwa vile roho yangu inataka niandike tuu yale yote yaliyomo akilini mwangu. Hivyo ndivyo nilivyo, na hiyo ndio furaha yangu.

Sasa kasheshe linakujaga pale ninapoandika makala za kisiasa hasa zenye maudhui ya kukemea, kukosoa na kuonya. Hapa ndipo kulinifanya niishi kwa hofu na kwa tahadhari kubwa sana.

Hofu yangu haikutoka ndani bali ilitoka nje kutoka katika sehemu zifuatazo;

1. Watu wanaonizunguka
Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki walikuwa wakiniambia niache kuandika mambo ya kisiasa, hasa yenye lengo la kukosoa, na kuwaonya wakubwa. Nakumba Mama yangu alinipigia simu akanikanya sana, na kunikemea, tuligombana sana, nikijaribu kumwambia asinifundishe kuwaogopa waovu, akaniambia kwa sauti ya kukata tamaa, akasema " Shauri yako hutatimiza ndoto yako" Mimi nikamjibu ndoto yangu ni kuona jamii yangu inaishi kwa haki na uhuru. Basi Mama yangu akasema amenawa mikono na kamwe hataongea na mimi tena kwa habari hizo.

Sisemi sikumuelewa mama yangu, nilimuelewa sana, alikuwa hataki nikutwe na madhila kama yaliyokuwa yanatokea, alionyesha upendo kama Mama. Mama yangu Mkubwa naye mara zote tuliingia kwenye migogoro ya namna hiyo hiyo, nilijaribu kumueleza lakini hakuweza kunielewa kama mimi nilivyoshindwa kumuelewa. Mjomba wangu mmoja naye kwa kujali alinipigia simu siku moja usiku wa manane, nilishangaa simu yake kwani hatukuwa na ukaribu wa kupigiana simu. Hivyo kuiona simu yake usiku ule ilinipa wasiwasi. Yeye naye alinisihi niachane na mambo hayo kwani ni hatari kwangu, aliongea kwa kilugha nafikiri ili nimuelewe vizuri kabisa.

Bibi yangu aliyenilea naye hakuwa nyuma, aliniambia niachane na hayo kwani maisha yangu yatakuwa mafupi, nakumbuka nilimjibu na kumuambia hivi " Bibi ni ipi faida uliyoipata kuishi miaka mingi na ipi hasara ya mtu aliyezaliwa akaishi siku moja?" Bibi hapo alipata kigugumizi. Nilijadiliana sana na Bibi yangu, hakutaka kunielewa.

Mchumba wangu naye hakuwa nyuma mara kwa mara alikuwa akinisihi nisiandike mambo hayo, kwani hataki kuniona katika hatari. Nilimuelewesha akanielewa kishingo upande. Marafiki zangu pia wanaonijua na wasionijua kwa sura(ana kwa ana) nao walinitisha na kunitia hofu..

2. MATUKIO YALIYOKUWA YAKIENDELEA
Baadhi ya matukio kama vile mauaji, utekaji na kutiwa korokoroni kwa baadhi ya wakosoaji nako kulikuwa sehemu ya kunitia hofu katika awamu ya tano. Hata hivyo kila tukio lililokuwa likitokea lazima awepo mtu wa kuniambia; unaona mwenzako, bado wewe. Yaani hiyo ilikuwa ni lazima.

Jambo moja ni kuwa mimi nilichokuwa najaribu kukieleza ndani ya jamii yangu ni kuamsha ari na ujasiri wa kukemea waovu, nilikuwa nahamasisha vijana wasioogope waovu hata kama wangekuwa na nguvu kiasi gani. Jambo moja nililowaambia watu wanitishiapo lilikuwa; sifundishwi kumheshimu na kumuogopa Muovu.

Hata hivyo nilikuwa mtu wa tahadhari, na kama nitakuwa mbali na nyumbani basi nilichunga mienendo yangu na wanaonizunguka, sikuweza kukaa chumbani pasipo kufunga mlango, sikuweza kufungua mlango unaobishwa pasipokusikia sauti ya mtu anayebisha. Sisemi tahadhari hizo zilinisaidia au zingeisaidia hashaa! nilifanya hayo kuepukana kukamatwa kizembe.

MAMBO NILIYOJIFUNZA KIPINDI HICHO;

1. Maovu yanazidi kwenye jamii kwa sababu ya watu wanaogopa kukemea waovu

2. Watu wa karibu wakiwemo wazazi , ndugu na marafiki ndio huwa waalimu wakuu wakufundisha watu uoga wa kumuogopa muovu. Hii ni kutokana na kukupenda na kuona usumbufu unaoweza kukupata na kuwapata

3. Uovu ukizoeleka unakuwa utamaduni ndani ya jamii kiasi kwamba waovu hutukuzwa na kupewa sifa au kujipa sifa

4. Hakuna mtu mwema anayenyamaza aonapo maovu, isipokuwa wanafiki

5. Waovu hutumia mbinu ya kuzima wasema ukweli ili kuhalalisha uovu wao uonekane ni wema

6. Uovu ukishatamalaki, akili ya jamii huwa yakiovu, waovu husifiwa na wenye haki hupondwa.

7. Kutokana na waovu kupenda kamera na kutenda wema mbele ya media, jamii ni hujikuta ikiwaona ni watu wema kumbe ni wabaya.

8. Uovu haufichiki kama vile ulivyo wema. Waovu hutumia nguvu kubwa kuficha ubaya wao, ila kadiri wanavyouficha ndivyo wanavyouibua uovu wao mwingine

9. Hata waovu hufa, tena hufa kabla ya wakati wao.

10. Muovu hana uhuru, kwani uhuru upo hivi; ukiuzuia nao unakuzuia, ukiuachia nao unakuachia. Waovu huzuia uhuru na kujikuta kumbe nao hawapo huru kupitia kuficha uhuru.

11. Muovu hawezi kuwa huru hata siku akifa, bado ataishi kama mtumwa huko aendako

Nilishawahi kusema na kila siku nasema; Taikon atakuheshimu na kukuogopa ukitenda haki na kufuata sheria za Mungu. Lakini kamwe dunia ingalipo, Taikon hataogopa mtu muovu hata angekuwa ni nani. Taikon haogopeshwi na elimu ya mtu, kazi ya mtu, cheo cha mtu, uzuri wa mtu au mamlaka. Ukitenda wema nitakupongeza, ukitenda mabaya nitakukemea na kukuonya, ukiwa na kiburi shauri yako.

Tuishi kwa upendo, upendo ndio utatufanya tuishi milele.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Iringa Mjini
Nimeipenda hii

"Uovu ukizoeleka unakuwa utamaduni ndani ya jamii kiasi kwamba waovu hutukuzwa na kupewa sifa au kujipa sifa,,,,,"
 
Nimependa hizi point zako

Jomba umetishananukuu point zako 6-10
 
Jomba umetisha!
Nanukuu point zako 6-10

Uovu ukizoeleka unakuwa utamaduni ndani ya jamii kiasi kwamba waovu hutukuzwa na kupewa sifa au kujipa sifa,,,,,

Hiyo palagraph inaelezea hali halisi kabisa ambayo ilikuwepo kabla jiwe hajatwaliwa,,ashukuriwe Mungu mkuu kwa kusikia kilio chetu.
Mungu ametusaidia sn tena sana
 
Kwa nini uliamua kuandika ukiwa umeweka majina yako na namba zako za simu wazi kabisa?

Uliwahi kupigiwa simu na watu wasiojulikana kukutisha?
 
Itoshe tu kusema kuanzia 2015-2021 nchi yetu ilikuwa na Wanaume wawili tu,waliotunishiana misuli kwelikweli.Hawa ni JM(mfalme Juha) na mwanasheria msomi TUNDU ANTIPASS LISSU,nadhani mshindi ametangazwa.
Dunia inachukua walio dhaifu.
Tabia uipendayo Sana ndiyo itakayokuua.
Ni kweli kabisa hao majamaa wawili ndo waliokuwa wakitunishiana misuli lakini Mungu kaamua kumtangaza mshindi..
 
ww jamaa huwa unapepea na uelekeo wa upepo

ulikuwa chawa wa karibu wa shujaa na bashite na magenge yao...

uliweka thread kadhaa za kumuabudu na kumsifu
Hapana,huyu Bw Robert hakuwa chawa. Nimeangalia post zake za zamani,jamaa anatosha! Namnukuu hapa chini

MUNGU AMEMPA KURA LISU, JE WEWE UTAMPA NANI?

Na, Robert Heriel

Hata Mungu hufanya uchaguzi, Hata Mungu hupiga kura. Sio mwanadamu peke yake apigaye kura, hata Mungu Muumba wa Mbingu na ardhi hupiga kura.

Katika Historia ya Biblia wapo watu kadhaa waliopigiwa kura na Mungu miongoni mwao ni hawa hapa;

1. Daudi mwana wa Yese
2. Yakobo mwana wa Isaka
3. Yusuph mwana wa Yakobo ndiye Israel
4. Suleiman mwana wa Daudi
5. Yesu mwana wa Maria
6. Yeremia Mwana wa Hilikia
7. Muhamad mwana wa Abdullah
8. Musa kutoka Kabila la Lawi Miongoni mwa wateule wengine.

Wapigiwa kura karibu wote au tuseme zaidi ya 99% ya waliochaguliwa na Mungu walikuwa na sifa zifuatazo;

1. Hawakutoka katika familia kubwa zenye utajiri. Karibu wote wametokea familia masikini au za kawaida
2. Wote walikuwa na ujasiri unaofanana wa kutetea haki
3. Karibia wote walikimbia uhamishoni
4. Karibia wote walinusurika kuuawa, na wapo waliouawa kabisa. Waliozeeka walikuwa wachache pia
5. Wote walipata kura chache kutoka kwa wanadamu wenzao, walikataliwa, ila walipata kura ya Mungu.
6. Karibu wote waligombana na serikali zilizokuwa madarakani kwa wakati wao. Na sifa zingine.

Mfalme Daudi hakupigiwa kura na wanadamu, au ndugu zake. Kisa kinaanzia pale Nabii Samweli anatumwa akampake mafuta Mfalme mpya wakati tayari yupo Mfalme Sauli anatawala. Nabii Samweli anamuwekea ubishi Mungu kwa kuogopa kuuawa na Mfalme Sauli mara atakaposikia kuwa yeye kaenda kumpaka mafuta mfalme mwingine. Hapa tunaweza kusema Nabii Samweli anaogopa kupindua serikali ya kifalme ya Sauli(Hata sasa ni kosa la jina kupindua serikali "UHAINI" na hukumu yake ni kifo) Basi tunaweza kusema Nabii Samweli alikuwa anahaki ya kukataa wito wa Mungu wa kwenda kumpaka mafuta Mfalme mpya Mfalme Sauli yungali hai.

Mungu anamshawishi Nabii Samweli kwa kumwambia kuwa Roho yake imehama kutoka kwa Mfalme Sauli kutokana na Maovu ayafanyayo. Basi Nabii Samweli akakubali wito wa Mungu wa kufanya kosa la Uhaini(kupindua serikali ya Sauli) huku akijua madhara yanayoweza kumpata.

Nabii Samweli anateremkia Bethlehemu huko aishipo Mzee Yese, ndiye huyo Baba wa watoto wakiume Nane Daudi akiwa mmoja wapo kama mtoto wa mwisho. Samweli alipoona watoto wakubwa wa Yese akiwepo ELIABU na ABINADABU moyo wake ukawachagua hao, hata Yese mwenyewe ambaye ni Baba alijua kuwa watoto wake wakubwa ndio watapata hiyo Bahati ya kupakwa mafuta ili baadaye mfalme atoke kutoka kwao. Lakini Kura ya Mungu haikuwa juu yao. Mungu akasema; Yeye aangalii sura au urefu wa mwili bali anaangalia Moyo.

Basi Daudi akaenda kuitwa kwani hakuwepo bali alikuwa akichunga mifugo huko porini. Alipofika tuu, Mungu akamuambia Nabii Samweli, mpake huyo Mafuta. Huyo ndiye atakuwa Mfalme.

Kumbuka, hata Mfalme Sauli alipakwa mafuta na alichaguliwa na Mungu lakini baadaye alikuja kuzingua, na ndio maana Kura ya Mungu ikahama kutoka kwake kwenda kwa Daudi.

Daudi anakuja kwenye utawala baada ya kumuua Goliath au Jaluti, kisha anakoswa koswa kuuawa na Mfalme Sauli, lakini Bado Mungu anakuwa juu yake.

Kisa cha Daudi ni moja ya visa vinavyoweza kumpa mtu maarifa na uzoefu wa mambo ya kisiasa na kiutawala.

Katika kisa hiko tunaona kuwa, Kura ya Mungu ilikuwa kwa Daudi na ndio maana Mfalme Sauli alishindwa, ingawaje naye alipewa kura zamani ndio maana akawa Mfalme.

Kisa cha Pili ni Kisa cha Suleiman mwana wa Daudi ambaye tumeona kwa ufupi kisa chake.

Baada ya Mfalme Daudi kuzeeka, kifo ndio ilikuwa jawabu. Kikawaida mtoto wa kwanza ndiye hurithi ufalme kwa Desturi ya kizamani mtoto wa kwanza ndiye alikuwa anarithi kiti cha Ufalme, Mtoto wa kwanza wa Daudi aliitwa Amnoni mama yake aliitwa Ahinoamu; Huyu aliuawa na Absalomu ambaye ni mtoto wa tatu wa Daudi kwa kosa la kumbaka Tamari(Dada yake Absalomu), Mtoto wa Pili aliitwa KILEABU, mama yake aliitwa Abigaeli, huyu naye alikufa. Mtoto wa tatu alikuwa ni Absalomu kwa mama aitwaye Maaka, huyu naye alikufa alipokuwa akipigana na Daudi Babaye ili ampoke ufalme.

Mtoto aliyefuatia ambaye mpaka Mfalme Daudi anazeeka na ndiye angepaswa achukue ufalme aliitwa Adoniya mama yake aliitwa Hagithi. Huyu kabla Mfalme Daudi hajafa ndiye alipaswa arithi kiti cha Ufalme kwa taratibu za kizamani. Na ndio maana Adoniya alipoona haoni dalili ya kupewa ufalme akaanza harakati za kuchukua ufalme.

Lakini Mungu alikuwa hajamchagua Adoniya Bali kura yake ilikuwa juu ya Suleiman ambaye Mama yake aliitwa Bathsheba, Solomoni au suleiman ni jina lililotungwa na Daudi, lakini Mungu alimpa jina liitwalo YEDIDIA yaani "Kwa ajili ya Mungu" kwa kinywa na Nabii Nathani.

Suleiman akatawazwa kuwa Mfalme kwa sababu alipewa kura na Mungu.

Tuishia hapo kwenye hiyo mifano miwili.

Kutawala kwa Mhe. Magufuli ndani ya nchi yetu, nako siwezi kuwa mnafiki kuwa mwaka 2015 kura ya Mungu ilikuwa kwa Mhe. Magufuli. Hata ukiangalia mazingira ya utokeaji wa Magufuli akiwa na visiki vya mpingo viwili ambavyo ni Mzee Edward Lowasa na Mzee Bernard Membe. Kwa hali ya kawaida hakuna aliyekuwa anamfikiria Magufuli atatawala nchi hii. Lakini Kura ya Mungu ilikuwa juu yake mwaka 2015. Magufuli hakuwa chochote mbele ya watu waliodhaniwa kuutwaa urais. Lakini Magufuli alikuwa chochote mbele za Mungu.

Lakini mwaka 2020. Mambo yamebadilika, Magufuli ameshindwa kulinda Kura ya Mungu juu yake kwa kushindwa kutetea baadhi ya haki za kuishi kwa Watanzania. Kitendo cha uwepo wa Mauaji na utekaji uliofanyika miaka hii mitano na hakuna hatua zilizochukuliwa zimeondoa kura ya Mungu kwa Magufuli. Kitendo cha Magufuli kushindwa kusimamia uhuru kwa vyama vyote kimeondoa kura ya Mungu juu yake.

Magufuli angekuwa Rais Bora kama mambo hayo mawili yangefanyika kwa usahihi. Na kura ya Mungu ingekuwa juu yake. Wala asingetumia nguvu nyingi kuomba kura awamu hii.

Na hata Huyu Lisu asingekuwa chochote kwenye uchaguzi huu. Lakini Kura ya Mungu imehama kwa Lisu na ndio maana utamuona Lisu hana nguvu yoyote yeye kama yeye lakini anapaka nguvu kwa kadiri Muda unavyoenda.

Naamini, Maandiko yangu mengi yanasomwa na watu wengi, yanasomwa na viongozi wengi,

Yeyote apataye Nafasi ya Urais, iwe Tundu Lisu, iwe Mhe. John Pombe Magufuli Lindeni kura ya Mungu kwa kujali na kutetea yafuatayo;

1. Haki za watu, ikiwepo haki ya kuishi. Haiwezekani mtu afe au apotee kama mnyama alafu serikali ikae kimya. Hakuna Mungu atakayefurahia utawala wa namna hiyo.

2. Kutetea nchi na wananchi
Tunataka Rais atakayetetea wananchi na nchi. Kila mwananchi ni muhimu kwa taifa hili. Hakuna aliyezaidi ya mwingine. Rais lazima ahamasishe umoja na heshima kwa kila mtu. Rais atakayetetea maslahi ya wananchi na rasilimali zake.

3. Atakayetambua Uongozi ni dhamana, asitumie kama nyenzo ya kuumiza wengine.
Tunataka Rais ambaye hatajifanya mungu mtu. Tunataka Rais ambaye atakubali kupongezwa na kukosolewa. Rais wa hivi lazima atakuwa mnyenyekevu

4. Mwenye hukumu zenye haki(asiwe Double Standard)
Tunataka Rais ambaye hatakuwa na mawe mawili ya kupimia. Huyo hatatenda haki, asihukumu kwa kubagua watu, au asitoe maendeleo kwa makundi ya watu bali apende nchi na wananchi wake wote. Iwe ni CCM au CHADEMA, iwe ni Mhaya au Mkaguru, iwe ni Mkristo au Muislamu. Wote wahukumiwe kwa haki pasi na hila

5. Atakayeleta maendeleo
Maendeleo yasiwe chanzo cha kuharibu haki na utu wa watu. Na ndio maana nimeiweka hii kama sababu ya tano na sio ya kwanza. Mwanadamu baada ya uhai kitu cha pili ni uhuru, uhuru huletwa na haki, haki huleta amani, amani ndio huzaa maendeleo.
Tunataka Rais atakayeweza kutuletea maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kifikra.

Mpaka sasa, Kura ya Mungu ipo na Tundu Lisu, hata kama wananchi hawatampa kura Lisu za kutosha kumfanya Tundu Lisu awe Rais, basi hii itamfanya MAGUFULI kama anahekima kujifunza mambo mengi ambayo naamini yatambadilisha kwa sehemu Kubwa.

Magufuli endapo utashika nafasi ya pili, jitahidi utumie nafasi hiyo kama njia ya kujisafisha mbele za Mungu, muombe Mungu msamaha kwa kushindwa mambo niliyoyataja hapo juu. Naamini unaelewa ninachokisema; usijejifanya kiburi kwa maana unafahamu fika umri ulionao kwa sasa ni mkubwa, ni umri wa kufanya matengenezo, umri wa kutubu. Umri wa kumaliza na Mungu.

Lakini ukijifanya jeuri ukatenda kwa kiburi basi fanya zaidi na zaidi kwa kadiri ya jeuri yako itakavyo kutuma. Lakini ukae ukijua hauna muda tena, nawe sasa ni mtu mzima.

Nawe Lisu, kama utapata kibali cha kuongoza nchi hii, Usije kutenda kwa hila, wala usijelipa kisasi, kwa maana kisasi hufanywa na waovu, bali muachie Mungu ndiye ajuaye.

Magufuli usijekuwa kama Mfalme Sauli alipokataa kuachia Ufalme kwa Daudi, akasahau hata yeye aliwekwa na Mungu na sasa huyo huyo aliyemweka ndiye anataka kumuengua. Kama utashindwa kihalali, muachie Lisu atawale. Nawe utakuwa kama Musa alivyolilia kufika Kanani lakini Mungu akakataa, akamuachia Joshua.

Lissu anaweza kuwa Joshua wa Magufuli. Lissu anaweza kuwa Daudi, na Magufuli akawa kama Sauli.

Nawe Lisu kama utapata nafasi ya kutawala uwe kama Mfalme Daudi, ambaye baada ya kuchukua Ufalme hakutaka kumlipa kisasi Mfalme Sauli aliyetaka kumuua.

Jamani andiko hili limekuwa refu sana, hata hivyo nimelifupisha mno, kwani yapo mengi niliyotaka kuyasema.

Kwa habari ya kura yangu, nitampa Tundu Lisu, lakini hata kama akishindwa sitamchukia Magufuli, nitamsapoti kwa yaliyo mema na nitampinga kwa mabaya. Hata Lisu naye kama atapata utawala nitamuunga kwa mema lakini kwa mabaya sitomnyamazia asilani.

Itoshe kusema; Tupendane, kwa maana wote wapendanao ni watoto wa Mungu.

Ulikuwa nami:

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Ila Mungu fundi kweli kweli,tulishakubali kuwa chini ya dhalim hadi 2025,kwa huruma zake katuepusha na huu mkono wa chuma bila kumwaga hata tone moja la damu. Asante Mungu.
 
Jiwe Kama jiwe..Kuna watu Ni hatari Sana..nikimkumbuka been saanane..kijana smart Sana..mwandishi mzuri Sana Kama Malisa..
Never never again!
 
Back
Top Bottom