Ushirikina michezoni: Ni dhana halisi ama ya kufikirika? Ukweli ni upi?

Nilijua tu hilo ndo litakuwa jibu lako!

Hamkosagi visingizio.

Uchawi haupo.
Uchawi kama upo basi tumroge JIWe
tapatalk_jpeg_1545225847540.jpeg
 
Ni mada mnyumbuliko yenye uwili wenye kusigana kinadharia, kiuhalisia na kusadikika kunakoacha maswali yenye majibu mchanganyiko....
Uchawi, upo, ushirikina upo, ulozi upo michezoni na watu wanafanya sana iwe Africa ama popote duniani, haya mambo yapo na yanafanyika sana... Shida ipo kwenye ufanisi na matokeo.. Ufanisi mara nyingi huwa ni chini ya asilimia 50 na matokeo pia huwa ni ya kubahatisha...

Kwanini iwe hivi?
Nakufundisha upate kuelimika... Uwe mwerevu na stadi usiyumbishwe ukayumba ushindwe kujua ukweli ni upi.... Usibaki na kizungumkuti....
Uchawi na mambo yote ya kishirikina vipo sana, baadhi ya mataifa huita mambo ya kitamaduni ama sayansi ya kiza... Ila kinachochangia ufanisi na matokeo kuwa hafifu ni kwamba nguvu ya uchawi huwa haifanyi kazi kwenye wingi (in bulk) kufeli hapa huwa kwingi
Nikupe mfano rahisi uelewe... Kwenye kabumbu wanaoingia uwanjani ni wachezaji 22, 11 kila timu, kuna refa na washika bendera 4 jumla ni watu 27 hivi... Hawa wote wana roho na kati yao kuna baadhi wamejizindika tayari hata nje tu ya michezo na roho zao zinatofautiana nguvu...
Formula ya uchawi ni kama miguu lazima ilingane ama kama matairi ya gari lazima yawe sawa... Kukiwa kuna utaofauti mambo hayaendi... Kwahiyo hata uchawi husika Utakuwa na nguvu lakini hautafanya kazi vizuri kutokana na nguvu tofauti tofauti utakaokutana nazo
Sasa basi nini kinafanyika? Ili uchawi uwe na matokeo yenye ufanisi tarajiwa inabidi uwekezwe/uwekwe kwa mtu mmoja tu.... Ni watu gani wanaolengwa basi
. Kipa
. Refarii
. Goli
. Mshambuliaji
. Mkabaji
. Mfungaji
Ni vigumu sana kuuroga mpira kwakuwa hupita kwenye miguu mingi ambayo yote ni miguu yenye viumbehai vyenye roho.... Kwahiyo hata kama timu nzima itapelekwa kwa sangoma lakini kuna key figures ndio hutiliwa maanani.....
Kwakuwa mpira ni magoli, na ili goli liingie inabidi mpira umpite mlinda goli na ili goli lithitibite linahitaji maamuzi ya refa kwa sehemu basi wafanyiwa dawa maranyingi huwa refa, golikipa na goli.... Chunguza utaona....

Nb. Mada hii ni kwa mtazamo wa kabumbu kwenye dhana nzima ya ushirikina michezoni
FB_IMG_1545554372013.jpg
 
Kuujua uchawi kuna raha na radha yake ambayo haielezeki, niliwahi kushuhudia kwa macho yangu jinsi wachawi (warogi) wanavyoshiriki chakula kinacholiwa na watu wengi.
.
Pindi utakapowaona hairuhusiwi kushituka wala watakavyokuwa wanakuletea madole yao machoni mwako usikwepe kufanya hivyo kuliniepusha na kisanga ambacho kingenitesa maisha yangu yote.
.
Wachawi wote SHIKAMONI
Duh!
 
CC : The Sun-of-a beach
Kule kwenye Jukwaa la Michezo kuna mtu anaitwa GENTAMYCINE alishauri mambo kadhaa ya "utaalamu wa giza" kama sehemu ya maandalizi ya Simba SC ili iifunge Nkana FC.

Nakumbuka alisisitiza,kocha asiache kumpanga Jonas Mkude,na pia Jonas Mkude akubali kubeba "mzigo" wa timu nzima maana yeye ndie mchezaji pekee ambaye nyota yake ilikuwa inang'aa kwa 100% siku chache kabla ya mechi (na huyu Mkude mara nyingi amekuwa akiwagomea viongozi kumbebesha hivyo vitu).

Sijui mdogo wangu Jonas alikubali?maana nilishangaa kumwona akifunga goli murua la kwanza,na baada ya hapo milango ya ushindi wa Simba ikafunguka.
 
Endeleeni tu kumchukulia ' Poa ' GENTAMYCINE. Na sikuishia hapo bali NILITAHADHARISHA pia katika huo huo ' Uzi ' kuwa kuna jambo la Kushtua na Kusikitisha litatokea ama kabla ya mchezo kuanza au wakati wa mchezo ila Mashabiki ' wasiogope ' kwahiyo hilo jambo ndilo litatusaidia katika ' Ushindi ' wetu na kweli likatokea. Rest In Peace Marehemu Kessy Rajab. Na Mdogo wangu Mkude ndiyo ' alibebeshwa ' mtambo wa ' Kiasili ' siku ile japo kuna baadhi ya Watu walitaka ' abebeshwe ' Okwi ila kwa Siku husika ' nyota ' yake ilikuwa siyo nzuri lakini kwa Mkude ilikuwa 100% sahihi kwa Kutufanikishia furaha tuliyoipata japo pia imetuachia ' Huzuni / Simanzi ' hiyo.
 
Mkuu mimi nimeacha kukuchukulia poa kabisa tangu Jumapili,iwe kwenye mada za soka au siasa.Na ule ushauri wako kwa Simba ulifaa sana na inabidi waendelee kukuconsult ili wasonge mbele zaidi.

Ila naomba muongeze na kitengo cha kuwashughulikia (kwa kipigo au namna yoyote) mashabiki wa Yanga wanaojitolea kuihujumu Simba SC kwenye michuano ya kimataifa,kama mlivyowafanya Jumamosi.Yaani hawakuridhika kuishangilia Nkana hadi wakaamua kuisaidia "kiufundi" utafikiri nao wanatoka Zambia?
 
Back
Top Bottom