Ushirikina katika nyumba za kupanga: Nipo katika mtihani mzito, ushauri wako ni muhimu

Wild fauna

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
460
250
Hellow wana bodi,

Mimi ni mpangaji wa nyumba, tupo familia tofauti tofauti 5. Katika nyumba hii tunayoishi mimi na wapangaji wenzangu hatukai na mwenye nyumba yeye anakaa mbali kabisa na sisi.

Kwa bahati mbaya/nzur alinichaguwa kama mwangaliz wa nyumba yake. Kwa maana ya kuandikia watu mikataba, kukusanya kodi, kumhamisha yeyote asiye endana na utaratibu tuliojiwekea.

Sasa kuna familia moja ina amini mambo ya kishirikiana sana, huwa inaleta waganga sana hapa nyumbani. Nadhan mnajua mambo ya kiganga yanavyokuwa, ni kuchoma choma miubani hovyo n.k

Sasa nilikuwa nawachunia maana hapa ni mjin na kila mmoja anapambana na hali yake. Kwahyo sina sababu ya kufuatilia fuatilia mambo ya watu sana, japo inaleta kero sana kwa wapangaji wengine.

Leo nikiwa nje ya nyumbani safarini. Alinipigia mwenye nyumba(landlord) akiniuliza upo wapi? Uko nyumbani? Nilimjibu sipo home akaniambia poa.

Akafunga safari akaja kwenye nyumba yake akakuta yule mpangaji anachoma ubani kama anachoma shamba la bangi vile, waganga wananena kwa lugha ambazo hata hazieleweki. Alipofika kwa mujibu wa nilivyoelezwa waganga walisitisha zoezi na mwenye nyumba kugomba sana na kuondoka baadaye akaniambia waandikie notis hao watu waondoke.

Ushauri wadau!
 

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,578
2,000
Vyuma vimekaza hadi kwenye uandishi!?

Aiseeeeh kazi Kweli Kweli.
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,888
2,000
..mwenye nyumba kugomba sana na kuondoka baadaye akaniambia waandikie notis hao watu waondoke. Ushauri wadau!
Unataka ushauri upi wakati Landlord keshafanya maamuzi? kama unaamini mambo hayo na unaogopa ''scud'' la waganga lisikurudie, msaidie landlord kudraft notisi then aje aitoe mwenyewe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom