Ushirikina katika nyumba za kupanga: Nipo katika mtihani mzito, ushauri wako ni muhimu

Hapa mwenye nyumba kuna jambo analikwepa kwanin asiandike yey
mwambie awape mwenyewe lasivyo utavunjwa mguu wa tatu ohoooo
 
Mwenye nyumba mwenyewe kaogopa msala we unajitia kakupa cheo, tuambie unaish wapi mana ukiandka tu leo hakuchi tumeanza kukusanya rambirambi jf
 
Wewe umepewa amri halafu unaomba ushauri, unataka kumpundua mwenye nyumba? Afanya uliyoagizwa.
 
Kama anakupunguziaga kodi kwa kazi hizo unazomfanyia basi Andika hiyo notice.kama la angalia kwanza kodi uliyolipa kama Ina muda marefu wa kuisha .Mwombe mwenye nyumba aandike hiyo notice nawe utaiwakilisha.Mweleze kweli tuu kuwa mko jirani na mhusika na upo uwezekano wa kuathiriwa kwa malipizo.
 
Hellow wana bodi,

Mimi ni mpangaji wa nyumba, tupo familia tofauti tofauti 5. Katika nyumba hii tunayoishi mimi na wapangaji wenzangu hatukai na mwenye nyumba yeye anakaa mbali kabisa na sisi.

Kwa bahati mbaya/nzur alinichaguwa kama mwangaliz wa nyumba yake. Kwa maana ya kuandikia watu mikataba, kukusanya kodi, kumhamisha yeyote asiye endana na utaratibu tuliojiwekea.

Sasa kuna familia moja ina amini mambo ya kishirikiana sana, huwa inaleta waganga sana hapa nyumbani. Nadhan mnajua mambo ya kiganga yanavyokuwa, ni kuchoma choma miubani hovyo n.k

Sasa nilikuwa nawachunia maana hapa ni mjin na kila mmoja anapambana na hali yake. Kwahyo sina sababu ya kufuatilia fuatilia mambo ya watu sana, japo inaleta kero sana kwa wapangaji wengine.

Leo nikiwa nje ya nyumbani safarini. Alinipigia mwenye nyumba(landlord) akiniuliza upo wapi? Uko nyumbani? Nilimjibu sipo home akaniambia poa.

Akafunga safari akaja kwenye nyumba yake akakuta yule mpangaji anachoma ubani kama anachoma shamba la bangi vile, waganga wananena kwa lugha ambazo hata hazieleweki. Alipofika kwa mujibu wa nilivyoelezwa waganga walisitisha zoezi na mwenye nyumba kugomba sana na kuondoka baadaye akaniambia waandikie notis hao watu waondoke.

Ushauri wadau!
hahahahaa unaogopa
 
Hii inanikumbusha rafki yangu alilala asubuhi kuamka akajukuta kanyolewa nywele kidogo kichwani
Alichokifanya aliwaita wapangaji wenzake woote na kuwaambia”HATA MNINYOE KIPARA MIMI KTK HII NYUMBA SIHAMI NG’OO,,!!!”
 
Hellow wana bodi,

Mimi ni mpangaji wa nyumba, tupo familia tofauti tofauti 5. Katika nyumba hii tunayoishi mimi na wapangaji wenzangu hatukai na mwenye nyumba yeye anakaa mbali kabisa na sisi.

Kwa bahati mbaya/nzur alinichaguwa kama mwangaliz wa nyumba yake. Kwa maana ya kuandikia watu mikataba, kukusanya kodi, kumhamisha yeyote asiye endana na utaratibu tuliojiwekea.

Sasa kuna familia moja ina amini mambo ya kishirikiana sana, huwa inaleta waganga sana hapa nyumbani. Nadhan mnajua mambo ya kiganga yanavyokuwa, ni kuchoma choma miubani hovyo n.k

Sasa nilikuwa nawachunia maana hapa ni mjin na kila mmoja anapambana na hali yake. Kwahyo sina sababu ya kufuatilia fuatilia mambo ya watu sana, japo inaleta kero sana kwa wapangaji wengine.

Leo nikiwa nje ya nyumbani safarini. Alinipigia mwenye nyumba(landlord) akiniuliza upo wapi? Uko nyumbani? Nilimjibu sipo home akaniambia poa.

Akafunga safari akaja kwenye nyumba yake akakuta yule mpangaji anachoma ubani kama anachoma shamba la bangi vile, waganga wananena kwa lugha ambazo hata hazieleweki. Alipofika kwa mujibu wa nilivyoelezwa waganga walisitisha zoezi na mwenye nyumba kugomba sana na kuondoka baadaye akaniambia waandikie notis hao watu waondoke.

Ushauri wadau!
Si umeona ugumu wa kazi aliyokupa mwenye nyumba?Mwambie hiyo kazi huiwezi,asimamie nyumba yake mwenyewe au achague mtu mwingine.Ulidhani dili,pole.
 
Back
Top Bottom