Dola Iddy Wa Chelsea
JF-Expert Member
- Sep 26, 2014
- 2,120
- 1,510
Wakati nipo nyunbani hapa karibu na Makoye lodge nikiwa zangu naweka oil kwenye pikipiki yangu ghafla nikashuhudia ugomvi mkubwa maeneo ya Makoye lodge.
Nikajaribu kujisogeza ili kupata mawili matatu juu ya nini kinachoendelea aisee kijana wa miaka 20s amekamatwa na baba yake kwa madai ameiba kiasi cha laki 3 jana usiku kutoka kwa baba yake mzazi na kwenda kuchukua chumba Makoye lodge ambapo ndipo alipokamatiwa na mzazi wake.
Ila kabla hajamdhibitiwa alimshambulia baba yake mzazi kwa mateke hadharani mbele ya umati wa watu ila baada ya muda raia walimdhibiti kwa kumfunga kamba na kumpeleka kituo cha polisi Ushirombo.
Pia kipindi baba yake anampekua kijana wake mifukoni mwa suruali alimkuta na kisu cha kukunja, pochi na fedha kiasi.
Kutokana na tukio hili je laiti kama wewe ndio ungekuwa baba mzazi wa kijana huyo utachukua hatua gani dhidi ya kijana wako?