Ushirikina michezoni: Ni dhana halisi ama ya kufikirika? Ukweli ni upi?

Mkuu mimi nimeacha kukuchukulia poa kabisa tangu Jumapili,iwe kwenye mada za soka au siasa.Na ule ushauri wako kwa Simba ulifaa sana na inabidi waendelee kukuconsult ili wasonge mbele zaidi.

Ila naomba muongeze na kitengo cha kuwashughulikia (kwa kipigo au namna yoyote) mashabiki wa Yanga wanaojitolea kuihujumu Simba SC kwenye michuano ya kimataifa,kama mlivyowafanya Jumamosi.Yaani hawakuridhika kuishangilia Nkana hadi wakaamua kuisaidia "kiufundi" utafikiri nao wanatoka Zambia?
 
Kinachimbiwa kitu golini kiasi kwamba golikipa anaona tu kivuli cha mpira tu . Anakaba kivuli na mpira wa kweli unapita . Hujawahi kuona goli linaingia kimaajabu ? Mpira ni uchawi wa ajabu , angalia hata no 11 ya wachezaji !
 
Wakuu,kuna wakati nilikuwa siamini kwamba uchawi au ushirikina upo,hadi pale 'wasimamia kucha' hao walipoanza ku-deal na maisha yangu ndo nikaamini uwepo wa wachawi/washirikina.

Wengi wanaokanusha uwepo wa mambo hayo,wanafanya hivyo kwavile hawajawahi kuwa victims/ exposed kwa mambo hayo.

Tukiachana na hayo,kuna dogo mmoja ambaye ni mchezaji wa timu moja ya ligi daraja la kwanza aliniambia jinsi ambavyo ushirikina uliwasaidia kushinda mechi.Mganga aliwaambia mechi ile ingekuwa ngumu,lakini atawasaidia kushinda kwa kuwaroga wachezaji wa timu pinzani wafanye makosa ya kijinga.Na kwamba watashinda 2 - 1.

Kabla ya mechi Mganga aliwaambia;"Mtatangulia kufungwa goli 1,na mechi itakuwa ngumu sana.Baadae mshambuliaji wa timu pinzani atampiga ngumi refarii bila sababu yoyote ya msingi na atalimwa red card,kisha beki mwingine atanawa mpira ndani ya 18 na refa atatenga tuta,ambalo watafunga na matokeo kuwa 1 - 1 kuelekea first half.

Mganga aliendelea;"..kipindi cha pili,dakika za lala salama,mchezaji wenu mmoja atakwatuliwa na beki wa timu pinzani,refa atatenga faulo.Ni sharti mchezaji wenu namba 9 akapige faulo ile,tena atumie mguu wa kulia.Na kabla hajapiga kuna upepo fulani utavuma ghafla ndipo apige,na mpira utazama moja kwa moja golini kuandika bao la 2".

Dogo hakuamini yaliyosemwa na mganga,lakini alistaajabu matukio yaliyosemwa sangoma yalitokea vile vile.Na wakatoka na ushindi wa magoli 2 - 1.Ilhali walikuwa wamezidiwa vibaya na wale jamaa.
 
Duu
 
.
IMG-20200110-WA0028.jpeg

Jr
 
Back
Top Bottom