Ushirikina michezoni: Ni dhana halisi ama ya kufikirika? Ukweli ni upi?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Ni mada mnyumbuliko yenye uwili wenye kusigana kinadharia, kiuhalisia na kusadikika kunakoacha maswali yenye majibu mchanganyiko....
Uchawi, upo, ushirikina upo, ulozi upo michezoni na watu wanafanya sana iwe Africa ama popote duniani, haya mambo yapo na yanafanyika sana... Shida ipo kwenye ufanisi na matokeo.. Ufanisi mara nyingi huwa ni chini ya asilimia 50 na matokeo pia huwa ni ya kubahatisha...

Kwanini iwe hivi?
Nakufundisha upate kuelimika... Uwe mwerevu na stadi usiyumbishwe ukayumba ushindwe kujua ukweli ni upi.... Usibaki na kizungumkuti....
Uchawi na mambo yote ya kishirikina vipo sana, baadhi ya mataifa huita mambo ya kitamaduni ama sayansi ya kiza... Ila kinachochangia ufanisi na matokeo kuwa hafifu ni kwamba nguvu ya uchawi huwa haifanyi kazi kwenye wingi (in bulk) kufeli hapa huwa kwingi
Nikupe mfano rahisi uelewe... Kwenye kabumbu wanaoingia uwanjani ni wachezaji 22, 11 kila timu, kuna refa na washika bendera 4 jumla ni watu 27 hivi... Hawa wote wana roho na kati yao kuna baadhi wamejizindika tayari hata nje tu ya michezo na roho zao zinatofautiana nguvu...
Formula ya uchawi ni kama miguu lazima ilingane ama kama matairi ya gari lazima yawe sawa... Kukiwa kuna utaofauti mambo hayaendi... Kwahiyo hata uchawi husika Utakuwa na nguvu lakini hautafanya kazi vizuri kutokana na nguvu tofauti tofauti utakaokutana nazo
Sasa basi nini kinafanyika? Ili uchawi uwe na matokeo yenye ufanisi tarajiwa inabidi uwekezwe/uwekwe kwa mtu mmoja tu.... Ni watu gani wanaolengwa basi
. Kipa
. Refarii
. Goli
. Mshambuliaji
. Mkabaji
. Mfungaji
Ni vigumu sana kuuroga mpira kwakuwa hupita kwenye miguu mingi ambayo yote ni miguu yenye viumbehai vyenye roho.... Kwahiyo hata kama timu nzima itapelekwa kwa sangoma lakini kuna key figures ndio hutiliwa maanani.....
Kwakuwa mpira ni magoli, na ili goli liingie inabidi mpira umpite mlinda goli na ili goli lithitibite linahitaji maamuzi ya refa kwa sehemu basi wafanyiwa dawa maranyingi huwa refa, golikipa na goli.... Chunguza utaona....

Nb. Mada hii ni kwa mtazamo wa kabumbu kwenye dhana nzima ya ushirikina michezoni
 
Kuujua uchawi kuna raha na radha yake ambayo haielezeki, niliwahi kushuhudia kwa macho yangu jinsi wachawi (warogi) wanavyoshiriki chakula kinacholiwa na watu wengi.
.
Pindi utakapowaona hairuhusiwi kushituka wala watakavyokuwa wanakuletea madole yao machoni mwako usikwepe kufanya hivyo kuliniepusha na kisanga ambacho kingenitesa maisha yangu yote.
.
Wachawi wote SHIKAMONI
 
Du umenikumbusha wimbo wa Afande Sele kabla hajawa "MGAMBO SELE".

"Tatizo kuna viongozi,wanaendekeza nguvu za giza kuliko pumzi,mpira ni mazoezi mchezaji hafanyi mazoezi kwenye mechi unampanga kisa anashika hirizi,katikati ya dimba anachimba anafukia mbuzi,kwa nguvu za shetani hatuwezi kuona ushindi pasipo ufundi hata tunywe damu ya bundi."
 
Mkuu nadhan ungeongeza nyama kidogo

Back
Top Bottom