Ushirikina katika nyumba za kupanga: Nipo katika mtihani mzito, ushauri wako ni muhimu

Hellow wana bodi,

Mimi ni mpangaji wa nyumba, tupo familia tofauti tofauti 5. Katika nyumba hii tunayoishi mimi na wapangaji wenzangu hatukai na mwenye nyumba yeye anakaa mbali kabisa na sisi.

Kwa bahati mbaya/nzur alinichaguwa kama mwangaliz wa nyumba yake. Kwa maana ya kuandikia watu mikataba, kukusanya kodi, kumhamisha yeyote asiye endana na utaratibu tuliojiwekea.

Sasa kuna familia moja ina amini mambo ya kishirikiana sana, huwa inaleta waganga sana hapa nyumbani. Nadhan mnajua mambo ya kiganga yanavyokuwa, ni kuchoma choma miubani hovyo n.k

Sasa nilikuwa nawachunia maana hapa ni mjin na kila mmoja anapambana na hali yake. Kwahyo sina sababu ya kufuatilia fuatilia mambo ya watu sana, japo inaleta kero sana kwa wapangaji wengine.

Leo nikiwa nje ya nyumbani safarini. Alinipigia mwenye nyumba(landlord) akiniuliza upo wapi? Uko nyumbani? Nilimjibu sipo home akaniambia poa.

Akafunga safari akaja kwenye nyumba yake akakuta yule mpangaji anachoma ubani kama anachoma shamba la bangi vile, waganga wananena kwa lugha ambazo hata hazieleweki. Alipofika kwa mujibu wa nilivyoelezwa waganga walisitisha zoezi na mwenye nyumba kugomba sana na kuondoka baadaye akaniambia waandikie notis hao watu waondoke.

Ushauri wadau!
Mbona hata wewe mshirikina tu
 
sasa unaogopa nn kufanya ulichoagizwa na mwenye nyumba ushapata ushauri tayar
 
Saidia kufukuza wote hao, waende wakafukize kwao au kwa wafukizaji wenzao, imani chafu sana hizo..
 
Kwani nawe huwa unalipa kodi au una offer ya usimamizi? Jibu kwanza hilo
 
Back
Top Bottom