Ushirikina kuanzia Kura za Maoni hadi Uchaguzi Mkuu

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,427
Wakuu,

Kama mnavyojua hiki ndio kipindi kigumu kwa wanasiasa wengi wenye tamaa za madaraka na hasa ambao kwao madaraka ni fursa binafsi ingawa mbele ya hadhara hujinasibu kama lengo ni utumishi wa wananchi.

Kipindi hiki ndio huwa neema kwa waganga wa kienyeji, makafara ya kila namna na matumizi ya fedha makubwa kuhakikisha wanapata wanachotaka na si kutumwa na wananchi. Ni wanasiasa wachache ambao tegemea lao ni Mungu pekee

Kwa wanasiasa ambao tegemeo lao ni Mungu pekee watambue wanaingia vitani si na wanasiasa wenzao tu bali baadhi ya wanasiasa wenzao wenye connections zinazosindikizwa na falme za giza. Hivyo ni vizuri pia na wewe kukaa mkao wa kivita ukivaa silaha zote za vita za kiroho

Kwa ufupi ukitaka kubakia salama lazima ujikabidhi kwa Mungu bila mawaa. Kama ni Mkristo ni kukaa katika toba na maombi bila kukoma. Ukiweza usikose misa kila siku na kushiriki Ekaristi bila kukosa

Kila aliyechukua form ni haki yake kushiriki na nafikiri badala ya kubeza watu wengi kujitokeza tunapaswa kuchukulia kama ni afya njema kidemokrasia.

Kwa wale watia nia ambao wanataka moto na nguvu ya maombi katika safari yao hii karibuni sana kuanzia leo tar 17-26 July kwenye kongamano kubwa la Roho Mtakatifu litakalofanyika viwanja vya Emaus Ubungo ambalo limeandaliwa na Karistimatiki Katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam. Kongamano hilo litarushwa live Tv na Radio Tumaini, Tv na radio Upendo kuanzia saa nane mchana.

Soma hili tangazo kwa taarifa zaidi.

IMG-20200717-WA0001.jpg
 
Umeupa promo sana ushirikina kuliko hata hilo kongamano, unathibitisha jinsi shiriki ilivyo na nguvu kuliko dini.
 
Mkuu nimestaajabu sana leo!

Kumbe unakuwaga ni mtu wa dini?

Any way, yote kwa yote, lakini ulichoongea ni madini tupu, ndiyo uhalisia wa mambo utakavyokuwa, ni vita kubwa sana hii watu wanaenda kupigana.
 
Atakama hawajamuamini kristo waje tu, wakipata ubunge wanaendelea na yesu au wanasubili homa ya miaka mitano ijayo
 
samahani mkuu, hivi kuna mwanasiasa anaemtegemea Mungu hapa Tanzania?.........


unaweza kumtaja/kuwataja?.......
 
samahani mkuu, hivi kuna mwanasiasa anaemtegemea Mungu hapa Tanzania?.........


unaweza kumtaja/kuwataja?.......
Mkuu kwasisi Wakatoliki kuna kipengele Padre anapohadhimisha Ekaristi huwa anasema kwa nukuu isiyo rasmi ..."Bwana uwahurumie hawa watumishi wako ambao imani yao WEWE pekee waijua" ....
 
Back
Top Bottom