Linamo
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 9,976
- 24,494
Habari Jf.
Tarehe 11/2/2013 niliwahi kuandika hapa kuhusu tatizo langu la kutopata mtoto kwa muda mrefu. Wengi mliguswa na tatizo langu na mlijitoa kunishauri na kuniagizia kwa madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na wengine mlijitolea kuniombea kila mmoja kwa imani yake.
Tarehe 14/8/2013 nilirudi tena hapa kwa tatizo hili hili tena kwa awamu hii ya pili nikiwa nimekata tamaa kabisa,lakini bado mlionekana kuwa pamoja na mimi kwa kunifariji hamkukata tamaa bado mliniagizia sehemu mbalimbali za kuweza kutatua tatizo langu. Hii ilikuwa faraja kwangu na nikiri iliendelea kunipa nguvu.
Niliendelea kuhangaika kwa madktari bingwa wa magonjwa ya wanawake. Regency,Muhimbili, KCMC na sehemu nyingine nyingi nilizoagiziwa. Sehemu zote hizo niliambiwa sina tatizo. Nilisafisha mpaka mirija ya uzazi lakini bado hali ilibaki vilevile.
Nikiwa nimekata tamaa kabisa baada ya kuhangaika pasi mafanikio tarehe 10/ 5 /2016 niliumwa ghafla nikaenda hospital wakaniambia ni malaria nikapewa dawa nikatumia. Lakini nikaendelea kuumwa nakarudi hospital baada ya kufanya vipimo nikaambiwa ni Mjamzito kwa kweli sikuamini hata kidogo nilihisi labda ni masihara lakini ulikuwa kweli.
Kipindi chote cha ujauzito hakikuwa kizuri kwangu niliumwa Sana niliishiwa damu kupelekea kulazwa kwa muda mrefu Sana. Hakika Mungu ni mwema na anatenda kwa wakati wake tena katika kipindi tulichokata tamaa kabisa.
Tarehe 14/12/2016 nilifanikiwa kupata mtoto wa kiume.Japo nilijifungua kwa tabu Sana lakini Leo naitwa MAMA hakuna linaloshindikana Maombi ni suluhisho la matatizo yetu.
Nawashukuru Sana kwa ushauri na maombi yenu. Hakika tumelifanikisha hili.
Hope is the only thing stronger than Fear!!!