Ushirikiano wa China na Afrika wa “Ukanda Mmoja Njia Moja” wapaswa kulindwa sio kudhalilishwa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
微信图片_20210427161413.jpg
Gazeti la Financial Times la Uingereza limetoa makala likilitilia mashaka Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” BRI na kusema uwekezaji wa China katika sekta ya miundombinu barani Afrika “unakaribia kukauka”. Makala hiyo pia imemnukuu afisa mmoja wa Afrika Kusini akisema nchi za Afrika zinapaswa kusaini makubaliano na China, sio BRI.

Hii si mara ya kwanza kwa vyombo vya habari vya magharibi kuusemea vibaya ushirikiano wa China na Afrika chini ya pendekezo la BRI. Vikiwa na nia mbaya, mwaka 2013 wakati BRI ilipoanzishwa, vilisema China inafanya njama na kutoa vitisho kupitia pendekezo hilo, kisha vilisema BRI ni “mtego wa madeni”, na sasa vinatia chumvi changamoto za kifedha zinazosababishwa na janga la COVID-19 kwenye ushirikiano wa China na Afrika chini ya BRI. Lakini kama alivyosema mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa China na Afrika kilicho chini ya Chuo Kikuu cha Johannesburg, Afrika Kusini Bw. David Monyae, hivi ndivyo jinsi vyombo vya habari vya magharibi kwa muda mrefu vinavyotumia kuharibu ushirikiano kati ya China na Afrika likitajwa suala la maendeleo ya nchi.

Ushirikiano wa China na Afrika katika miaka kadhaa iliyopita umeonesha kuwa pendekezo la BRI lililotolewa na China linaendana na malengo ya nchi za Afrika ya kupunguza umaskini na kutafuta maendeleo. Umoja wa Afrika umetunga Ajenda 2063, ili kutimiza malengo ya maendeleo, nchi za Afrika zinatakiwa kujenga miundo mbinu kama vile bandari, barabara kuu na viwanja vya ndege. Hadi kufikia mwaka 2019, uwekezaji wa moja kwa moja wa jumla wa China barani Afrika ulikuwa umefikia dola za kimarekani bilioni 49.1, ikiwa ni ongezeko la mara 100 kuliko mwaka 2000, nyingi zikiwa katika sekta ya miundo mbinu. Katika miongo hii miwili, miradi mikubwa ya miundombinu ambayo imemalizika na kuanza kutumiwa ikiwemo reli ya Mombasa-Nairobi, reli ya Addis Ababa–Djibouti na bomba la gesi asili la Tanzania imetoa mchango muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika. Na bandari ya Lamu iliyojengwa na kampuni ya China pia itaanza kutumiwa mwezi Juni mwaka huu. Bandari hiyo itashughulikia makontena na mizigo ya mafuta inayosafirishwa kati ya Afrika Mashariki na sehemu nyingine duniani, na kufanya Kenya kuwa chaguo la kwanza kwa Ethiopia, Sudan Kusini na Somalia.

Lakini kama uhusiano wowote duniani, ushirikiano wa China na Afrika wa BRI pia utashuhudia kipindi cha maendeleo ya kasi na kipindi cha maendeleo tulivu, pengine tukio la ghafla kama vile janga la ugonjwa wa COVID-19. Janga hilo limeleta madhara makubwa kwa uchumi wa dunia, na hakuna nchi inayoweza kuepukana nalo. Hata hivyo takwimu zilizotolewa mwaka huu na Wizara ya Biashara ya China zimeonesha kuwa ikiwa mwekezaji mkubwa zaidi na mwenzi mzuri wa maendeleo wa Afrika, katika miezi kumi na moja ya mwanzo ya mwaka 2020, thamani ya uwekezaji wa China barani Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 2.8, likiwa ni ongezeko la asilimia 0.04 kuliko mwaka 2019 kipindi kama hicho. Vilevile mwezi Disemba mwaka jana, China pia ilisaini makubaliano na Umoja wa Afrika kuhusu kuhimiza kwa pamoja mpango wa ushirikiano wa ujenzi kuhusu BRI ili kuunganisha pendekezo hilo na Ajenda 2063 kwa kina zaidi.

Afrika ni sehemu muhimu isiyoweza kukosekana katika pendekezo la BRI. Hivi sasa nchi za Afrika zaidi ya 40 na kamati ya Umoja wa Afrika zimesaini mikataba ya ushirikiano na China kuhusu BRI, idadi ambayo imechukua theluthi moja ya nchi na mashirika ya kimataifa yaliyojiunga na pendekezo hilo duniani. Vyombo vya habari kama Gazeti la Financial Times viliuangalia vibaya ushirikiano wa China na Afrika wa BRI, na pia havielewi kuwa pendekezo la BRI si mpango wa miaka mitano au kumi, bali ni njia ya kudumu ya kutafuta maendeleo. BRI ni pendekezo lenye unyumbufu na linaweza kuhimili changamoto mbalimbali, na kwa kuwa na mawazo yenye ubunifu na kuona mbali tu, ndio thamani yake halisi inaweza kutambuliwa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom