Ushoga Tanzania: 1500 wajitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia Moja Iringa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Kukithiri kwa biashara haramu ya ngono pamoja na tabia ya ushoga mkoani Iringa kunadaiwa kusababishwa na baadhi ya vijana wa vyuo vikuu waonafika mkoani humo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu, huku miongoni mwao wakitaka starehe zilizo nje ya uwezo wao.

Tamaa ya kumiliki vitu vya thamani – ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwahadaa baadhi ya wasomi hao wa vyuo vikuu, jambo linalosababisha wengi wao kuangukia katika wimbi la biashara ya ngono na ushoga na kuufanya ongezeko la maambukzi ya vvu.

Kwa mkoa wa Iringa inadaiwa kuwa zaidi ya mashoga 1500 wamejitangaza wenyewe kuendesha biashara haramu ya ngono, jambo ambalo kiafya linadaiwa kuwa ni hatari kwa maambukizi ya virus vya ukimwi.

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa ndiyo wanaonyooshewa kidole kuhusika na biashara hiyo ya ngono na tabia ya ushoga- ambapo shirika la restless development linalojihusisha na masuala ya afya ya uzazi na makuzi kwa vijana- kupitia mradi wa dance for life- limewakutanisha viongozi hawa wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa- ili kujadili namna ya kujinasua katika wimbi hilo la ushoga na biashara haramu ya ngono.

Serikali inaona tatizo hilo la ushoga na biashara ya ngono litamalizwa na jamii yenyewe, endapo tu wazazi na walezi watakemea mapema mienendo hatarishi ya vijana wao.

Ushoga ni tabia inayofanywa na baadhi ya wanaume, kwa kujihusisha kimapenzi na wanaume wenzao, suala ambalo kwa kiwango kikubwa linatajwa kuchochewa na mambo ya utandawazi, ambao unaibua mitindo mbalimbali na tabia mpya kila uchwao.

Chanzo: Star tv
 
Last edited by a moderator:

hiyo ni Iringa mji mdogo, je miji mikubwa si ndio itakuwa na idadi kubwa?
 
Yani 0713 zinafumuliwa na kusambaratishwa yan hiki kizazi sodoma ni cha mtoto
 
Hili suala la ushoga ifikie kipindi serikali itangaze kuwa Janga la taifa. Watoto wadogo mashoga wamejaa badoo wanajinadi hadharani kabisa. Kwa mji kama Dar es salaam ni almost kila mtaa una kijana shoga. Tena vijana wadogo kweli huwezi amini.

Mungu atunusuru
 
Hata Njombe wapo wengi tu, kuna shirika lilifanya research na kuwatafuta hhao watu via radio na walijitokeza wazi kibao.
 
Sababu siyo iringa ndogo juwa sababu wazawa wale ni starehee sana?? Na ulevi sana na maambukizi mengi sana'hiyo iringa haijawahi kushuka maambuukizi ya vvu
 
Back
Top Bottom