Ushirikina (Ujinga) karne hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushirikina (Ujinga) karne hii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DoubleOSeven, Feb 3, 2011.

 1. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ukichanganya simulizi za miujiza ya kina Shehe Hayahaya na mineno inayosemwa kama Mlingotini, zana za ushirikina kama viungo vya albino, viungo mbalimbali vya watu wa jinsia zote, ngozi ya binadamu na wiki hii, VIUNGO vya watoto njiti na maiti za vichanga unaweza kupaka picha moja chafu kwelikweli kuhusu UJINGA ULIVYOKITHIRI katika jamii ya Watanzania.

  Licha ya simulizi nyingine zinazohusu misululu ya viongozi mabalimbali kushinda kwa waganga kuna visa vingine vinavyoashiria upumbavu wa hali ya juu. Nakumbuka kile cha vijana wa KIMERU walivyohamasika kumshughulikia punda jike waliyemkata miguu huko wakiamini ni njia mkato ya kupata utajiri wa madini kule Merelani. Kafara zinazotolewa migodini ndio basi tena.

  Leo hii wapo Vigogo wengi ambao ukienda kwao utakaowakuta humo ni pamoja na wataalamu wa kupulizia. Naambiwa wapo wa ku-charge battery za hirizi, pete na ushenzi mwingine wajuao wao.

  Sijui ni percentage ngapi ya Watanzania walobaki katika UJINGA unaohusishwa na hizi imani katika karne hii.

  Nasikitika sana kwamba katika karne hii, miaka 50 baada ya uhuru, nchi yetu inazidi kujizindika kwenye ujinga na umaskini hapo hapo licha ya kuwa na hazina kubwa za aina mbalimbali na watu wengi tu wenye uwezo.
  UJINGA uliobobewa Tanzania ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Nini kifanyike?
   
 2. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu
   
 3. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kila Mtanzania ana haki ya kuamini na kuabudu kile anachokiona kinamfaa.
  So kwa wewe ambaye unaingia Kanisani au kuingia Msikitini usijione bora kuliko wale wanaokwenda makaburini ama kwenye mapango ama kwenye miti mikubwa na kuabudu.
  Au wale wanaotoa kafara kwenye migodi.

  Wewe hiyo imani unayoipigia chapuo hapa na ambayo unaiona ndio baab kubwa kwa taarifa yako uliletewa na mkoloni.
  Na ulivyomjinga umeikumbatia na kuitukuza na kuisahau na kuiponda ile imani yako waliyokuwa nayo babu zako kabla ya ukoloni kuja.

  Leo hii kuna watu wanaamini Jua, kuna watu wanaamini Bahari, kuna watu wanaamini Nyota nk nk nk nk
  Lakini wewe kwa ufinyo wako wa Fikra utawaita wale ni washirikina na wachawi...

  So jifunze kuheshimu imani za watu kama ambavyo wenzako wanavyokuheshimu wewe na imani yako hiyo uliyoletewa na mkoloni na kisha kuitupilia mbali imani yako ya asili....
   
 4. D

  Donell Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Yaani ni kweli kabisa, na ndio maana tunaendelea kuwa masikini.Taifa gani litaendelea kwa kuamini imani za kishirikina? Kuanzia Viongozi mpaka wananchi wa kawaida wote ushirikina.Taifa hilo litazidi kuwa masikini milele na milele kwa sababu Mungu ameshalipa kisogo na hatutapata neema ya Mungu.Mpaka tubadilike ndio tutaona maendeleo ya kweli lakini kama tutaendelea hivihivi hatufanyi vitu mpaka ukacheck "jamaa" walai hatutaendelea.
   
 5. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... yapo mazuri katika imani za asili na ya kijinga mno, what i am going to refer to as being profound ignorance... katika imani hizohizo. Yale ya kijinga, ya kishirikina hayafai na yataendelea kupumbaza. Hivi kweli jitu zima unaweza amini...safari za ungo into outer space !!!... basi nakumbukia zama za Sputnik na Yuri Gagarin katika competition hiyo.

  Mtu mjinga hata mafundisho ya dini hataweza kuyaelewa. Kwa uwezo gani?
   
 6. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mkoloni amefanikiwa alichokitaka...
   
 7. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Labda uulize ni percentage ngapi ya Watanzania ambao hawajihusishi na ujinga huu! Haijalishi kiwango cha elimu wala status ya maisha, wengi wetu tumejikuta tunaishi maisha ya aina mbili; kwanza yale ya wazi ya usomi na 'uzungu' kisha yale ya gizani kwenda kwa 'mafundi' kukutengenezea mambo yako. Iwe maofisini au kwenye biashara hakuna eneo utawakosa wanaotegemea ushirikina 'kuimarisha' nafasi zao.

  Kama mnaamini uchawi unafanyakazi basi tusaidieni tuwaloge MAFISADI wanaotafuna taifa letu!
   
 8. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Na nyote mnaoamini ktk huo uzungu tusaidieni pia kuwamaliza hao mafisadi wanaolimaliza Taifa hili.
   
 9. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  kama kuabudu imani za asili ya Mtanzania ni ushirikina basi napenda kujitangaza hadharani kuwa mimi ni Mshirikina nambari moja.

  Ila Hasilani abadani ukoloni hautosha kwa kuwa baadhi ya watu wameukumbatia uzungu na kusahau asili zao.
   
 10. U

  Ulimali Member

  #10
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hiki ndicho kinachotuponza Watanzania kuwa masikini kwa kuelemea nguvu za giza. Viongozi wengi wa nchi yetu wameifanya nchi kuwa ya laana baada ya kuacha kutegemea Mungu wa kweli na kujishirikisha na shetani(ushirikina). Amini usiamini viongozi wengi wa Tanzania hasa wanaopendelea kuva yale mapete ni washirika wakubwa wa majini na ushetani. kiongozi wa nanma hiyo huleta laana kwenye nchi ni bora mapagani kuliko huyu anayeshirikiana na ibilisi direct kwa sababu mungu hashirikiani na shetani. Wakati wa uchaguzi usombe mlingotini wanavyofukuzana. Lakini pia waelewe mwisho wao huwa mbaya kabisa.
   
 11. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... Asante mkuu. Inawezekana sana ukaambiwa ati MAFISADI hawalogeki kwani timu zao za ufundi ni kali zaidi. Nguvu ya vijisenti na utaalamu at par!

  Nategemea aje mtu na hoja hapa ya aina hii.... ultimately, yanayotokea nje ya Tanzania katika nyanja zote yanatuhusu pia. Tanzania sio kisiwa. Changanya na challenges za kuwemo ndani ya globalized village, tutake au tusitake, mojawapo ya factors za kuwa-marginalized ni pamoja na kuendeleza IGNORANCE kwa ukataa maendeleo yanayohitajika kifikra na watu kujikomboa from UJINGA na mengineyo stahili.

  Leo hii Tanzania inaelekea kuwa a failed state. UJINGA umechangia sana katika hilo. impact ya KUKUMBATIA UJINGA ni kubwa mno. Mataifa mengine duniani walikuwa katika UJINGA huo karne kibao zilizopita.

  Mila potofu na imani za aina ile ya kwa mbuyu hazina cha ziada ila mitambiko tu. Jana nimesoma pahala kwamba jamaa wamegundua planets kibao kwenye outer space. Television za toboatobo inabidi sasa ziwe digital.
   
 12. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ina maana dini zinazo promote moral values ni sawa na huo upupu wa waganga?

  Mwenzetu utakuwa una matatizo kama una support huo upumbavu. Hawa waganga ni chanzo cha kuvuruga social cohesion and corrupting social moral. Mbali na hayo aliyoyasema bwana mkubwa waganga ni waongo na wachochezi. Wagombanishaji wa familia na jamii kwa jinsi wanavyo wapa watu unnecessary irrational thoughts.

  Matokeo yake watu kuwa na fikra za ajabu na ukatili ndani ya jamii kisa ushauri wa mganga lini umeona mchungaji au shekhe anasema tukate viuongo vya watu kwa utajiri.

  Kuna dini nyingine zinafanya ibada kiajabu ajabu kama kwenda kucheza ngoma za kuomba mvua, lakini kuchinja watu kwa ajili ya mvua si sawa.

  Waganga lazima wadhibitiwe kwa kweli enough is enough its time we reduce the irrational thoughts in the social ambazo chanzo ni waganga (wachomwe moto tu).
   
 13. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hivi kwa nini masharti ya ushirikina always ni magumu na yakikatili.......kwa nini siku moja sharti lisiwe, nenda kale korosho? au sharti mkonyeze demu bomba? au sharti imba ule wimbo wa ABCD?
   
 14. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ah,nimesoma thread yako,ila ambacho siku-grasp vizuri ni kama unaamini ushirikina ni kitu hewa.Let me tell you,wewe ndiye ambaye uko mbali sana na uhalisia wa mambo.Kama hujui wazungu waliotuletea what we wrongly call education(hapa nina hakika hutanielewa) ndio washirikina wa kutupwa.In fact they are about to announce that technologies nyingi tunazotumia zina ushirikina ndani yake!Nadhani siku hiyo mlango wa kutokea utautafuta.Ni hivi, kama unaamini Mungu yupo,lazima uamini pia kwamba shetani yupo.that is what the Bible teaches me.Na kama shetani yupo basi no doubt about it ushirikina upo!Waliotu-braiwash mpaka tukaamini hakuna uchawi ni Wazungu.Walikuwa na sababu zao.Let me remind you kwamba uchawi tunaukataa on grounds of religion only,ni kinyume cha mapenzi ya Mungu, but it's real.
   
 15. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... au sharti awe amefaulu/afaulu mtihani wa Mathematics
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Usikurupuke kama Makamba...
  Soma post zangu zoote uone kama nimewataja waganga.
  Au soma post yangu yoyote kama utaona nimesapoti swala la kuchinja Mtu.

  Mimi nimezungumzia swala langu binafsi la Imani na kuabudu...
  Je watanzania hizo mnazoabudu ni Imani zenu za tangu na tangu?
  Na je hayo mnayoabudu sasa mliyaabudu tangu enzi na enzi?
  Ziko wapi imani zenu?

  Hayo ya waganga na kuchinjana siyafahamu.

  So kama huna cha kuandika basi ni bora ukachukue kopo ukachambe
   
 17. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nasikia ati huko bara kuwa waganga wanatengeneza utajiri kwa masharti usile vizuri, usivae vizuri na wala usilale mahala pazuri. Hata kama una ghorofa inabidi utenge chumba cha vumbi ulale chini. Je hii ni kweli? Kama ni kweli utajiri una faida gani?
   
 18. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #18
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Eeh! Mkuu wewe ndiye umekurupuka... Mtoa mada hajataja misikiti, makanisa wala watu kuabudu jua au miti.. ametoa mifano ya uchunaji ngozi, viungo vya albino, watoto wachanga na njiti, vijana kumwingilia mnyama kwa maelekezo ya mganga nk. Sasa hiyo hasira yako mkuu imetoka wapi??? Wewe UNAKUBALIANA NA HIVYO VITENDO???
   
 19. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi sikubaliani na hayo uliyoyaorodhesha na wala hii imani ambayo ninayo haituruhusu kufanya hayo.
  Ila mimi nimesimama kwenye imani ya mababu niliyonayo...
   
 20. Mwelewa

  Mwelewa JF-Expert Member

  #20
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 2,312
  Likes Received: 2,522
  Trophy Points: 280

  Mr Kijoka nadhani hujaelewa mtoa mada anachozungumzia, maana point zako zinalenga kumkabili bila yakuelewa anacho maanisha, nadhani point sio kukashifu imani za watu wala kuziona hazifai ila swala muhimu hizo imani zina uelekeo mzuri kwa jamii? Hebu fikiri mtu anakutwa na ngozi ya mwanadamu mwenzake je hiyo imani ni sawa?
  Kamwe hatuna mamlaka ya kuingilia imani za watu ila na wao imani zao hazina mamlaka ya kuifanya jamii iwe na hofu kwao,,, uchawi wa kukata viungo vya binadamu mwenzako huo ni upuuzi tena ni zama za giza kabisa!
   
Loading...