Ushirikina & Mawazo ya Uharibifu : Ni Utamaduni wa Mtanzania?

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,078
2,443
Wakuu::

Baada ya Miaka 15 ya kuchapa kazi, Baba_Enock ameweza kujenga vyumba viwili maeneo ya Buza na sasa amehamia huko na anaishi na familia yake raha mustarehe!

Takribani miezi miwili hawa majirani zangu ambao wengi wao wanaonekana kuwa maeneo hayo kwa miongo mingi wamekuwa wakifanya vitimbi na vituko vingi ambavyo kwa uhakika sijui vinaashiria nini?

1 .. Kila siku usiku lazima majirani wafanye "patrol" kuzunguka "nyumba" na kusikiliza nini kinaendelea ndani kwangu!

2 .. Kila siku asubuhi lazima nikute mifuko ya "rambo" kadhaa iliyojaa vinyesi ndani ya uwanja wa nyumba yangu!

3 .. Kila siku "barabara" inayoelekea nyumbani kwangu lazima utakuta kuna mashimo yanayochimbwa aidha usiku wakati nimelala au mchana wakati sipo nyumbani!

4 .. Kila siku muda wa "kulala" wa hawa majirani zangu sio kabla ya saa nane usiku!

5 .. Kila wiki lazima majirani zangu hawa wana sherehe ya aina fulani na hizi sherehe zinakesha!

Nikijumlisha yote haya naona kuna hali fulani ya hawa majirani kutaka kuharibu na kukatisha tamaa maisha ya Baba_Enock and Co..

Sasa najaribu kuuliza ni kwanini Wa-Tanzania wanatabia ya kupenda "kuharibu" na "kukatisha tamaa" maendeleo ya mtu mwingine badala ya kusaidi "kuonyesha njia" na "kutia moyo" watu wanaonyesha nia ya kutaka kubadilisha maisha yao kuwa bora?

Je hii tabia ya kutaka "kuharibu" au "kuvuruga" ni "Utamaduni Wetu"?

Nawasilisha

BE
 
Njoo ufanyiwe maombi baba Enock. Hao watu wanataka kukunanihii umwache mkeo na Enock wakusaidie kuwatunza
 
Watu kama hao wapo sana katika jamii yetu, ni watu wenye wivu na roho mbaya. Wengine ni washirikina na wengine sio lakini cha msingi jihadhari nao saana majirani zako sio watu wema kwako hata kidogo. chunga sana vyakula na maji watakuja kukuwekea sumu au kukudhuru kuwa mwangalifu sana Baba Enock
 
umesahau na WIZI ni tabia ya watanzania.wee subiri utakaribishwa kwa kuibiwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom