Ushirikina huu kiboko! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushirikina huu kiboko!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Faith, Aug 6, 2008.

 1. Faith

  Faith Member

  #1
  Aug 6, 2008
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  from
  http://www.lukwangule.blogspot.com


  ushirikina wachakaza sarafu za Tanzania

  Ubora wa sarafu ya Tanzania katika mzunguko unaathiriwa na imani za kichawi ambapo nyingi ya sarafu hizo huharibika kutokana na kutumbukizwa katika mapipa ya pombe kwa lengo la kuvutia wanywaji.
  Matukio ya imani za aina hiyo yapo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
  Msimamizi wa kitengo cha fedha cha benki kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Vicenti Mtani amesema kwamba imani hizi za kishirikina ambazo zinaharibu sarafu ya shilingi mia na shilingi hamsini pia huharibu noti za shilingi mia tano ambazo huchanwa kidogo pembeni kuzuia mtu mwingine kuchukua fedha za yule anayetoa noti hiyo asizichukue kiuchawi.
  Ofisa huyo ambaye alinukuliwa mjini hapa katika banda la maonyesho la nanenane na mwandishi Rashid Mwinda wa Majira amesema kwamba imani hizo za kishirikina zinachakaza sarafu kwa kasi na kusababisha hasara katika uchumi wa nchi.
  Amesema niu gharama kubwa kurejesha sarafu na noti hizo katika mzunguko kwani zinatakiwa kutengenezwa upya na kuliiingizia taifa hasara.
  Afisa huyo alikuwa akielezea matumizi bora ya fedha katika maonyesho hayo ya nanenane kwa kulingana na utafiti ambao tayari benki hiyo umeufanya.
  Amesema kwamba watu wanaamini kwamba madini yaliyotumika katika kutengeneza sarafu yana mvuto mkubwa kwa watumiaji pombe ikiwa na kuifanya kuwa kali na kuvutia.

  Aidha inaaminika kuwa fedha hizo pia zikitumika katika chungu cha kuuzia huvutia wateja

  kwa kweli hii kali!kwa dunia ya leo hii!
   
 2. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  hizo pesa kwanza utangenezaji wake ni mbovu ... karatasi zenyewe hafifu si tatizo la uchawi kama uchawi ni wa enzi na enzi .... hela zinachakaa zenyewe kwa uhafifu wake ..
   
 3. k

  kalld Member

  #3
  Aug 6, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna mambo ya ajabu ukisoma mambo ya bongo ! hebu angalia hiii!
  Chuma ulete yazua songombingo Dar, Wakimbiza pesa benki kwa hofu  *Wakimbiza pesa benki kwa hofu

  Na Adam Hussein

  MZOZO mkubwa huenda ukazuka kati ya baadhi ya wenye nyumba na wapangaji katika maeneo mbalimbali wilayani Temeke huku wapangaji wakidai kuwa wenye nyumba wanaingia mifukoni mwao kwa kutumua juju na kuchomoa pesa zao kimiujiza kwa mtindo unaojulikana zaidi kama chuma ulete.

  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba baadhi ya wapangaji katika maeneo ya Kigamboni, Mtoni na Yombo wamekuwa kwenye mzozo mkubwa na wenye nyumba kwa imani kuwa wanaibiwa pesa zao kimiuijiza na kuwaacha kwenye lindi la umaskini.

  Baba mmoja anayeishi Kigamboni aliyeomba jina lake lisitajwe kwa hodu ya kutimuliwa kwenye nyumba amedai, anashangazwa na mzee mwenye nyumba ambaye amekuwa akifukiza madawa fulani ndani ya nyumba na kusababisha baadhi yao kuhama kwa kuhofia pesa zao zisichukuliwe.

  "Kila anapofukiza dawa hizo, utakuta mpangaji yoyote akiingia na pesa na kuziweka nyumbani, zinapotea katika mazingira ya kutatanisha au matumizi yasiyojulikana na kujikuta pesa inakwisha haraka," amelalamika na kuongeza: " "Lakini asipofukiza dawa utakuta pesa inatulia na unaweza kufanya mambo ya maana."

  Akadai kuwa baba huyo ana wake wawili hana kazi na familia inakula na inalala na si kwamba ana watoto wakubwa wanaomsaidia kwani yeye anashinda amekaa akicheza bao katika vijiwe vya eneo hilo na muda wa chakula ukifika anakula na kulala.

  Hofu hiyo ya kupoteza pesa kwa njia hiyo sasa imewafanya wakazi wengi wa jiji kukimbilia benki mara tu wanapopokea mishahara au malipo yoyote kutokana na biashara zao wakidai kwamba wanazinusuru na wenye nyumba wajanja.

  Mama mmoja ambaye amejitambulisha kwa jina la Apronia amesema: "Ilibidi niende kwa mganga ili atambue nini kinachofanya nishindwe kufanya maendeleo wakati nina uwezo wa kuingiza pesa za kutosha ambazo zinaweza kunipa maendeleo makubwa. Mganga alinishauri nihame nyumba na nikaanza kupata maendeleo."

  Hamza Jumanne anayeishi katika Nyumba za Tazara Temeke anashangazwa na matumizi ya pesa siku hizi. "Tuko watu watano kwenye familia ila nikipata shilingi elfu hamsini Ijumaa nikifika Jumatatu ninakuwa sina kitu. Sio bure, naona tunachezewa," amedai.

  Mkazi wa Kurasini, Joseph Mlawa amekana akisema kwamba chuma ulete ni imani za watu ambao hawajui kwamba kutokana na mfumuko wa bei pesa inatumika nyingi kununulia vitu vichache.

  "Hapa hakuna mchawi. Ni kupanda tu kwa hali ya maisha kwa sababu kama mwaka jana ulitumia sh 10,000 kununua vitu vitano, leo utatumia pesa hiyo kununua vitu viwili vitatu tu. Kama ni chuma ulete inaletwa na hali ya uchumi na wala siyo wenye nyumba," amesema Mlawa.

  Amesema kuwa wanaoamini kwamba kuna chuma ulete wanashindwa kwenda na wakati na kufuatilia vizuri mabadiliko ya bei za vitu, mapato na matumizi yao nyumbani na nje ya nyumba.

  "Kila siku tunaambiwa shilingi inashuka thamani maana yake ni kwamba unatumia pesa nyingi kununua vitu vichache tu. Hebu angalia kwa sasa nauli zinapanda, vinywaji vinapanda, mboga zinapanda, dawa zinapanda na hata hao waganga wanaotuambia kuna chuma ulete wamepandisha dau. Nasema chuma ulete ipo kwenye hali halisi ya maisha lakini siyo wenye nyumba," amesisitiza.
  Imani kwamba kuna chuma ulete inazidi kuota mizizi hasa jijini Dar es Salaam ambapo matumizi ya pesa ni makubwa huku baadhi wakiamini kwamba wanachomolewa pesa kwa kutumia madawa na wengine wakiamini kwamba kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma ndiko kunasababisha hali hiyo.
  source:dar leo
   
 4. k

  kalld Member

  #4
  Aug 6, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shule ya biashara/uchumi kwa raia ni muhimu sana
   
 5. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  kusema ukweli imani hizi za kishirikina ndio zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu katika maeneo ya vijijini, maana watu wanashindwa kufanya vitu vya maana kwa kuogopa ushirikina au uchawi.
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Badala ya kuzingatia usemi wa mali bila daftari hupotea bila habari...Wao wanabaki kuwalaumu popobawa tuu!
   
Loading...